Je kuna ukweli wowote wa hizi imani katika ulimwengu wa kiroho?

MR TOXIC

Senior Member
Jun 4, 2019
190
525
Hello JF

Naomba kufahamu ukweli kuhusu hizi imani ambazo zinaonekana kuwa common miongoni mwa jamii mbali mbali za hapa kwetu.

Je kuna ukweli wowote kwamba mwanaume akipigwa na mwiko wa kusongea ugari anapoteza uwezo wa kupata mtoto??

Je kuna ukweli wowote kwamba ukifagia nyumba au ofisi jioni na kutoa uchafu nje unakuwa una kimbiza bahati au utajiri??

Je hii dhana ya mtu kutumia tafsida katika baadhi ya vitu kwa mfano "dawa ya mboga" anapoenda kununua chumvi nyakati za jioni inahusiana vipi na maisha halisi katika ulimwengu wa kawaida??

Je kuna ukweli wowote kwamba mtoto akikalia kinu wakati akiwa mdogo anapoteza uwezo wa kurefuka siku za usoni baada ya kukua??

Naomba wajuvi wa haya mambo wanitoe tongo tongo isije kufikia mahala tunafanya mambo hatufanikiwi au tukapata madhara kwa sababu ya kuchukulia poa imani kama hizi.
 
'Je kuna ukweli wowote kwamba ukifagia nyumba au ofisi jioni na kutoa uchafu nje unakuwa una kimbiza bahati au utajiri?? '

Sidhani. kama ni hivyo wote wanaoishi ghetto wangeongoza kuwa millionea
 
Hello JF

Naomba kufahamu ukweli kuhusu hizi imani ambazo zinaonekana kuwa common miongoni mwa jamii mbali mbali za hapa kwetu.

Je kuna ukweli wowote kwamba mwanaume akipigwa na mwiko wa kusongea ugari anapoteza uwezo wa kupata mtoto??

Je kuna ukweli wowote kwamba ukifagia nyumba au ofisi jioni na kutoa uchafu nje unakuwa una kimbiza bahati au utajiri??

Je hii dhana ya mtu kutumia tafsida katika baadhi ya vitu kwa mfano "dawa ya mboga" anapoenda kununua chumvi nyakati za jioni inahusiana vipi na maisha halisi katika ulimwengu wa kawaida??

Je kuna ukweli wowote kwamba mtoto akikalia kinu wakati akiwa mdogo anapoteza uwezo wa kurefuka siku za usoni baada ya kukua??

Naomba wajuvi wa haya mambo wanitoe tongo tongo isije kufikia mahala tunafanya mambo hatufanikiwi au tukapata madhara kwa sababu ya kuchukulia poa imani kama hizi.
SOMEHOW I CAN CLARIFY KUWA NI IMANI DHABITI INAWEZA KUFANYA YOTE HAYA AU MENGINE MENGI ZAIDI YA HAYA KUWA HALISI AU NA UKWELI MTUPU. BRO IT'S ONLY YOUR ACTUAL FAITH ON THINGS WHICH MIGHT TRANSFORM WHATSOEVER INTO REALITY AT THE END, WHETHER TO BE PROVED BY SOMEBODY OR OTHERWISE.
 
Back
Top Bottom