Je, kuna ubaya Tanzania ikavikwapua na kuvifanya visiwa vya Comoro sehemu ya Tanzania?

Hahaha, sio kutawala, ni kuungana tu, kama Zanzibar na Tanganyika ilivyokuwa...

Zanzibar na Tanganyika hakuna muungano, bali Tanganyika anaitawala Zanzibar kimabavu.
Tunaweza kushirikiana na Comoro kibiashara vizuri tu bila ya hata muungano ikiwa patakua na misingi mizuri itakayowekwa.
Hata kwa Zanzibar naamini kungekua na mahusiana mazuri zaidi baina ya Bara na Zanzibar kama uhusiano wetu ungekua upo kwa target za kimaendeleo kama Biashara, Utalii na employment opportunities kiujumla.Kuliko huu muungano wa kijeshi unaoendelea kimabavu unaoendeleza kuzalisha chuki na visasi baina yetu.

Moja ya sifa mbaya ya Binaadamu ni kupenda kumtawala mwenziwe, Sisi tunalia na Wazungu kua wametutawala nawanaendelea kulazimisha kutuendesha lakini tunajisahau sisi wenyewe tunayafanya hayo hayo kwa wenzetu.
 
Zitumike mbinu za kidiplomasia, ikishindikana kwa ustaarabu basi liundwe zengwe na vikwapuliwe kwa nguvu, maana wanasema umoja ni nguvu, ni kama Zanzibar tu ikivyonyakuliwa. Nasema hivi maana kuna kitu cha ajabu sana nimekigundua baada ya kuencounter wacomorro kadha wa kadha katika mizunguko hasa ya Kariakoo.
Kiukweli hawa watu wanajiina ni waTanzania kamili kabisa, na wanataka haki zote sawana mTanzania mwingine yeyote yule. Yaani uFaransa anatoka alikotoka kisha anakuja uwani kwetu kumiliku kisiwa, huu ni upunguani wa wapi huu?

Tunaomba tupewe historia ya Commoro kwanza ili tujue tulikwama wapi?

Moja ya manufaa makubwa sana ambayo nimeyaona kwa integration tuliyoifanya na Zanzibar ni 'huge economic, social & political cooperation', fikiria ni kwa urahisi kiasi gani Tanesco imeweza kuuza umeme mwingi sana visiwani bila vikwazo vyovyote, fikiria namna wanafunzi wanapokuja kusoma vyuo vikuu vya bara na kupata mikopo minono ya Heslb bila hiyana wala vikwazo vyovyote vile, pia ona jinsi watu toka visiwani wanavyokuja kupata ajira na kufanya biashara bara bila usumbufu, fikiria jinsi bara tunavyoagiza maziwa toka Zanzibar bila shida yeyote ile, faida ni lukuki.

Lakini ninachokisikia kwa chini ya kapeti ni kwamba kisiwa kimoja wapo cha Comoros kinachomilikiwa na wazungu kinatumika vibaya kutunyonya na kututikisa, mfano eti kuna wakati walikuwa wananunua ng'ombe maelfu kwa maelfu, wanapelekwa hapo kisiwani, wanachakatwa kisha nyama kupelekwa paris, lakini kiutaratibu walipaswa watengeneze kiwanda cha kuchakata hizo nyama hapa nchini kisha zisafirishwe kwenda paris tokea hapa na mapato stahiki ya kodi ya baki hapa, huo ni mfani tu.
Kingine ni Tax evasion techniques kama zile zinazofanyika visiwa vya Seychelles, ni kwamba kampuni inacheza sarakasi kwa kutumia mamlaka za visiwa zilizopo karibu na nchi yako, hivyo wanakuja kufanya biashara kwako lakini base yake anaiweka uwani kwako ambapo huwezi kumfikia sababu ni mamlaka ya mtu mwingine, hii michezo ilitaka kufanyika kwa kuitumia Zanzibar hasa katika uagizaji wa sukari na spea za pikipiki, lakini kwakuwa tuna-control na Zenji ilikuwa ni rahisi kwetu kudhibiti hali hiyo.

