Je, kuna uhusiano wowote kati ya kutoweka kwa "wasiojulikana" na kuibuka kwa "majambazi" nchini?

M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
13,203
23,019
Ni mwaka jana tu hapa tulikuwa tukihabarishwa mara kadhaa kuwa baadhi ya wananchi (hususani wanaharakati na wanasiasa) walikuwa "wakitwaliwa" na watu "wasiojulikana". Hili iko well documented na sidhani kuna haja ya kupoteza muda kulirudia hapa.

Kuanzia mwezi jana kumekuwepo na wimbi la matukio kadhaa ya ujambazi nchini ambayo yalikuwa nadra sana zile nyakati ambazo "wasiojulikana" walikuwa wakitamba. At the same time, "wasiojulikana" hatuwasikii tena. Hata wale waliokuwa wakijulikana hadi wanatamba kwa ku post vitisho vilivyorekodiwa kwenye social media sasa hivi hawasikiki tena na inasemekana hali zao kiuchumi ni dhoofu bin hali.

Maswali yangu....

1. Watu "wasiojulikana" wamepotelea wapi na kwa nini?
2. "Majambazi" walikuwa wamejificha wapi na kwa nini wajitokeze sasa?
3. Hypothesis 1: je, "wasiojulikana" walikuwa wanafanya hayo waliyokuwa wakiyafanya kwa ajili ya kujipatia riziki kutoka kwa wafadhili wao?
4. Hypothesis 2: je, "wasiojulikana" ndiyo hawa "majambazi", ila sasa wamebadili mtindo wa kujipatia kipato kutokana na kukosa wafadhili?

Hatutafuti mchawi. Tunatafuta logic. Tunaisaka linkage kama tunaweza kuipata.

Bwana Yesu asifiwe.
Tumsifu Yesu Kristo.
Ramadhan Mubarak.
 
Hayo majambazi yamekwapua wapi?

Maana mimi nasikia tu majambazi, Majambazi. Yamepiga wapi tukio?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom