Je, kuna uhusiano wowote kati ya Barrick Gold na George Bush Snr?

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,722
Haya Makampuni makubwa duniani nayo huwa hayakosi wakubwa nyuma yao.

Tunapomjadili Myahudi Comredi Peter Munk ambaye ni raia wa Canada baada ya kukimbia Kuuwawa na Adolf Hitler nchini Hungary na moja ya watu wanaoheshimiwa sana nchini humo huwezi kufunga mjadala na kuondoka. Mwenyekiti na Muanzilishi huyu Mstaafu wa kampuni ambalo Lina hisa karibu 60% kwenye kampuni la Acacia zamani African Barrick Gold ambalo hadi sasa wingu la utata limetanda juu ya nani yuko sahihi wao au tume yetu. Binafsi niko upande wa tume, maana hadi sasa hakuna maelezo ya kisomi na kichambuzi kupinga hata kimoja walichobaini. Huu ndio ukweli uliopo hadi sasa (current truth).

Katika dawati langu la utafiti uchwara(usio rasmi) kutoka katika vyanzo mitandao vingi vinasisitiza huwezi kuitaja Barrick Bila Kumtaja Mkuu wa zamani wa shirika la Ujasusi la US na Rais Mstaafu wa nchi hiyo George Bush Snr.

Wakosoaji na waandishi juu ya kampuni hili wanamtaja nguri huyu wa siasa duniani kama miongoni kwa washirika wakuu wa kampuni hii. Vyanzo vingine vimeenda mbali na kusema amewahi kuwa board members wa kampuni hii kubwa ya madini duniani na mengine mengi. Hili ni dokezo tu unaweza kuzama zaidi.

Haya yanaandikwa ili kujua uzito na ukubwa wa vita hivi. Na kamwe siasa isiingizwe zaidi ya kujikita kwenye facts and findings, sheria na mambo ya kitaalam katika sekta hiyo nono duniani kwa sababu wenda tukajichanganya na kupoteza zawadi hii nono Mungu aliyotupatia Watanzania.

Ninaamini pamoja na yote na historia yenye pande nyingi pande nyingine zinatia hofu tukisimama katika haki tutashinda ila tukisimama ktk propaganda kwenye mambo makubwa ya kidunia kama haya itakuwa kwetu. Hongera Rais kwa kuweka tume ya kiuchumi na kisheria kuongeza umakini ktk Kila hatua unayopiga.

Unaweza Pitia vyanzo mitandao kupata maarifa zaidi.

Peter Munk’s final play - Macleans.ca
The Truth Buried Alive
Founding members of Barrick’s Barricudas - American Herald Tribune
Barrick Founder Peter Munk's 34 Golden Rules, by @tommy
Barrick Gold
 
Back
Top Bottom