Mk54
JF-Expert Member
- Dec 29, 2016
- 1,997
- 3,932
Ni kwa kipindi kirefu sana tangu tuingie kwenye mfumo wa Vyama vingi. Sijawahi kuridhishwa na mfumo wa Uongozi unaoendeshwa na chama tawala.
Ni chama ambacho kila kinachofanywa ni kwa mujibu wa kisiasa; ni kipindi cha wakati huu utaona ujenzi wa barabara usio na kiwango unaendelea, viongozi wanatumbuliwa ili kuamsha hisia za wananchi (Hivi suala la Kangi Lugola limeishia wapi? Mmeshasahau?).
Ukusanyaji wa kodi umekuwa wa speed ili kuhakikisha project kubwa zinakamilika ikiwa ni pamoja na Miradi ya Chato.
Ni lazima ikamilike kipindi cha awamu ya 5; huenda Rais ajaye mwaka 2025 akaisimamisha baadhi ya miradi inayoonekana kwenda kinyume na Sheria za Manunuzi ya Umma ya mwaka 2011 na Kanuni zake za mwaka 2013 pamoja na Marekebisho ya mwaka 2016.
Pamoja na haya yote, sidhani kama kuna Mtanzania yeyote mwenye akili timamu anayetamani Chama cha Mapinduzi kitoke Madarakani; hii haimaanishi kwamba CCM wanafanya vyema; Tanzania hatujawahi kupata Upinzani wenye tija na manufaa ya Taifa.
Tuliwaamini wapinzani katika kusimamia dafina na hazina ya Taifa letu, badala yake;
· Mpinzani anaomba kununua kesi ya Tanzania na Barrick ili Tanzania ishindwe na kuliingiza Taifa katika hasara
· Mpinzani anaandika barua kwenda nchi za Magharibi ili kusimamisha msaada wa fedha za elimu za ndugu zetu wa kike ambapo kijijini kwake kuna wasichana wengi wanakaa chini ya mawe
· Wapinzani ambao wanataka maridhiano ya kisiasa huku wanasambaza sumu kwa viongozi wa kidini na kulitia Taifa letu kwenye machafuko ya kiimani
· Wapinzani ambao wanachochea maandamano kupitia Mjane anayeishi nje ya nchi ili nchi yetu imwage damu na kuingia katika historia butu
· Upinzania ambao unaitia Taifa hasara ikiwa ni pamoja na kupokea Ruzuku ambazo ni kodi za wananchi huku wao wakienda kuzitumia kwa ajili ya matumbo yao
· Upinzani ambao hauna msimamo katika kauli zao badala yake wanapokea wala rushwa na kuwapa nafasi za juu kabisa; Je tukitoa hazina na dafina ya Taifa letu itakuwaje?
Hivyo, kuna haja ya vijana kati ya miaka 30-45 mjipange na kutengeneza Upinzani usiokuwa na Tamaa, Rushwa, Ukabila, Dini na Ngono na wenye nia Thabiti ya kuingia Magogoni ili kuleta muktadha chanya kwenye Taifa la Tanzania.
Kwa upinzani upi kwa mfano utakaomfanya Rais wa sasa asiweze kushinda Uchaguzi ujao?Kwa nini tunapoteza muda na fedha wakati majibu yapo Dhahiri.
Tunachangamoto nyingi katika Afya, Miundo mbinu, Ajira, Elimu, Kilimo na mfano wake; je ni kwanini hizi fedha zisielekezwe kwenye tija? Tunafanya uchaguzi mkuu kuridhisha wazungu au kwa manufaa yetu?
Mwisho, Sikubaliani na Magufuli Katika Ubabe Wake, Kujichukulia Yupo Juu Ya Nchi. Utasikia Akisema Nita-----Nitafanya Hivi au Vile. Tanzania Ni Taifa, Haufanyi Bali Tunafanya.
Serikali Ifikirie Namna ya Kuachana na Uchaguzi Mkuu na Gharama zote Ziende Kwenye Shughuli za Maendeleo ya Taifa Letu Adhimu
Thank you.