Je, kuna ukweli pendo la kwanza ni tofauti na pendo linalofuata?

amshapopo

JF-Expert Member
Sep 7, 2014
693
1,199
Habari wadau,

Tumekua tukibishana na wenzangu kuhusiana na upendo wa kwanza yaani truly love. Kuna wanaosema upendo wa kwanza unakua wakujitoa sana yaani kama msichana ama mvulana anakua na truly love na pindi mahusiano yanapoparanganyika huwa inaumiza sana kwa mlengwa aliyependa na kujisucrifice kwenye huo upendo.

Na wameenda mbali zaidi kuwa yule aliyeumizwa akianzisha mahusiano tena huwa hapendi kama alivyopenda mwanzo hata akija kuoa ama kuolewa.

Na wameenda mbali zaidi wakisema aliyependa huwa anamkumbuka sana mpenzi wake wa kwanza aliyewahi kumpenda licha ya maumivu aliyowahi kuyapata na sometimes moyo huwa radhi kumsamehe mpendwa wake huyo japo huwa haiwezekani.

Upande mwingine wanasema mahusiano yanadepend na uliyempata awe wa kwanza awe wa mwisho yaani moyo unapenda unapopata sehemu unapopendwa (contingent) na haijalishi wa kwanza ama wa mwisho yoyote anaweza kuuteka moyo yaani hamna anayeweza kuuteka moyo permanently.

Je, ukweli ni upi kuhusiana na hizi idea mbili?

Kumbuka hatuongelei mwaume wa kwanza ama mwanamke wa kwanza kwani unaweza kuwa wa kwanza na usipendwe. Tunaongelea truly love ya kwanza.

Nawasilisha.
 
Kwamba nimependana na A kwa mara ya kwanza watakaofuata upendo hautakua kama vile? Hapana siyo kweli.

Kitakachokusumbua ni kama ulianza mapenzi ukubwani.
 
Hayo mambo nasikia wanayo sana watoto wa kike
Kwangu binafsi hio formula ya first love never dies haifanyi kazi
Uhusiano ukivunjika ujue nakusahau moja kwa moja.
 
First true love is reasonably innocent, and has no baggage. The next relationship(s) will always be affected by the previous one(s), positively or negatively.
 
Si kweli unaweza kupenda sana bt baadae unaweza kumpenda mtu tena kuliko ata Yule wa kwanza
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom