Je, kuna ulazima gani wa kulipa mahari kwenye dunia ya leo ya usawa wa kijinsia?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,597
154,852
Ndoa nyingi za Kiafrika huambatana na mahari, ambapo mwanaume hupangiwa vitu vya kuwapelekea wazazi wa mwanamke ikiwa kama asante au shukrani ya kumlea binti vyema.

Mahari inatofautiana lati ya jamii moja na nyingine. Wasukuma hutoa ng'ombe wengi zaidi kwa binti mweupe.

KWENYE dunia ya leo ambapo usawa wa kijinsia unahubiriwa je, kuna haja ya kuendeleza utamaduni wa kulipa mahari?

64308930_2892018007494159_4527951336024571904_n.jpg
 
Kuna ulazima kwa kujibu wa dini lakini sasa inatakiwa ukinganishe thamani ya mahari na binti
 
Kwa kuwa wanataka haki sawa sioni ulazima!!
Hata hivyo mahali si kitu kama wanaoona hawapendani kwa dhati au madishi yao yameyumba!..
Huu utamaduni huko mbeleni utakuja uteketee!.. mahali ni kama kumuuza mtu tu akatumike huko!
Ndio maana wengine huwa wapole wa kipuuzi kisa mahali.. Ni kama vile kidhibiti!.

Kikubwa ni kupendana,kuishi kwa malengo na kuyatumia madishi yenu kisawasawa!
 
Mahali hizi ndo zinasababisha Wanawake waonekane Kama vyomba vya sitarehe tu Kama vyombo vingine.

Just imagine pande mbili zinakaa kuanza kujadili Bei/thamani ya binti Tena na bageini inakuwepo utafkri wanauziana nguo za mitumba kutoka kwa marehemu Nkuruzinza.

Mahali Ni ujinga Sana na sitakuja kumuuza mtoto wangu wa kike endapo nikifikia huko.
 
Tunafuata dini ndio inatulazimisha kulipa, ingekuwa tunafwata katiba hii hii tayari wanaume tungekuwa tumebadili
 
Mahari sio Ahsante wala Shukrani kwa familia ya binti kusema hivyo ni kupotosha lengo la wazee wetu wa zamani wa kiafrika...

Kutolewa kwa mahari ni kipimo kwa kijana anayehitaji kuoa na familia yake kwa ujumla kuonyesha au kuwaaminisha wazazi wa binti kuwa binti yao anakwenda sehemu sahihi ambayo uzalishaji wa mali upo...Aendi kuwa mtumwa wa kuzalisha mali.

Ebu fikiria unahitaji kuoa kisha unaenda kwao binti wanakupangia mahari ya kutoa ikakushinda kutoa...wazo la kwanza utakalo kuwa nalo na wale wazazi wa binti ni kuwa wewe ni maskini wazee wa zamani awakupenda watoto wao waende kwenye familia duni ndo maana walifikia hadi pahali wanamchagulia binti familia ya kwenda kuolewa kukwepa binti yao kuteseka.

Au fikiri umeoa unaishi na mwanamke ulishajitambulisha kwao na mahari ukapangiwa ila ujawah kutoa hata senti:...
 
Ebu fikiria unahitaji kuoa kisha unaenda kwao binti wanakupangia mahari ya kutoa ikakushinda kutoa...wazo la kwanza utakalo kuwa nalo na wale wazazi wa binti ni kuwa wewe ni maskini wazee wa zamani awakupenda watoto wao waende kwenye familia duni ndo maana walifikia hadi pahali wanamchagulia binti familia ya kwenda kuolewa kukwepa binti yao kuteseka.
Hii inategemea, kwa maisha ya sasa kuna baadhi ya wazazi wamefanya mahari kama biashara, unakuta wanaitisha mahari kubwa kiasi kwamba unaona unakomolewa.
 
Hii inategemea, kwa maisha ya sasa kuna baadhi ya wazazi wamefanya mahari kama biashara, unakuta wanaitisha mahari kubwa kiasi kwamba unaona unakomolewa.
Mahari kubwa inategemea unaoa sehemu gani na binti wenyewe yuko ktk hali gani muda huo
 
Usawa uliopo ni wamaneno hakuna usawa wa 50 kwa 50 maana wao wameumbwa kuwa dhaifu siku zote mbele yetu
 
Baba Yake anajua?
Anajua ila sasa yeye ni mlokole baada ya kutubu dhambi ya kumchukua mama Pamela kwa mkopo zamani hizo ili kufidia hela zake alizokula! So kwa kuwa yeye si mkamilifu ameamua kunisamehe tu ili naye asamehewe na baba wa mbinguni
 
Back
Top Bottom