===============================

===============================

Likes 52 tayari 😀👍👏💪

visiwa vya unguja na pemba mpaka leo vinawatesa ... haya mnataka kuongeza gunia la misumari kichwani... SHUBBAMITTTT hamtaweza
 
Zanzibar na Tanganyika hakuna muungano, bali Tanganyika anaitawala Zanzibar kimabavu.
Tunaweza kushirikiana na Comoro kibiashara vizuri tu bila ya hata muungano ikiwa patakua na misingi mizuri itakayowekwa.
Hata kwa Zanzibar naamini kungekua na mahusiana mazuri zaidi baina ya Bara na Zanzibar kama uhusiano wetu ungekua upo kwa target za kimaendeleo kama Biashara, Utalii na employment opportunities kiujumla.Kuliko huu muungano wa kijeshi unaoendelea kimabavu unaoendeleza kuzalisha chuki na visasi baina yetu.

Moja ya sifa mbaya ya Binaadamu ni kupenda kumtawala mwenziwe, Sisi tunalia na Wazungu kua wametutawala nawanaendelea kulazimisha kutuendesha lakini tunajisahau sisi wenyewe tunayafanya hayo hayo kwa wenzetu.
Sawa lakini ushirikiano si kibiashara tu, bali kijamii na kisiasa ni muhimu pia, na hii ndio huzaa umja na nguvu ya kweli isiyo na shaka ndani yake, leo hii Afrika ingekuwa nchi moja na yenye Rais mmoja hivi tungekosa kuwa na Permanent membership ya UN security council? Elewa msingi na mantiki ya hoja yangu.
 
visiwa vya unguja na pemba mpaka leo vinawatesa ... haya mnataka kuongeza gunia la misumari kichwani... SHUBBAMITTTT hamtaweza
Vimetushinda vipi wakati umoja umetaradadi, hakuna mtu yeyote anaethubutu kuvichezea vile visiwa sababu ya umoja tulionao, vinginevyo leo tungesikia kuna boko haram, Alshabab na uamsho wamejazana mule.., umoja ni nguvu
 
Acha kuishi kwa misingi mibovu yapropaganda. Hebu fatilia sababu ya hizo za alshabab na boko haram utafahamu kuwa misingi yake inatokana na utawala mbovu na wa mabavu unaonea watu. Nahilo lipo ndani ya Tanzania ni muda tu ndani ya TZ tutayaona kama hayo.

Na kinachofanya uamini kama Zanzibar kungekua na Alshabab na boko haramu ni nin? au kwakua ni waislamu? Mbona Oman, UAE na Kuwait hakuna?
 
Sawa lakini ushirikiano si kibiashara tu, bali kijamii na kisiasa ni muhimu pia, na hii ndio huzaa umja na nguvu ya kweli isiyo na shaka ndani yake, leo hii Afrika ingekuwa nchi moja na yenye Rais mmoja hivi tungekosa kuwa na Permanent membership ya UN security council? Elewa msingi na mantiki ya hoja yangu.

Ndani ya akili yako unafikiri linawezekana hilo kwa Afrika? wangeanza kujifundisha kuachia madaraka vyama tawala wanaposhindwa chaguzi kwanza halafu ndio waanze harakati ya kuwa na nchi moja.
 
Acha kuishi kwa misingi mibovu yapropaganda. Hebu fatilia sababu ya hizo za alshabab na boko haram utafahamu kuwa misingi yake inatokana na utawala mbovu na wa mabavu unaonea watu. Nahilo lipo ndani ya Tanzania ni muda tu ndani ya TZ tutayaona kama hayo.

Na kinachofanya uamini kama Zanzibar kungekua na Alshabab na boko haramu ni nin? au kwakua ni waislamu? Mbona Oman, UAE na Kuwait hakuna?
Makundi ya kigaidi huwa yanapandikizwa na mabeberu ili kudestabilize sehemu mbali mbali duniani kwa maslahi yao binafsi, mfano kuuza silaha au kuiba madini katika ile.sintofahamu, na huwa wanachagua nchi ambazo ni dhaifu, lakini nchi iliyoungana na kuwa imara haiwezi kuchezewa chezewa kirahisi, ni waarabu walivyokuwa wanaichezea Zanzibar, lakini ilipoingia kwenye umoja na Tanaganyika hakuna hata inzi anaeleta shida kule, ni shwaaaaaari kabisa..., watalii wanamiminika tu.., waulize uamsho wakupe habari kamili..
 
