Je, Kuna Ufisadi Mkubwa Ndani ya Chadema?

ubongokid

JF-Expert Member
Apr 30, 2017
2,030
3,908
Habari za wakti huu;

Wakati tukielekea katika uchaguzi mkuu wa Chama Kikuu cha Demokrasia na Maendeleo nchini Tanzania Chadema mmoja wa wagombea wa nafasi ya mwenyekiti,Ndugu Kamanda Cecil Mwambe ameibuka na kudai kwamba Chadema inapata Pesa Nyingi za Ruzuku na haijaweza kufanya maendeleo kwa sababu ya usimamizi mbovu na pengine hata ufisadi mkubwa.

Hizi ni tuhuma nzito ambazo kama hazitajibiwa kwa uhakika kabla ya kesho kwenye uchaguzi kuna uwezekano kabisa zikasabisha Mgawanyiko ndani ya chama na hata kupelekea wajumbe kufanya maamuzi ambayo hayana msingi.Nasema hivi kama mtu ambaye nafahamu kwamba ndani ya Chadema kuna changamoto nyingi na kwamba kama ambavyo imekuwa kawaida katika siasa za nchi yetu,Chadema naye imekumbwa na tatizo la kuwa na Ombwe la uongozi ambapo bbadhi ya watu wanahodhi mammlaka ndani ya taasisi za kisiasa na kupelekea kufa kwa demokrasia ndani na nje ya chama.

Niseme tu kwamba Kamanda Mbowe ambaye anamaliza muda wake amefanya kazi kubwa sana katika kukifikisha chama hapa kilipo.Hata hivyo haitakuwa sawa kama chama hakitaweka wezi msingi hasa wa Kitakwimu kuhusu ukweli wa kwamba chama kinapokea Ruzuku inayofikia TZS Bil 13 na kwamba hata Makatibu wa Mikoa,na Wilaya wa Chama hawapewi malipo yoyote yale katika kuendesha shughuli za chama,hasa ukizingatia kwamba hawa ni viongozi wa chama ambao ni sehemu ya waendeshaji na wahamasishaji.

Swali ambalo linatakiwa kutolewa majibu ni Je ni kweli kwamba Chadema imepokea kiasi hicho cha Pesa kama Ruzuku?Swali lingine ni Je bajeti ya uendeshaji wa chama kwa mwaka ni kiasi gani?Na matumizi ya chama yanalenga katika maeneo gani ya msingi?Jebajeti ya Chama inapangwa kwa kutumia utaratibu gani na nani anaisimamia?taarifa ya Fedha huwa inatolewa kawa muda gani kwa watu gani na je huwa inafanyiwa auditing?

Je Watumishi wa chama wanalipwaje na masuala yote yanayohusiana na usimamizi wa mapato na matumizi.

Nisisitize hili kwamba kama wajumbe wataingia katika mkutano kesho bila hili kutolewa majibu na maelezo ya kina basi itakuwa ni tatizo kubwa sana hata kama Mbowe atashinda kwani Chadema kama Chama lazima kijipambanua kiitikadi na hata kiutendaji.Ni alzima Chadema ioneshe kwamba inao uwezo wakusimnamia rasilimali Pesa katika kuhakisha kwamba kinafikia malengo ya kichama na kisiasa.

Haipendezi hata kidgo Chadema kutaka kushika Dola iwapo usimamizi wake wa Rasilimali Pesa hauna uwazi na umakini.

NIkirudi kwenye suala la Wagombea wa Nafasi ya Ueneyekiti ni lazima niweke pia mtazamo wangu kuhusu suala hilo.

Ndugu Mbowe amekuwa katika nafasi ya uenyekiti katiki vipindi kadhaa vya nyuma.Katika kipindi hicho pembeni ya kusimamia shughuli za chama,katika kipindi hicho moja ya jukumu lake lilikuwa ni kuandaa Warithi wa nafasi ya Ueneyekiti ila kuhakikisha uendelevu wa Chama.Swali langu kwa ndugu Mwenyekiti Mbowe ni iwapo Kamanda Mwambe ni sehemu ya walioandaliwa kwa ajili ya Kushika nafasi hio au Mwambe amejitokeza tu from nowhere kuitaka nafasi hio.

Nafahamu kila mwamnachama anayo haki ya kugombea nafasi ya uenyekiti katika chama lakini hii haiondoi umuhimu wa kuwa na succession plan ili kama mambo yanapoenda kombo basi leadership iwe stable.Nasema hivi kama mtu ambaye nimeona madhara ya kutokuwa na mipango ya urithi wa uongozi na madhara yake.

Ni lazimi viongozi waandaliwe kwa ajili yakushika hatamu ila sio lazima wapewe nafasi ya kuwa viongozi.Simmanisha kuwabeba watu bali namaannisha kuwaandaa watu kuassume nafasi za uongozi.

Kuhusu Mwambe kutaka nafasi y akuwa mwnyekiti hoja ya msingi ni iwapo kuna uwezekano kwamba Mwambe ni Mamluki.Na hata kama ni mamluki na ameweza kupita mchujo wa kamati basi ina maanda hata kamati nayo ina mamluki ambao ndio waliompitisha.

Kwa ujumla nafikiri kwamba iwapo Chadema wamempitisha Mwambe wakiwa na lengo la kuonesha tu kwamba kuna Demokrasia ndani ya Chama ilhali hawana nia ya dhati ya kumpokea kama mwenyekiti wa Chama basi ni jambo la hatari sana.Ni ja mbo la hatari kwa sababu iwapo Mwambe atashinda atajikuta anakutana na oposition kutoka kwa wale walwe ambao wamemchagua.

Ni Mtazamo tu,Tusijenge Chuki.
 
Maendeleo gani wakati serikali ya chama chake ina hakikisha pesa yote ina ishia mahakamani? Hizi propaganda za Ccm hazita pata nafasi ya kuibomoa Chadema.
 
FB_IMG_1576576523453.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unahangaika sana leo


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom