Patriot
JF-Expert Member
- Feb 11, 2008
- 5,698
- 4,693
Wanabodi,
Usingizi umekata kutokana na mawazo ya huku kukaza kwa vyuma!, mtu unalala hujui kesho siku itaanza vipi, ukiwa totally empty!. Hivyo faraja yangu pekee ni JF. Nimesoma uzi fulani, nikaanza kuwaza na kujiuliza maswali huku mengine nikijijibu mwenyewe.
Huu ni uzi wa swali kuhusu I.Q za baadhi ya wanasiasa wetu wanaotuhumiwa kuwa na low I.Q, wakiwemo mawaziri, wabunge na wakuu wa mikoa, na vigogo wengine wengi, hivyo nikajiuliza kwanza jee ni kweli hawa wanaotuhumiwa kuwa na low I.Q, jee ni kweli wana low I.Q, au ni mtu tuu ametoa mawazo tofauti, wewe huyapendi, ndio unamtukana ana low I.Q?.
Ndipo nikaanza kujiuliza, jee kuna uwezekano watu wenye I.Q ndogo ni kutokana na makabila yao, kiwango chao umasikini kwenye makuzi, au pia heights zao have something to do with low I.Q, yaani mtu akiwa mfupi, anakuwa na akili fupi?.
Naomba kukiri zaidi ya kukosa usingizi, nimekuwa inspired na motivated kupandisha bandiko hili kutokana na hoja za mwana jf huyu, jidu-la-mabambasi, katika bandiko lake hili
Juma Nkamia ana tatizo la msingi!
Mkuu Jidu, kwa vile mimi nimefanya kazi na Mhe. Juma Mkamia alipojoin RTD, hivyo naomba nisicomment kuhusu I.Q yake, ila generally kuna uhusiano mkubwa kati ya kiwango cha I.Q na object poverty. Maeneo yenye umasikini uliotopea, I.Q za wengi ziko low!.
Angalia level ya umasikini ukanda wa Pwani, including Zanzibar, mikoa ya Singida, Dodoma, Lindi na Mtwara, au makabila yenye umasikini uliotopea kama Wagogo, Warangi, Wanyaturu, Wabarbaig, Wasandawe, Wataturu, Wahadzabe, Wazaramo, Wandengereko etc, linganisha na mikoa yanye neema, Kilimanjaro, Bukoba, Mbeya, Iringa, Mwanza, etc, angalia I.Q za Wachagga, Wahaya, Wanyakyusa etc, bila kusahau the royal tribe, Wasukuma, watu wanaokula vizuri, wanakuwa na I.Q kubwa. Makabila ya mlo mmoja, wanakuwa na low I.Q!.
Data zangu ni kwa mujibu wa random sampling ya matokeo ya mitihani ya kidato cha 4!. Hili hata Mwalimu Nyerere aliliona, hivyo hadi leo, japo Tanzania nzima wanafanya mtihani mmoja wa darasa la saba lakini cut off points za kufaulu ni tofauti mikoa na mikoa ili Watanzania wote wapate fursa za kuendelea kielimu. Tungetumia uniform cut off points, shule zote za sekondari zingejaa Wachagga, Wahaya na Wanyakysa na kuna makabila wasingegusa secondari!.
Mwalimu Nyerere aliwahi kuwasomesha kwa nguvu watoto 4 wa kabila la Wahadzabe, wote walifeli darasa la saba, lakini akalazimisha waende sekondari kwa lazima. Wakasomea pale Pugu, na wote wanne walipata Divisheni Zero!.
Niliwahi kuuliza swali hili, sikupata jibu
Inawezekana Vipi Zanzibar Hakuna Div I, Div II, wala Div III , Wao ni Div IV na Div Zero Tuu?!.
Ila pia kuna uhusiano kati ya heigh ya mtu na akili zake, mtu akiwa mfupi, anakuwa na akili fupi!' Anza kuwa observe heights za waropokaji bungeni, utaniambia!'
Hili la watu wafupi, nililizungumza hapa, wanafanya vitu vya ajabu kutafuta recognition ili ku compensate inferiority complex yao inayosababishwa na height!.
Je, kuna ukweli watu wafupi wana inferiority complex hivyo kukasirika sana wanapohisi kudharauliwa?
