Je Kuna Uhusiano Kati ya Logo ya Big Brother Africa & Symbols Za ILLUMINATI?

Iselamagazi

Iselamagazi

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2011
Messages
2,327
Likes
117
Points
160
Iselamagazi

Iselamagazi

JF-Expert Member
Joined Sep 26, 2011
2,327 117 160
Salaam wana Jamvi!

Kuna speculations nyingi sasa kwamba, yapo mahusiano makubwa kati ya LOGO ya Big Brother Africa (BBA) na alama za Illuminati. Je kuna ukweli wowote katika hili?
Ni nani mfadhili/wafadhili wa BBA?

GONGA HAPA!
 
Attachments:

Mourinho

Mourinho

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2012
Messages
4,627
Likes
110
Points
160
Age
98
Mourinho

Mourinho

JF-Expert Member
Joined Jul 24, 2012
4,627 110 160
Illuminati ni nini labla?
 
SONGOKA

SONGOKA

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Messages
1,760
Likes
1,084
Points
280
SONGOKA

SONGOKA

JF-Expert Member
Joined Mar 8, 2012
1,760 1,084 280
je kuna uhusiano gani kati ya jicho la mwanadamu na illuminati symbols
 
queeny

queeny

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2012
Messages
587
Likes
17
Points
35
queeny

queeny

JF-Expert Member
Joined Nov 1, 2012
587 17 35
I have always had doubt about this show, am not exactly sure what it is
 
O

option

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2013
Messages
1,760
Likes
873
Points
280
O

option

JF-Expert Member
Joined Jan 15, 2013
1,760 873 280
mimi binafsi sio mfatiliaji wa big brother na siko aware na nembo yao. but yale mambo ambayo wanayafanya huwa naona ni ya kishetani kabisa. asee sio nembo tu mi nahisi ile shughuli mzima ni ya mashetani.
 
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Messages
107,249
Likes
131,748
Points
280
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2012
107,249 131,748 280
Ilitabiriwa kuwa illuminants ndio watatawala dunia na namba 666 itatumika kila mahali watu hawatatumia pesa tena kufanya miamala bali namba hiyo(666)? Angalia leo kila kitu ni password kuanzia kwenye simu mpaka vitambulisho vyetu .huduma za kibenki zote na manunuzi ya aina mbalimbali tunatumia namba zetu za siri je utabiri umetiMia
Kwa wasiofahamu maana ya illuminant; hili ni daraja la juu katika ngazi za imani ya freemason au wajenzi huru
 
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Messages
107,249
Likes
131,748
Points
280
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2012
107,249 131,748 280
Nembo za illuminants Zipo kila mahali kwa sasa na kuna wakati tunazitumia na kuziabudu bila wenyewe kuwa na habari mfano chukua chupa ya majina ya kilimanjaro halafu geuza juu chini angalia kwa makini ile nakshi iliyozunguka ile chupa utagundua kitu
Angalia bunge letu pale Dom Angalia ule mzunguko wa past na nakshi zake angalia na mpangilio wa ndani aerial view Utagundua kitu
 
kizomanizo

kizomanizo

Member
Joined
Jan 26, 2010
Messages
64
Likes
4
Points
15
kizomanizo

kizomanizo

Member
Joined Jan 26, 2010
64 4 15
Ilitabiriwa kuwa illuminants ndio watatawala dunia na namba 666 itatumika kila mahali watu hawatatumia pesa tena kufanya miamala bali namba hiyo(666)? Angalia leo kila kitu ni password kuanzia kwenye simu mpaka vitambulisho vyetu .huduma za kibenki zote na manunuzi ya aina mbalimbali tunatumia namba zetu za siri je utabiri umetiMia
Kwa wasiofahamu maana ya illuminant; hili ni daraja la juu katika ngazi za imani ya freemason au wajenzi huru
We bwana Mshana acha kupotosha umma. Usijifanye unafahamu nini maana ya hiyo illuminati wakati huna hata japo kauelewa ka hiyo jamii.

Unasema wao ni hadhi ya juu kabisa ya umasoni, huo ni uongo maana haina uhusiano wowote na umasoni. Illuminati ni jamii ya watu waliokuwa na uelewa mkubwa yapata miaka 500 hivi iliyopita ambao walikua wakitoa mafunzo ya kidunia kinyume na yale ambayo kanisa lilikua linataka yafundishwe.

