Je, kuna umuhimu wa upimaji wa virusi vya UKIMWI (HIV/AIDS) kuwa lazima?

Rich Hash

Senior Member
Mar 7, 2017
149
203
Je, kuna umuhimu wa Serikali duniani kote kuamua kulifanya suala la upimaji wa UKIMWI kuwa suala la lazima!

Ni suala ambalo mara kadhaa limekua likileta mjadala mkali kwa wanaoangalia maslahi ya jamii juu ya umuhimu wa kupima dhidi ya watetea haki za binadamu kuwa uamuzi huo ni kinyume na haki za binadamu.

Kufuatia takwimu za UNAIDS watu zaidi ya milioni 36.9 duniani wanaishi na maambukizi ya virusi vya UKIMWI. Takwimu hizo zinaonyesha kuwa Afrika ya Kusini ndio nchi inayoongoza kwa maambukisi hayo ikiwa na jumla ya waathirika milioni 7.2.

Zaidi ya asilimia 50 ya waathirika wa ugonjwa wa UKIMWI wa dunia nzima wanatokea Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika. Kwa hiyo linapokuja suala la upimaji wa lazima wa ugonjwa huo katika ukanda huu sio suala linalohitaji mjadala zaidi ya utekelezaji huenda ikalenda unafuu wa makali ya ugonjwa huo.

Hongera kwa wazo zuri, japo bado sijaona sababu zako za msingi.

Tofauti na haki za binadamu, ninaamini utakubaliana na mimi kuwa uwezo wa watu kuchanganua na kupokea mambo unatofautiana.

Kuna watu wakigundua kuwa wana UKIMWI wala haiwapi shida "kivile". Ila kuna wengine hali ni tofauti, hata kama wakipewa Ushauri Nasaha. Hivyo, kwa maoni yangu, ninaona suala hili libaki kuwa hiari ya mtu.

Kuna magonjwa mengi tu ambayo ni hatari sana, pengine kuzidi hata UKIMWI. Kwa mfano; Ugonjwa wa Homa ya Ini B (Hepatitis B), ni hatari mara 50 -100 ukilinganisha na UKIMWI (Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali na Shirika la Afya Duniani - WHO).

Ninafikiri magonjwa hatari kama haya, na yafananayo, ndio yangewekwa kuwa lazima. Sio UKIMWI.
 
Kosa kubwa lillofanyka n kuweka usiri kwenye matokeo ya vipimo
Kwanini watu wa kipindupindu wanatengwa na wenye HIV wanaachwa
tu waambukize wapendavyo?
 
Inabidi sasa hivi Mahospitalini kipimo cha ukimwi kiwe ni lazima mtu apimwe akienda kupima UTI, MARALIA, PRESHA au ugonjwa wowote ule apimwe na Ukimwi nadhani hapa itasaidia kupata Takwimu halisi za waathirika wa Ugonjwa huu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Je, kuna umuhimu wa Serikali duniani kote kuamua kulifanya suala la upimaji wa UKIMWI kuwa suala la lazima!"

Hakuna! Kwa sababu AIDS ni malnutrition na sio HIV. Kusini mwa jangwa la Sahara wengi wao wana Ukosefu wa Kinga Mwilini(AIDS) kutoka na lishe duni. HIV hasababishi AIDS, kwani HIV harmless kwa human body.
 
Hongera kwa wazo zuri, japo bado sijaona sababu zako za msingi.

Tofauti na haki za binadamu, ninaamini utakubaliana na mimi kuwa uwezo wa watu kuchanganua na kupokea mambo unatofautiana.

Kuna watu wakigundua kuwa wana UKIMWI wala haiwapi shida "kivile". Ila kuna wengine hali ni tofauti, hata kama wakipewa Ushauri Nasaha. Hivyo, kwa maoni yangu, ninaona suala hili libaki kuwa hiari ya mtu.

Kuna magonjwa mengi tu ambayo ni hatari sana, pengine kuzidi hata UKIMWI. Kwa mfano; Ugonjwa wa Homa ya Ini B (Hepatitis B), ni hatari mara 50 -100 ukilinganisha na UKIMWI (Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali na Shirika la Afya Duniani - WHO).

Ninafikiri magonjwa hatari kama haya, na yafananayo, ndio yangewekwa kuwa lazima. Sio UKIMWI.
 
Hongera kwa wazo zuri, japo bado sijaona sababu zako za msingi.

Tofauti na haki za binadamu, ninaamini utakubaliana na mimi kuwa uwezo wa watu kuchanganua na kupokea mambo unatofautiana.

Kuna watu wakigundua kuwa wana UKIMWI wala haiwapi shida "kivile". Ila kuna wengine hali ni tofauti, hata kama wakipewa Ushauri nasaha. Hivyo, kwa maoni yangu, ninaona libaki kuwa hiari ya mtu.

Kuna magonjwa mengi tu ambayo ni hatari sana, pengine kuzidi hata UKIMWI. Kwa mfano; Ugonjwa wa Homa ya Ini B (Hepatitis B), ni hatari mara 50-100 ukilinganisha na UKIMWI (Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali na Shirika la Afya Duniani -WHO).

Ninafikiri magonjwa hatari kama hayo ndio yangewekwa kuwa lazima. Na sio UKIMWI.
Ukimwi unashikiwa bango maana ukiwa nao watu wanajua ulifanya matusi.
 
Ukishawapima utawapa dawa za kuwaponya? Au unataka kujua takwimu tu ,Je waathirika itawasaidiaje....
 
Back
Top Bottom