Je, kuna umuhimu wa kuwa na wabunge ambao kimsingi hawatusaidii sisi wananchi!?

nsasa

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
310
413
Habar za asubuhi wanajamii forum.
Poleni na majukum ya kutafuta pesa.
Kuanzia wiki hiii kumekua na malumbano bungeni wabunge wengi wa Chama tawala wakipigia chapuo rais kuongezewa muda il aendeleze mazuri waliyoyaona wao.

Binafsi sifurahishwi kabisa na wawakilishi hawa wa wananchi kwa sababu tunayowatuma hawayasemi...hawatusemei shida zetu na matatizo tuliyowatuma wakatuwakilishe, matokeo yake wamebadili mada na kusemea matumbo yao na kujikomba kulikopitiliza kwa Rais.

Najiuliza n kwel wananchi wa CHEMBA mmemtuma Nkamia aseme Rais aongezewe Muda!?
Uropokaji na uchambaji wa KIBAJAJI...michambo ya MILINGA na wabunge wengine wa CCM, hayo ndo mliyotumwa na wananchi!?

Wabunge wa chama tawala ndo wamekua mazwazwa kulamba miguu ya watawala....na kusifia kila kitu kinachofanywa na AWAMU hii.


Je hamna namna yeyote ya kikatiba tofaut na Kura kufuta uwakilishi wao ili turud wote kitaaa waone watoto wanavopata shida kukalia mawe....wazeee wanavopata shida kupata malipo yao halali ya penshen, wajawazito wanavopata shida mahospitalin!???

Kama wanaona utendaji wa rais n wa kutukuka basi wamwache abaki yeye aongoze nchi....ila sisi hatuwataki wao kama wawakilish maana hatuioni kazi yao hata kidogo.

Warud mtaani tupambane na kuisoma namba pamoja.

Binafsi natamani BUNGE lisiwepo.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kitendo cha kumfanya Rais kuwa mwenyekiti wa chama kina athari kubwa hasa kwa wana CCM . Wabunge na wanachama watahakikisha wanajikomba vya kutosha ili kutafuta teuzi. Kwa ujumla tu ni bure kuwa na wabunge aina hii.

Mfano 2015 July Mzee Kikwete akiwa amebakiza miezi mitatu tu ofisini. Nilishangaa wabunge chini ya mama Makinda walipojikomba na kugawa gas na mafuta kwa wawekezaji bila faida yoyote kwa nchi . Haya yalifanyika ili kumfurahisha bwana mkubwa Rais

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu ni kweli uyasemayo kwasababu mara nyingi wawakilishi wetu au wabunge tunaowachagua kutoka CCM licha ya kuwasilisha haja zetu bungeni ili ziifikie serikali kama ambavyo wamekuwa wakijinadi muda wa kampeni, wakishafika bungeni wanasahau majukumu ya msingi na jukumu kubwa ambalo wanabeba ni kusifia mfumo na Serikali kwa ujumla utadhani kwamba mtu aliyepo vijijini ndani ndani huko alikuwa na haja ya kumchagua mwakilishi ili akaisifie serikali mbali na kuwasilisha kero anazokumbana nazo.

Shida nyingine ni kwamba watanzania wengi hasa tulioko huku vijijini hatuna muda wa kuwafuatilia wawakilishi wetu wawapo bungeni aidha kwa kusikiliza redio wakati au kwa njia yoyote ile ili tuweze kuwasikiliza kwa umakini na kuwatathimi ili kujua kama wamebeba dhana ya uwakilishi jambo ambalo mwisho wa siku linasababisha tuendelee kuwachagua tukiamini ipo siku watatusaidia.
 
Back
Top Bottom