Kupingana huko na kanisa ndio kukafanya wawe watu wa sirisiri kwa kuwa wakati ule kanisa katoliki lilikua na nguvu za kiserikali lingeweza kuwahukumu kifo kama wangefanya mambo yao kwa uwazi.

Hii Big Brother yenu ni takataka ambayo haina uwezo wa ku'illuminate' watu kwa hiyo huo mjicho wao ni kwamba tu huyo kaka mkubwa anakuona kila mahali mpaka uchi wako ukiwa msalani.

Kuhusu maisha kuwa dijitali pia unapotosha umma, ni kwa sababu ya watu wenye mawazo hasi na ya kichawichawi kama haya, jamii yetu haikui kwa kasi inayotakiwa. Badala ya kufurahia kwamba sasa jamii inaelekea kutokuwa na matumizi ya fedha za makaratasi wewe unaanza kuunganisha na mistari ya vitabu ambayo haina uhusiano hata chembe na maisha haya. We baki ukisubiri sijui 666 ndio ichukue dunia, utangoja sana. Miaka hiyo ya 1500 hivi ilikua dizaini kama ni ujanja flani kumponda Papa kwamba yeye ndiye 666 kwa kutumia maandishi fulani yakiyoko kwenye kofia ama fimbo yake. Sasa hivi mmekuja na suala la ATM duh.

Kwa kukusaidia tu, hayo maandishi kwa kofia ya Papa yanasema kwa kirumi hivi:

VICARIUS FILII DEI

Kwa namna ya kuichanganua na kwanini iko hivyo, soma zaidi utajua. Acheni maneno ya kwenye magazeti ya udaku na mjisomeshe zaidi.
 
Iselamagazi

Iselamagazi

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2011
Messages
2,327
Likes
117
Points
160
Iselamagazi

Iselamagazi

JF-Expert Member
Joined Sep 26, 2011
2,327 117 160
Ilitabiriwa kuwa illuminants ndio watatawala dunia na namba 666 itatumika kila mahali watu hawatatumia pesa tena kufanya miamala bali namba hiyo(666)? Angalia leo kila kitu ni password kuanzia kwenye simu mpaka vitambulisho vyetu .huduma za kibenki zote na manunuzi ya aina mbalimbali tunatumia namba zetu za siri je utabiri umetiMia
Kwa wasiofahamu maana ya illuminant; hili ni daraja la juu katika ngazi za imani ya freemason au wajenzi huru
Kumbe! Weka reference kidogo mkuu mshana jr!
 
Last edited by a moderator:
Iselamagazi

Iselamagazi

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2011
Messages
2,327
Likes
117
Points
160
Iselamagazi

Iselamagazi

JF-Expert Member
Joined Sep 26, 2011
2,327 117 160
Satanic Signs - everywhere.
They 've got us surrounded!

Satanic Signs:
- Eye of Horus (including Big Brother Africa Logo?),
- The dot in the circle,
- Rising sun (Swoosh as in horizon),
- Compass & Square,
- Number 666,
- Two towers,
- Pentagram & Pyramid
You may click here: ILLUMINATI SIGNS & IMAGES
 
kamtu33

kamtu33

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2012
Messages
980
Likes
199
Points
60
kamtu33

kamtu33

JF-Expert Member
Joined Mar 15, 2012
980 199 60
kizomanizo ebu rudi tena hapa ufunguke zaidi maana una pointi nyingi ambazo zitaelimisha zaidi tutoke kwenye huu utata
 
Last edited by a moderator:
B

bagi

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2011
Messages
902
Likes
289
Points
80
Age
38
B

bagi

JF-Expert Member
Joined Nov 7, 2011
902 289 80
kizomanizo .mwaga point zaid watu waelimike
 
neemamushi

neemamushi

Member
Joined
Jun 15, 2012
Messages
36
Likes
0
Points
13
Age
25
neemamushi

neemamushi

Member
Joined Jun 15, 2012
36 0 13
Ndugu mshana ungefafanua hyo vicarious gil dei vizur
 
kizomanizo

kizomanizo

Member
Joined
Jan 26, 2010
Messages
64
Likes
4
Points
15
kizomanizo

kizomanizo

Member
Joined Jan 26, 2010
64 4 15
Ni kizomanizo ndo kamwaga hyo lecture,mshana mweupe2 anamwaga matangopori hapa hahaha
Haya nimerudi hapa sasa. Nitaeleza kidogo juu ya Iluminati (tena) na hiyo sentensi ya kirumi.