Ndani ya akili yako unafikiri linawezekana hilo kwa Afrika? wangeanza kujifundisha kuachia madaraka vyama tawala wanaposhindwa chaguzi kwanza halafu ndio waanze harakati ya kuwa na nchi moja.
Marekani ambayo leo tunaiona ndio giant walikuwa ni vinchi vidogo vidogo kama sisi, ikabidi ipiganwe vita kubwa sana ya kumaliza utumwa kati ya north na south, lakini hatimae umoja ulipatikana, hata sisi huku lazima tuanze kidogo kidogo.., kama alivyoanzisha Karume na Nyerere mwaka 1964, hadi leo hakuna aliyeweza kufanikisha walichofanikisha hawa wazee..., one day yes...!
 
Makundi ya kigaidi huwa yanapandikizwa na mabeberu ili kudestabilize sehemu mbali mbali duniani kwa maslahi yao binafsi, mfano kuuza silaha au kuiba madini katika ile.sintofahamu, na huwa wanachagua nchi ambazo ni dhaifu, lakini nchi iliyoungana na kuwa imara haiwezi kuchezewa chezewa kirahisi, ni waarabu walivyokuwa wanaichezea Zanzibar, lakini ilipoingia kwenye umoja na Tanaganyika hakuna hata inzi anaeleta shida kule, ni shwaaaaaari kabisa..., watalii wanamiminika tu.., waulize uamsho wakupe habari kamili..

Labda ungetufahamisha hao waarabu walikua wanaichezea vipi Zanzibar. Na kulikua na shida gani kabla ya huo Muungano na Tanganyika
 
Kulitokea uhuru feki ambapo kuna waarabu flani ndio wakawa wanjidai wanaiendesha nchi kikoloni..., na ndio ikapelekea mapinduzi, sasa wale waliopinduliwa baada ya mapinduzi hawakukubali kirahisi hivyo wakawa wanajipanga kufanya mapinduzi na wao, ndio maana Zenji wakajikabidhisha kwenye mikono salama ya Tanganyika
 
Azali Assoumani (Arabic: غزالي عثماني‎, born January 1, 1959) is a Comorian politician who is the President of the Comoros. He has been in office since 2016. Previously he was President from 1999 to 2002 and again from 2002 to 2006.

President of the Comoros
Azali Assoumani
غزالي عثماني
Azali Assoumani 2018.jpg
Azali in 2018
Incumbent
Assumed office
26 May 2016
Vice PresidentAbdallah Said Sarouma (2016-2019)
Djaffar Ahmed Said(2016-2019)
Moustadroine Abdou(2016-2019)[1]
Preceded byIkililou Dhoinine
In office
26 May 2002 – 26 May 2006
Vice PresidentCaabi El-Yachroutu Mohamed
Rachidi ben Massonde
Preceded byHamada Madi (Acting)
Succeeded byAhmed Abdallah Mohamed Sambi
In office
30 April 1999 – 21 January 2002
Preceded byTadjidine Ben Said Massounde (Acting)
Succeeded byHamada Madi (Actin
 
Kulitokea uhuru feki ambapo kuna waarabu flani ndio wakawa wanjidai wanaiendesha nchi kikoloni..., na ndio ikapelekea mapinduzi, sasa wale waliopinduliwa baada ya mapinduzi hawakukubali kirahisi hivyo wakawa wanajipanga kufanya mapinduzi na wao, ndio maana Zenji wakajikabidhisha kwenye mikono salama ya Tanganyika

Mkuu ningeshauri ukapitie tena historia ya Zanzibar kwa utulivu. inaonekanwa ulilishwa sana matango pori.
 
Back
Top Bottom