Je, kuna ukweli gani kuhusu hii nadharia?

OIL CHAFU

JF-Expert Member
Jun 8, 2012
996
773
Nilishawahi kuisoma mahali (japo nimesahau ni wapi, huenda hata hapa JF), na pia nimeshawahi kuambiwa na watu wazima kuwa ukiwa unaenda kwa shughuli fulani (huenda ni biashara fulani, au shughuli nyingine) kuwa usifanye sex asubuhi ya siku hiyo. Huenda kuna mambo mbali mbali ambayo mtu hupewa masharti kuwa siku moja kabla ya kwenda kwenye hiyo issue yako, hakikisha hulali na mwanamke.

Sasa nauliza hivi kuna ukweli gani juu ya hii mada? Na kuna uhusiano gani kati ya kulala na mwanamke na mafanikio ya shughuli husika? Kumbuka watu wengi wanapenda ile cha asubuhi wanasema ni kitamu kweli. Mimi binafsi nimekutana na jambo hili kama mara tatu hivi nilipatawa na mkosi, sasa hii ya mara ya tatu kuna mtu nilikutana naye na ndiye alinisaidia, nakumbuka nilikuwa shamba. Yule mtu aliniuliza, vipi usiku ulikuwa na shemeji? Nikashangaa, nikamwuliza kwa nini unauliza hivyo? Akanijibu kuwa ukitaka mafanikio katika maisha yako unapopanga ratiba za shughuli zako nyeti, usilale na mwanamke usiku wa kuamkia siku hiyo.

Nimewaza mpaka leo sijapata jibu.
 
Me imani hio ya kijinga staki hata kuwa nayo.. Asubuhi napiga mapema tu... Labda kwa sababu ya elimu niliyonayo ndo maana imani za kiswahili zozote huwa hazina maana kwangu
 
Imani tu. Ronaldo (The OG one), aliwahi kusema yeye mara nyingi kabla ya game, ilikuwa anapiga game(figuratively), na inampa stamina(nadhani) uwanjani(literally).

Except if it stinks(your game or that thang), then your whole day will as well.
 
Me imani hio ya kijinga staki hata kuwa nayo.. Asubuhi napiga mapema tu... Labda kwa sababu ya elimu niliyonayo ndo maana imani za kiswahili zozote huwa hazina maana kwangu
mwenzetu una elimu kiasi gani mpaka unasahau mambo ya kiswahili? nauliza tu
 
Elimu ya kuunga unga ya hapa na pake
sawa mkuu,
siku moja nilikuwa kijijini mzee mmoja akaniambia wanapata shida kwa sababu wanaongozwa na kiongozi asie na elimu, nikamuuliza yup, akajibu mkuu wa kaya, ndio maana hawana maendeleo! nikakaa kimya maana mkuu wa kaya wa wakati huo alikuwa ni mchumi kutoka UDSM!!! siku njema
 
Ni hivi unapo maliza ku sex unatakiwa kuwa msafi kabla hujatoka kwenda kwenye pilika zako ili kuondoa harufu mbaya,vinginevyo utanuka harufu mbaya kutwa nzima na ndio hapo mantiki ya imani hyo inapojitokeza,
 
Hii imani iko based na uzinzi
na sio mkeo wa ndoa......

uzinzi kwa maana kuna imani baadhi ya watu wana mikosi
lakini mkeo au mumeo ni part of you..

hawezi kukuletea mkosi....
 
Nilishawahi kuisoma mahali (japo nimesahau ni wapi, huenda hata hapa JF), na pia nimeshawahi kuambiwa na watu wazima kuwa ukiwa unaenda kwa shughuli fulani (huenda ni biashara fulani, au shughuli nyingine) kuwa usifanye sex asubuhi ya siku hiyo. Huenda kuna mambo mbali mbali ambayo mtu hupewa masharti kuwa siku moja kabla ya kwenda kwenye hiyo issue yako, hakikisha hulali na mwanamke.

Sasa nauliza hivi kuna ukweli gani juu ya hii mada? Na kuna uhusiano gani kati ya kulala na mwanamke na mafanikio ya shughuli husika? Kumbuka watu wengi wanapenda ile cha asubuhi wanasema ni kitamu kweli. Mimi binafsi nimekutana na jambo hili kama mara tatu hivi nilipatawa na mkosi, sasa hii ya mara ya tatu kuna mtu nilikutana naye na ndiye alinisaidia, nakumbuka nilikuwa shamba. Yule mtu aliniuliza, vipi usiku ulikuwa na shemeji? Nikashangaa, nikamwuliza kwa nini unauliza hivyo? Akanijibu kuwa ukitaka mafanikio katika maisha yako unapopanga ratiba za shughuli zako nyeti, usilale na mwanamke usiku wa kuamkia siku hiyo.

Nimewaza mpaka leo sijapata jibu.
Ngono ni kama maagano au ibada, wengine wakiota tu wanaharibikiwa mambo yao
 
Take for example Wahehe na Wachaga.

Wachaga wana mambo wanayoamini.
Wahehe wana mambo wanayoamini.
Kati ya hayo,yapo yanayoshabihana na yapo yanayokinzana.

Wapo wahehe waliofanikiwa.
Wapo wachaga waliofanikiwa.

Wachaga waliofanikiwa na Wahehe waliofanikiwa hawafanani katika kila wanachokiamini.

UTAKUA UMENIELEWA!
 
Wakuu ngoja nichangie hoja hii kwa kuweka pembeni hii western education.Wakati fulani nikiwa kijijini,timu yetu ya mpira wa kijiji tulipokuwa na mashindano au mechi wazee wetu walituonya sana kufanya mapenz usiku wa kuamkia siku ya mechi.Hivyo tulikuwa tunalala kambi au kuzingatia maneno yao lakini sikuhoji sana juu ya mwiko huo
 
Back
Top Bottom