Illuminati

Tofauti na maoni ya watu wengi ambayo yamekuwa yakiyokana na maneno ya kuzungumzwa mitaani yaani porojo, Illuminati sio kundi la watu wa uchawi uchawi. Moja ya dhumuni kuu la kuanzishwa kwa jamii ya illuminati ilikua ni kupinga imani za kishirikina na imani za kidini kuingizwa katika maisha ya raia ya kila siku.

Huko Bavaria Ujerumani mnamo miaka ya kati ya 1700 hivi ndio kuna watu wasomi na wanasayansi waliamua kuanzisha jamii ya watu walioona mwangaza(ndio maana ya illuminati) ya huko Bavaria. Kwa kuwa miaka ile ya utawala wa kikabaila(feudalism) maaskofu, kanisa na maduki walikuwa na nguvu sana, walitaka sera zao ndio ziwe kama muongozo au katiba ya jamii. Maaskofu walitoa hukumu za kunyongwa wanaowapinga, maduki waliohodhi ardhi waliwaita watu wazanfiki na wachawi(villains). Hii yote ilionekana kwenda kinyume na maendeleo ya kiuchumi wakati huo. Ikumbukwe kuwa miaka hiyo ndio nchi kama Marekani zilikua zinapata uhuru wake na biashara ya mbali kupitia bahari ikaanza kushamiri. Hawa watu waliokuwa na mwangaza wa elimu wakaanzisha jamii yao ila ikawapasa kufanya mambo kwa siri maana utawala ungewahukumu kifo kutokana na kuhubiri sera tofauti na dini, uchawi na ufalme.

Baada ya miaka kumi hivi, kikundi hiki kiliweza kuchota wasomi wengi kama kina Wolfgan van Goethe na wana diplomasia kadha wa kadha kama kina Brunswick ambao walikuwa na ushawishi kwa jamii. Hatua ya serikali ya Bavaria wakati huo kupiga marufuku vikundi vyote vya siri siri ndio imeleta minong'ono mingi sana kuhusu illuminati mpaka leo hii. Taarifa rasmi zinasema kwamba baada ya marufuku hiyo, illuminati ilikosa nguvu na hatimaye kufa kabisa ndani ya hiyo miaka kumi. Vipi vikundi kadha wa kadha ndani ya nchi kama Ufaransa na Bavaria kwenyewe waliibuka baada ya miongo kadhaa na kusema illuminati haikufa na wao ndio wanaoiendeleza. Miaka ya hivi majuzi kutokana na ukuaji wa usambazaji habari na watu kuwa na uwezo wa kuchapa habari zao wenyewe, wimbi jipya la kutangaza watu ni wa illuminati likaibuka tena mara tukasikia rais Bush mdogo ni illuminati, mara mwanamuziki Jay Z naye ni mmojawao. Kwa nijuavyo mimi, kama dhana ya uilluminati bado ni ile ile ya kutoa mwangaza (illumination), wako watu wazuri zaidi na wasomi wangekiwa humo na sio Jay Z, Kanumba na Diamond.

Mwanzo nilimshambulia Mshana kwa kuwachanganya Illuminati na Wamasoni, ni kweli kuwa wao sio wamoja kimalengo na kivikundi. Wamasoni wao wapo kaa mambo ya kiinani zaidi wakati waluminati wao wapo kwa mambo ya kidunia zaidi. Tutaelezana kuhusu wamasoni huko mbeleni.

Halafu kwa mtoa hoja, nembo ya illuminati sio jicho linalotazama bali ni bundi aloketi juu ya kitabu kilichofunguliwa. Sasa sijui nembo ya BBA na bundi na kitabu vina uhusiano gani. Utakuwa umechukua porojo za hapa ukachanganya na za pale basi ba wewe ukawa na cha kuandika humu jamvini.

