Je, kuna ulazima TICTS iendelee kutoa huduma wakati imefeli!?

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
6,825
9,528
Ripoti kwa mujibu wa gazeti la the Guardian la Jumanne 19 Julai 2022 kampuni hii yenye dhamana ya ku-handle container cargo bandari ya Dar es Salaam uwezo wake umefifia.

Guardian wanasema takwimu za Mamlaka ya Bandari zinaonyesha kwamba TICTS mwaka uliopita yaani 2021 walionyesha ongezeko la 0.8% ya container cargo iliyosimamiwa na hao TICTS.

Kwa mwaka 2021 hao jamaa walishughulikia makontena ya futi 40 yapatayo 606,169 kikiwa kiwango cha ongezeko hafifu la makontena 601,654 ya urefu huohuo waliyoya-handle 2020.

Wachambuzi wanasema katika kipindi cha MIAKA MITANO ILIYOPITA bandari ya Dar performance yake imezidiwa na bandari nyingi shindani za ukanda huu.

SASA, kwa kuwa bandari ndiyo mshipa mku wa wa damu...na kwa kuwa, TICTS wameshindwa kuperform kwa kiwango stahiki, na kwa kuwa kampuni lukuki huko duniani zinaweza kutenda na kututoa kimasomaso tukaweza kushindana, na kwa kuwa Serikali imeruhusu bandari kavu...ni wakati sasa mkataba wa TICTS unapoisha mwezi mmoja ujao...apewe kandarasi mwingine na mwenye uwezo wa hii kazi.

Mkulima nikiwa Mwenge Dar es Salaam.
 
Naskia wapo "bize" saa hv kwenye idara nyeti kupitisha bahasha ili wamwage wino tena...
 
Ticts mnawaonea sana,mwaka2021 ulikuwa mwaka mgumu sana,kila sehemu duniani,pia kumbukeni eneo la ticts mle ndani ni dogo sana,ticts wana vifaa vya kisasa na wafanya kazi hodari,tatizo nafasi eneo lao ni dogo sana,
 
Kwanza mambo ya mikataba iachie serikali,labda ka we una maslahi na kampuni hizo mpya, kijana acha uchawi
 
Back
Top Bottom