Je, kuna ubaya Tanzania ikavikwapua na kuvifanya visiwa vya Comoro sehemu ya Tanzania?

FRANCIS DA DON

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Messages
16,133
Points
2,000
FRANCIS DA DON

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined Sep 4, 2013
16,133 2,000
Zitumike mbinu za kidiplomasia, ikishindikana kwa ustaarabu basi liundwe zengwe na vikwapuliwe kwa nguvu, maana wanasema umoja ni nguvu, ni kama Zanzibar tu ikivyonyakuliwa. Nasema hivi maana kuna kitu cha ajabu sana nimekigundua baada ya kuencounter wacomorro kadha wa kadha katika mizunguko hasa ya Kariakoo.
Kiukweli hawa watu wanajiina ni waTanzania kamili kabisa, na wanataka haki zote sawana mTanzania mwingine yeyote yule. Yaani uFaransa anatoka alikotoka kisha anakuja uwani kwetu kumiliku kisiwa, huu ni upunguani wa wapi huu?

Tunaomba tupewe historia ya Commoro kwanza ili tujue tulikwama wapi?

Moja ya manufaa makubwa sana ambayo nimeyaona kwa integration tuliyoifanya na Zanzibar ni 'huge economic, social & political cooperation', fikiria ni kwa urahisi kiasi gani Tanesco imeweza kuuza umeme mwingi sana visiwani bila vikwazo vyovyote, fikiria namna wanafunzi wanapokuja kusoma vyuo vikuu vya bara na kupata mikopo minono ya Heslb bila hiyana wala vikwazo vyovyote vile, pia ona jinsi watu toka visiwani wanavyokuja kupata ajira na kufanya biashara bara bila usumbufu, fikiria jinsi bara tunavyoagiza maziwa toka Zanzibar bila shida yeyote ile, faida ni lukuki.

Lakini ninachokisikia kwa chini ya kapeti ni kwamba kisiwa kimoja wapo cha Comoros kinachomilikiwa na wazungu kinatumika vibaya kutunyonya na kututikisa, mfano eti kuna wakati walikuwa wananunua ng'ombe maelfu kwa maelfu, wanapelekwa hapo kisiwani, wanachakatwa kisha nyama kupelekwa paris, lakini kiutaratibu walipaswa watengeneze kiwanda cha kuchakata hizo nyama hapa nchini kisha zisafirishwe kwenda paris tokea hapa na mapato stahiki ya kodi ya baki hapa, huo ni mfani tu.
Kingine ni Tax evasion techniques kama zile zinazofanyika visiwa vya Seychelles, ni kwamba kampuni inacheza sarakasi kwa kutumia mamlaka za visiwa zilizopo karibu na nchi yako, hivyo wanakuja kufanya biashara kwako lakini base yake anaiweka uwani kwako ambapo huwezi kumfikia sababu ni mamlaka ya mtu mwingine, hii michezo ilitaka kufanyika kwa kuitumia Zanzibar hasa katika uagizaji wa sukari na spea za pikipiki, lakini kwakuwa tuna-control na Zenji ilikuwa ni rahisi kwetu kudhibiti hali hiyo.

===============================
===============================

Likes 56 tayari 😀👍👏💪
 
124 Ali

124 Ali

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2010
Messages
7,306
Points
2,000
124 Ali

124 Ali

JF-Expert Member
Joined Apr 25, 2010
7,306 2,000
hapo zenjiber tu kamas zinatutoka ndio ije kuwa comoro?pale wana visiwa vitatu kama zenji vyenye wakaazi,kutokana na fujo zao za uchaguzi sasa wameamua hakuna kupiga kura ila wanafanya zamu ya kutawala kila kisiwa kinatoa mtu wao .
miaka michache nyuma mmoja wa rais wa kisiwa kimojawapo aligoma kuachia kiti ndio akatimuliwa na wanajeshi wa tz bila hata risasi kuruka wafuasi waliposikia zogo la nyimbo za kuhamasisha kuto kwa wajeda wetu kakikimbia mbio tena kajifanya demu asinyakwe
 
FRANCIS DA DON

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Messages
16,133
Points
2,000
FRANCIS DA DON

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined Sep 4, 2013
16,133 2,000
Tuongeze mpaka kama iddi amini... Twende mpaka Mombasa na Kigali na Bujumbura na Lilongwe na kote kote...
Hao tayari kuna mchakato wa East African Federation ambao unaendelea, ila tukishaungana na hao waje watukute tayari tuna mtaji wa kutosha kapuni, la sivyo tutakuwa wanyonge, hasa kwa Kenya.
 
FRANCIS DA DON

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Messages
16,133
Points
2,000
FRANCIS DA DON

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined Sep 4, 2013
16,133 2,000
Ikitokea hivyo, basi hata hayo mahusiano ya kibiashara na ufaransa yatakufa. Tz inatumika ndiyo sivyo na karibu kila jirani yake, wananufaika uwezo wetu, ila sisi hatupati la maana.
Kwahiyo tukae tu na kukubali hali hiyo bila kuchukua hatua?
 
ndio walewale

ndio walewale

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Messages
1,426
Points
2,000
ndio walewale

ndio walewale

JF-Expert Member
Joined Apr 20, 2013
1,426 2,000
Simaanishi kwamba 'tuoe' moja kwa moja, tupeleke tu barua ya 'uchumba' kwanza, kisha tuone muelekeo wao upo vipi..
Mchumba akionyesha ''kukubali'' ? Tunatia mimba na kukimbia (tutalea mtoto) au tunaweka ndani (ili watoto wa ndoani wapate 'mama mdogo') ?
 
FRANCIS DA DON

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Messages
16,133
Points
2,000
FRANCIS DA DON

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined Sep 4, 2013
16,133 2,000
uroho wa ardhi huu. wakati simiyu hakuna hata wakulima ardhi liko bwelele
Hapana, hapa nazungumzia ushirikiano wa kibiashara, kijamii na kisiasa na watu wa nje ya mipaka yetu.., huku ni kuongeza fursa kwao na kwetu (Mutual beneficiation)
 
FRANCIS DA DON

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Messages
16,133
Points
2,000
FRANCIS DA DON

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined Sep 4, 2013
16,133 2,000
Tanzania tunauza nini kwenda Comoro? Tuanzie hapo..
 
mitale na midimu

mitale na midimu

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2015
Messages
9,870
Points
2,000
mitale na midimu

mitale na midimu

JF-Expert Member
Joined Aug 26, 2015
9,870 2,000
uroho wa ardhi huu. wakati simiyu hakuna hata wakulima ardhi liko bwelele
 
Z

ZEE LA HEKIMA

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2015
Messages
1,221
Points
2,000
Z

ZEE LA HEKIMA

JF-Expert Member
Joined Aug 10, 2015
1,221 2,000
Ndoto nzuri. Lakini kama tumeshindwa kutatua "kero za muungano" na visiwani kwa miaka yoooote, tukijiongezea visiwa vingine si ndio tutakuwa tumejiweka vibaya kabisa?
 

Forum statistics

Threads 1,326,670
Members 509,565
Posts 32,230,401
Top