VICARIVS FILII DEI

Hiyo kauli hapo juu ilikuwepo tangu karne ya 3 hivi yaani kama miaka 278 baada ya Yesu. Ni jina ambalo alipewa askofu wa Roma ambaye ndiye Papa kwa wengi wetu. Biblia za kikatoliki(lazima kueleweka hapa) zinaonesha kwamba Yesu kwa maneno yake aliwaambia mitume kwamba huyu ndiye Kefa (Petro) na juu ya mwamba huo atalijenga kanisa lake. Na pia alitumia lugha ya kumkabidhi funguo za rehema ili kila atalolifunga duniani, na mbinguni pia litafungwa. Mistari hiyo inafanya kanisa katoliki kuamini kuwa Petro mtumw ndie alikuwa papa wa kwanza kabisa. Kwa wasomaji wa mara kwa mara wa biblia watafahamu kwamba baada ya Yesu kuondoka, kuna wakati ulitokea mkwaruzano mkubwa kati ya Paulo na Petro juu ya kuwapokea watu toka mataifa mablimbali(wasio wayahudi). Baada ya mkwaruzano huo Petro aliamua kuhubiri kwa wayahudi wakati Paulo alienda kwa watu wa nje (gentiles). Baada ya kufa kwa Petro(au hata kabla, sina ushahidi) aliteuliwa mtu chini ya uangalizi wa Paulo ili ashike nafasi ya Petro na mtu huyo angekaa Roma(ambapo ndio ilikua kama New York ya dunia enzi hizo) na aendeleze huduma kwa watu wa dunia nzima. Huyu mtu alikuwa akiitwa Linus na vile vile kanisa katoliki linamtaja kuwa ndiye Papa wa pili baada ya Petro.

Hayo maneno yooote juu ya kina petro nimeyasema ili kumjenga msomaji ajue matumizi ya hiyo sentensi ya kirumi. Baada ha kupita mapapa kadhaa, wakaanza kuwaita kwa cheo yaani mrithi wa kazi ya mwana wa mungu. Kama alivyoachiwa Kefa na Yesu, naye kumuachia Linus na kadhalika na kadhalika. Vicarivs Filii Dei kwa tafsiri ya kiingereza ni 'vicar of the son of God' na kwa kiswahili ni kama tu kusema mrithi wa mwana wa Mungu. Sasa baada ya karne kadhaa, kuna wachambuzi wakaanza kuchambua jina la kile cheo kwa namba za kirumi. Ikumbukwe kwamba warumi hawakuwa na tofauti kati ya alfabeti U na V wakati huo, kwa hiyo hilo jina miaka ya 1000 hivi lilianza kuandikwa kwa herufi kama za leo yaani 'VICARIUS FILII DEI'. Sasa ukichukua kila herufi ndani ya hilo neno na kuipa thamani yake kama na mba ya kirumi na kuipa thamani ya 0 herufi isiyo na namba ya kirumi, jumla unapata 666.
V = 5
I = 1
C = 100
A
R
I = 1
V = 5
S

F
I = 1
L = 50
I = 1
I = 1

D = 500
E
I = 1

Hapo ukifanya hisabu utaona kuna 5+1+100+1+5+1+50+1+1+500+1=666

Miaka hiyo ya kati ikawa ni fursa ya watu kusema wameshamjua mpinga Kristo kwamba ni Papa maana namba yake kama ilivyofunuliwa kwenye vitabu vya Ufunuo na Danieli, namba yake ni 666. Hii ilikaa kwa muda sana mpaka watu wakaichoka japo bado kashfa hii inasemwa semwa na baadhi ya watu. Naona sasa watu kama kina Mshana wamekuja na mpya za kusema Password na ATM na mambo ya dijitali ndio 666 mpya. Tusubiri miaka mingine 1000 ndio watabadilika.

Source: ku Google hapa na pale na kusoma baadhi ya vitabu na makala. Hasa hasa Roberts, J.M. (1974). The Mythology of Secret Societies.
 
Mkuu kizomanizo, endelea kusoma hivyo vitabu vyako pamoja na makala, nakupa hongera! Labda ungepitia pia hapa kisha linganisha na haya uliyomwaga hapa jamvini.
GONGA HAPA:
21 GOALS OF THE ILLUMINATI!!!
 
Last edited by a moderator:
salimkabora

salimkabora

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2012
Messages
2,449
Likes
85
Points
145
salimkabora

salimkabora

JF-Expert Member
Joined Nov 10, 2012
2,449 85 145
We bwana Mshana acha kupotosha umma. Usijifanye unafahamu nini maana ya hiyo illuminati wakati huna hata japo kauelewa ka hiyo jamii.

