Je kuna umuhimu wa kuwa na utabiri wa hali ya hewa kutoka TMA?

Top Thinker

Senior Member
Sep 8, 2011
183
125
Wote tumeshuhudia jinsi mvua na radi zilivyoleta maafa jijini dar es salaam hadi watu kupoteza maisha, lakini utabiri wa hali ya hewa kutoka tma mara baada ya taarifa za habari jana tar 19 hakuna walichosema kuhusiana na radi na mvua kali zaidi ya kusema "hali ya mawingu kiasi", sasa tutaendelea kudanganywa hadi lini?? Wangekuwa wakweli angalau ndugu zetu wa mabondeni wangechukua tahadhari.
 
wanalostishwa na wachawi wao wakitabiri kwamba mvua itanyesha wachawi wanafunga anga kwa hiyo linatoa jua tu na wakitabiri kwamba mvua haitanyesha wanashusha mvua hawa jamaa ni noma. Nitarudi baadae
 
Kutabiri mvua wakati wa masika hata mi naweza. Kesho kutakuwa na mawingu kiasi, mvua kali, jua, upepo wa rasharasha, manyunyu na joto kali. Matarajio mabadiliko kidogo.
 
hiyo idara inatakiwa kuwa mordenised
umuhimu wake utaonekana tukipata majanga makubwa zaidi mfano tsunami....

sasa hivi iko useless
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom