Je, kuna umuhimu gani wa Mama kunyonyesha Mtoto wake?

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
1_20210113_134752_0000.png


Umuhimu wa kunyonyesha kwa mama ni kama ifuatavyo:-

Mama anayenyonyesha huepukana na adha za uzazi na kurejea katika hali yake ya kawaida kwa haraka na kirahisi. Hii ni kutokana na Homoni za Oxytocin ambazo hutoka wakati wa kunyonyesha zinazosaidia kurudisha mji wa mimba katika hali yake ya awali na kusaidia kukoma kwa haraka kwa damu itokayo baada ya uzazi.

Tafiti zinaonesha kuwa wanawake walionyonyesha wana uwezekano mdogo sana wa kupata Saratani ya Ovari na ya Matiti.

Vilevile Mwanamke aliyenyonyesha ana uwezekano mdogo sana kupata uzito uliokithiri na magonjwa yatokanayo na matatizo ya moyo kama shinikizo la damu na mafuta mengi mwilini.

Lakini pia, unyonyeshaji unachelewesha kurejea kwa mzunguko wa hedhi kwa mama hivyo hutoa mda kati ya mimba moja na nyingine.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom