Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,633
- 697,782
JamiiForums
Moderator
Naomba mada hii msiipeleke kule jukwaa la malalamiko, ushauri na pongezi... Ni mada ya kuamsha mjadala juu ya kile kinachoendelea sasa hivi hapa Jamiiforums
Natangaza maslahi yangu kwenye hili... Sina tatizo na mtu anayeomba msaada... Na nimeshasaidia sana... Na mimi vilevile katika maisha yangu nimeshasaidiwa sana tu, tena na watu baki... Hivyo nisitafsiriwe vinginevyo
JamiiForums nadhani inaingia mwaka wake wa 12 tangu kuanzishwa kwake... Imepitia vipindi vingi... Vigumu na vyepesi... Lakini kubwa kuliko yote imeendelea kukua, kujulikana, kujitangaza vizuri na kuaminika zaidi kuliko mitandao mingine mikubwa....
Hili limevutia wengi kujiunga na huu mtandao.... Na halijatokea kwa bahati mbaya bali kujituma kwa uongozi, kusimamia sheria taratibu za jukwaa kwa ukamilifu wake...
Sasa basi hali ya uchumi wa nchi, ukosefu wa ajira, maisha magumu kumepelekea wengi kukimbilia JF kuomba misaada mbali mbali kuanzia karo za shule, nguo, chakula na mahitaji mengine muhimu
Wapo wafuatiliaji hivyo wakiona mmoja kasaidika na huja ama hushauriwa nao kuomba....
Ni katika makundi hayo waongo, wadanganyifu na matapeli pia hawakosekani... Mifano iko mingi tuu....
RAI YANGU
Je kutokana na ongezeko kubwa la wataka misaada.... Ni wakati muafaka sasa wa kuwa na jukwaa maalum kwa ajili ya hili jambo?
Je hii haitavutia wengi zaidi na kugeuza JF sehemu ya kuombea misaada?
Je ithibati na uhalisia wa wataka misaada vitahakikiwa na nani?
Je tunaweza kuwa na mawazo mbadala kwenye hili?
Ni mjadala wa wazi unaoweza kutoa suluhisho kwenye hili.. Karibuni