Blue G
JF-Expert Member
- Jun 20, 2012
- 5,335
- 3,652
Habarini wana MMU,
Za siku mbili tatu kwa wale wahenga wenzangu akina Mr Rocky,Tized ,Tamatheo na wengine wengi wa zileee Enzi zetu
Leo ninalo hili wakuu,
Katika mambo ambayo nimekuwa nikiamini sikuzote ni kuwa mtu mzima hawezi kubadilishwa mpaka awe ameamua mwenyewe eiza kwa kuona aina ya Maisha anayoishi hayana maana bali hasara tu kwake,au ameona anaumia tu na kupata majeraha kutokana na lifestyle yake au amechoshwa na aina hiyo ya Maisha na hivyo anataka kubadilisha aishi vingine au kaingiwa vilivyo na maneno matakatifu ya Mungu na hivyo akaamua kubadilisha kabisa mwenendo wake mzima wa Maisha ili kutapatanisha Maisha yake na maandiko matakatifu ya Mungu.
Lakini kwa upande wa pili kuna watu huwa wanaamini katika nguvu ya mapenzi kuweza kumbadilisha mtu,(hata kwa sie wapenda series tumeona series nyingi mtu akitransfrom kwa ajili ya mapenzi au kwa ajili ya mtu Fulani) japo ni mpenzi sana wa series za namna hii lakini hazijawahi kuathiri mtizamo wangu juu ya kumadilisha mtu mzima)
Sasa leo nimeona nililete hili kwenu wana MMU Great Thinkers,je kuna ukweli kuwa mtu anaweza kumbadilisha mtu mzima?kuna watu humu wamewahi kubadilika kwa sababu ya mtu au mapenzi kumwelekea mtu Fulani?kuna yeyote amewahi kufanya jitihada za kumbadilisha mtu na akafanikiwa?kuna mtu yeyote ambaye amewahi kuhisi atambadilisha mtu na kuishia kuvunjika moyo baada ya kuona kafanya kila jitihada na ikashindikana?kuna mtu yeyote ambaye amewahi kufanya kila wezalo kubadilika kwa ajili ya mtu au jitihada za mtu kumbadilisha?
Tafadhalini naombeni tushare uzoefu wetu wana MMU