Je, kuna uhusiano gani kati ya umaskini na ubilionea? Mabilionea wakubwa wengi duniani wanatoka familia maskini hata wa hapa Tanzania

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,911
51,889
Natafakari uhusiano wa ubilionea na umaskini

Ukiangalia mabilionea wote wanaoongoza duniani wamezaliwa familia duni au za kawaida tu wakiwemo akina Bill Gates.

Ukija Tanzania Bilionea Bakheresa alizaliwa familia ya kimaskini tu.
Ukija akina Reginald Mengi hivyo hivyo wametokana na familia maskini.
Ukija Bilionea Laizer huyu juzi tu aliyepata jiwe la Tanzanite la bilioni nane kazaliwa familia maskini tu.

Ukienda kenya familia tajiri namba moja Kenya ni ya Kenyatta. Na mzee Kenyatta alizaliwa familia maskini ya kutupwa.

Asia nzima bilionea namba moja ni Mukesh Ambani ambaye alitokea familia ya kawaida ya chini.

Hebu wataalamu elezeni kwa nini? Watu wengi hudhani mabilionea huzalishwa na mabilionea lakini ukifuatilia historia za mabilionea waliopo sasa hivi utagundua kuwa sio kweli wametoka chini kwa watu maskini na wa kawaida sijui kwa nini.
 
Tukimaliza tujiulize tena ni kwanini viongozi waliotoka familia maskini duniani hupenda kuona wananchi wao wanateseka kinyama halafu wao wanakua wana-act kama ni masiah hivi wametumwa kuja kuwakomboa.
 
Mbona umechagua kwa kudonodonoa lazima itakuwa upo sahihi tu ukidonodonoa.

Ningekuona wa maana ungefanya hivi ukachukua list ya ma Billionaire 100 duniani then ufanye study yako, ma billionaire 20 Tanzania then fanya study, chukua maBillionaire 30 Africa then fanya study then uhitimishe hapa sio unadonoa eti Bakhresa je Mo unamuachaje, eti Bill je Jeff kwanini umeache, acha zako.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom