je kuna udhaifu katika kudhibiti madawa ya kulevya kwa vijana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

je kuna udhaifu katika kudhibiti madawa ya kulevya kwa vijana

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by youngforeva, Aug 26, 2011.

 1. youngforeva

  youngforeva Member

  #1
  Aug 26, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  AKIFAFANUA kuhusu uingizwaji wa madawa ya kulevya nchini,kijana mmoja aliyewahi kutumiwa kama mvushaji wa madawa hayo(jina linahifadhiwa) ya kulevya alifafanua kuwa,mambo kama hayo hayawezi kuzuilika hata kidogo kwani baadhi ya viongozi wa jeshi la polisi kitengo cha kudhibiti madawa nchini wanahusika kwa asilimia nyingi sana.wameweka watu wao kila kona,airport,bandari na sehemu nyingine za mipakani maana wanakula na wale wanaoingiza madawa ya kulevya nchini.Kijana huyo ambaye kwa sasa amesema ameacha kutumia madawa hayo alifafanua kwa kusema haya;

  Mimi nilikuwa nikitumiwa kuwekewewa pipi tumboni, tunasafirishwa hadi Pakistani na wakati tukifika kule tunafanyiwa operesheni ya tumbo na kuingiziwa pipi za madawa ya kulevya na baadaye tunafungiwa ndani,tunawekwa katika majeneza kama watu tuliokwisha kufariki na tunasafirishwa hadi uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam au uwanja wa kimataifa wa KIA uliopo Kilimanjaro,tukishafika hapo tunasafirishwa hadi Dar es salaam,na kufichwa mahali hadi inapofika mida ya usiku ndiyo tunapelekwa katika nyumba iliyopo Mikocheni,hapo ndiyo tunafanyiwa upasuaji tena na kutolewa hizo pipi ,halafu mwisho tunapewa pesa kidogo ambazo hata hazikidhi mahitaji sawa na kazi tuliyofanya.

  WAKATI HUO HUO,viongozi wa dini ambao wamepaswa kuwa mfano wa kuigwa ili kumaliza tatizo hilo kwa vijana wanawafundisha huko kwenye makanisa na misikiti,imekuwa tofauti kwani wao baadhi yao ndiyo wamekuwa wakijihusisha na shughuli za uuzaji wa madawa ya kulevya.

  Ilikuwa machi 4,mwaka 2011,mchungaji Dennis Okechuku wa kanisa la lord choose charismatic Revival Church la Biafra kinondoni jijini Dar es salaam alitiwa mbaroni baada ya kukutwa na kilo 81 za herione,majira ya saa 2.45 usiku,katika mtaa wa mtongani kunduchi,nyumba namba 593.(kwa hisani ya hassbaby’s blog.wwwhassbaby’s.blogspot.com.muendelezo soma www.vijanatanzania.wordpress.com
   
Loading...