Je, kuna ulazima wowote kuendelea kutoa matokeo ya darasa la saba kwa mfumo wa madaraja (Grades)

The lost

JF-Expert Member
Jul 3, 2017
2,695
8,209
Wakuu salaam.

Hivi majuzi baraza la mitihani la taifa (NECTA) lilitangaza matokeo ya darasa la saba. Katika matokeo hayo bado baraza limekuwa likitumia utaratibu uleule wa kutangaza shule zilizofanya vizuri, wanafunzi waliofutiwa matokeo, mikoa ilioongoza n.k. lakini jambo kubwa kabisa baraza halisemi ni somo gani Mwanafunzi wamefanya vizuri na lipi wamefanya vibaya.

Binafsi sioni umhimu wa kuto matokeo ya kijana mdogo wa darasa la saba kwa mfumo wa grade, badala yake napendekeza mfumo wao uwe wa PASS tu na kila Mwanafunzi aendelee kidato cha kwanza na utahini mkubwa ufanyike kidato cha NNE.

Ambapo hapo kidato cha NNE wanafunzi watakaofaulu vizuri wataendelea na kidato cha tano huko wakihitimu wapatiwe cheti cha high school diploma na watakao fanya vizuri waendelee na chuo kikuu.

Vijana watakaopata medium marks kidato cha NNE waende vyuo vya kati kusomea ufundi na non professional courses. Nasema non professional courses kwa maana kwamba ualimu, sheria na utabibu pamoja na uchumi zitambulike kama professional na zitolewe kwa ngazi ya shahada tu.
 
Hivi hawa waliopata grde c nao watakua wamefaulu kwenda kidato cha kwanza?
 

Attachments

  • Screenshot_2020-11-22-09-56-32.png
    Screenshot_2020-11-22-09-56-32.png
    18.5 KB · Views: 2
Sera ya elimu ya 2014 iliondoa hili kitambo. Mitaala na walimu walikuwa tayari. Elimu ya msingi ingeishia darasa la sita na hawa darasa la saba wa mwaka huu wangekuwa wa mwisho, wangeenda sekondari na wenzao wa darasa la sita mtihani wa darasa la sita ungekuwa kama wa la nne wa sasa, ukishindwa unarudia darasa.

Uncle na Ndalichako na wenzao wakakwepa gharama wakapotezea sera.

Tunahitaji mfumo ambao sera zikipitishwa isiwe rahisi kubadilisha hivi.

Hiyo sera utekelezaji ungekuwa mgumu mwanzoni lakini baadaye ingetoa majibu mengi ya matatizo yetu ya kijamii.

Tungeongeza muda wa watoto wote kukaa shuleni na matumizi ya sheria zinazowalinda wakiwa watoto ambazo sasa watoto wasio shuleni haziwagusi sana
Mfano.
Ajira kwa watoto
Mapenzi, Ndoa na mimba utotoni.

Tungewapa nafasi wazazi urahisi kuwashirikisha kazi au ujuzi watoto wanapomaliza shule. Mtoto wa miaka 16 au 17 ni rahisi kumfundisha ujuzi wa kazi akaweza kuanza kujiajiri kuliko sasa watoto wanamaliza na miaka 13/14 anabaki nyumbani tu.

Haya yangetupa majibu mengine:
Ya kuongezeka wasomi
Kupungua matatizo ya lishe na afya.
Kuongezeka kwa watu wenye ujuzi
Kupunguza unyanyasaji wa kijinsia.
Kuongeza rasilimali watu wenye ufahamu na ujuzi kwenye soko la ajira.

Ila ndo hivyo siasa zimeenda na kesho yetu.
 
Back
Top Bottom