Unasema wao ni hadhi ya juu kabisa ya umasoni, huo ni uongo maana haina uhusiano wowote na umasoni. Illuminati ni jamii ya watu waliokuwa na uelewa mkubwa yapata miaka 500 hivi iliyopita ambao walikua wakitoa mafunzo ya kidunia kinyume na yale ambayo kanisa lilikua linataka yafundishwe.

Kupingana huko na kanisa ndio kukafanya wawe watu wa sirisiri kwa kuwa wakati ule kanisa katoliki lilikua na nguvu za kiserikali lingeweza kuwahukumu kifo kama wangefanya mambo yao kwa uwazi.

Hii Big Brother yenu ni takataka ambayo haina uwezo wa ku'illuminate' watu kwa hiyo huo mjicho wao ni kwamba tu huyo kaka mkubwa anakuona kila mahali mpaka uchi wako ukiwa msalani.

Kuhusu maisha kuwa dijitali pia unapotosha umma, ni kwa sababu ya watu wenye mawazo hasi na ya kichawichawi kama haya, jamii yetu haikui kwa kasi inayotakiwa. Badala ya kufurahia kwamba sasa jamii inaelekea kutokuwa na matumizi ya fedha za makaratasi wewe unaanza kuunganisha na mistari ya vitabu ambayo haina uhusiano hata chembe na maisha haya. We baki ukisubiri sijui 666 ndio ichukue dunia, utangoja sana. Miaka hiyo ya 1500 hivi ilikua dizaini kama ni ujanja flani kumponda Papa kwamba yeye ndiye 666 kwa kutumia maandishi fulani yakiyoko kwenye kofia ama fimbo yake. Sasa hivi mmekuja na suala la ATM duh.

Kwa kukusaidia tu, hayo maandishi kwa kofia ya Papa yanasema kwa kirumi hivi:

VICARIUS FILII DEI

Kwa namna ya kuichanganua na kwanini iko hivyo, soma zaidi utajua. Acheni maneno ya kwenye magazeti ya udaku na mjisomeshe zaidi.
Wewe ndio mbulula kabisa kama hujui illuminati ni zile familia 13 za kiyahudi zinazomiliki jamiii ya freemason kama kijakazi chake na hiyo 666 ni namba yao muhimu inayozingatia miungu yao 36; hebu jumlisha 1 mpaka 36 uniambie umepata ngapi kama sio 666 na nembo zote unazoziona kwenye BBA zinasimamia mojawapo ya miungu hiyo 36; haya ni mambo yanayofunuliwa na wenye hekima pekee hongera MSHANA
 
kizomanizo

kizomanizo

Member
Joined
Jan 26, 2010
Messages
64
Likes
4
Points
15
kizomanizo

kizomanizo

Member
Joined Jan 26, 2010
64 4 15
Wewe ndio mbulula kabisa kama hujui illuminati ni zile familia 13 za kiyahudi zinazomiliki jamiii ya freemason kama kijakazi chake na hiyo 666 ni namba yao muhimu inayozingatia miungu yao 36; hebu jumlisha 1 mpaka 36 uniambie umepata ngapi kama sio 666 na nembo zote unazoziona kwenye BBA zinasimamia mojawapo ya miungu hiyo 36; haya ni mambo yanayofunuliwa na wenye hekima pekee hongera MSHANA
Mbulula ndio nini?
Sibishii mawazo binafsi ila mimi nimetoa mawazo yaliyoandikwa na kupigwa chapa sehemu mbali mbali. Kama ni hizo website za watu wanaojuandikia huwa nazisoma nyingi sana ndugu yangu. Conspiracies ni nyingi sana ila nataka ujue kwamba kama kitu ni cha siri ama kimemaanishwa kuwa cha kificho, wewe usingepata kukisikia. Kusema kwamba ni wachache wenye maono ni sawa na imani tu. kama ukiamini uchawi upo utawaona wote wasioamini kwamba hawajapata hekma hiyo. Nimejaribu kuzungumza vigezo na sio porojo. Kuna porojo nyingi sana humu ulimwenguni nyingine za Sayari X, kuna za Reptoids, kuna za Sumeria, za Neil Armstrong kutotua kwenye mwezi na hata hapa karibuni za kina Dan Brown kwamba Yesu alikuwa na familia yaani mke na watoto. Ukiamua kuzifuata ni haki yako maana wapo hata wanaoamini mawe ni miungu.
 
Forum statistics

Threads 1,272,602
Members 490,036
Posts 30,454,852