Hili la poverty level na low I.Q lina athari kubwa kisiasa, angalia levels za umasikini kwenye maeneo watu waliochagua upinzani, ulinganishe na ngome za CCM, utakuta kwenye umasikini uliotopea ndizo ngome za CCM, na kule kwenye ehueni, ndio wamewachagua wapinzani, angalia Kilimanjaro, Bukoba, Arusha, Tanga, Iringa, Mbeya etc, mkoa kama Dodoma hauwezi kuchagua upinzani, they are just too poor to understand wanachagua nini!. Hata Singida, Lissu is an exceptional case. Hivyo hii situation ya I.Q level ina effects kwenye siasa zetu, hivyo kuendelea kushinda kwa CCM, has something to do with this na nilisema hapa
Watanzania ni ignorants au tumelogwa? October 25, tutafanya informed decision au tutachagua tuu?
Mtazamo: Kanda ya Kaskazini, CCM imechokwa mpaka basi!
Ikitokea CCM ishinde, Je ushindi huo ni kutokana kuwekeza kwenye Maendeleo au kwenye Ignorance?
Kuichagua tena CCM, Je ni kielelezo cha kufanya informed decision, au ni Ignorance?
Hoja zote hizo zinauhusiano na I.Q, na kitu cha ajabu kabisa, kwa kadri vyuma vinavyobana, ndivyo CCM inavyoimarika, mtashuhudia 2020, karibu majimbo yote ya upinzani kama sio yote kabisa huku bara, yatairejesha CCM, upinzani utaanza tena 2025 baada ya rais Magufuli kuipeleka Tanzania kwenye uchumi wa kati, na kuumaliza umasikini.
NB. Kwenye every general rules, there is always exceptional to the case, hivyo hivyo kuna watu wa makabila masikini wenye high I.Q, na kuna watu wafupi wenye akili ndefu na kuna mijitu mibonge yenye akili fupi and vice versa!.
Paskali
Rejea
Kuwa Kichaa Sio Mpaka Kuokota Makopo!. Jee Tanzania Tuna Vichaa Wengi Kuliko Tunavyojidhania?!.
------------
Mdau field marshall1 amepanua wigo wa mjadala huu. Unaweza kusoma hoja zake na kushiriki mjadala >> Tatizo la ufukara kwa baadhi ya makabila ni mfumo wa maisha (Lifestyles)
Ni vizuri kujiuliza kama binadamu. Uko sahihi. Hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya IQ na kabila. Ila kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya IQ na makuzi/malezi na pia vinasaba kwa maana ya lishe na mambo mengine yanayozunguka. Lishe ni muhimu sana! Kuna watu wanahusisha umaskini, lakini nadhani ni pale umaskini unapoutafsiri kwa maana ya mjini. Yaani kuwa na gari, nyumba kubwa, nk. Hiyo hapana.Tukiongelea umasikini wa Kanda na mikoa mleta mada aliyooridhesha hapa tuanzie na historia ya Tanzania na influence ya wakoloni.
Mikoa ya Bukoba, Kilimanjaro, Tanga, Mbeya ni mikoa iliiyobahatika kupata shule za kwanza baada ya wazungu kuleta elimu. Hata Zanzibar.
Tofauti kubwa hapa ni kuwa Zanzibar na Tanga ilimezwa na utamaduni wa ki Arabu kabla ya uzungu.
Pamoja na kuwa shule zilikuwepo lakini wazazi wengi walipata wakati mgumu kuchagua kati ya elimu dunia na elimu akhera.
Kwa dhana ya dini Tanga wamegawanyika sana. Unakuta ukoo mmoja wale walioamua kwenda katika shule za wamissionary walibadili dini.
Utamaduni waawaarabu kwa wakati ule ulikuwa ni biashara na biashara zao nyingi ilikuwa utumwa na kilimo cha minazi. Minazi ikitunzwa vizuri hukaa kwa miaka 50-100. Hivyo ili fanya wazee wapumzike.
Hata hivyo ninaamini mikoa ya Pwani imetoa wazee wengi wakiokuwa na mchango mkubwa katika taifa.
Angalia wale jamaa wa kale ka-kisiwa ka ziwa victoria Ukerewe (Siyo dhambi kuwataja, tuvumiliane) wanavyojulikana kwa IQ kubwa, lakini siyo matajili. IQ yao inachangiwa na lishe! Samaki kwa wiiingi, ugali kidogo. Kwa mwanakijiji wa kisiwani kula samaki siyo utajili! Ni sehemu ya maisha yake. Hapo sasa ndo kabila linaingia maana ukiwa kabila lako liko maeneo ambao mulo ni tatizo, jamii nzima hujikuta kichwani ni patupu!
Kuna makabila yanaonyesha kitu kama IQ kumbe siyo! Kwa sababu tu ya kuweza kuingia mashuleni kwa uwezo wa kifedha, wamejikuta sehemu muhimu, ila kiukweli siyo IQ, ni shida! Tutofautishe IQ na shule.