Je, kuna Tundu (Hollow) katika Ncha ya Kaskazini linalotoa miale ya Mwanga kutokea Ndani ya Dunia?

Mgambilwa ni mntu

JF-Expert Member
May 30, 2017
2,869
3,188
Baadhi ya Wataalamu wa Conspiracy Theory wamekuwa wakionyesha kuwa, Dunia ni hollow (Tundu) ambalo lina mwanga (Jua dogo) kwa ndani na kuwa kuna viumbe (Aliens) wanaoishi ndani yake wakiwa na ustaarabu wa hali ya juu. Ustaarabu huo unaitwa Agartha na Mji Mkuu ni Shamballah
IMG_4884.jpg
Wataalamu hao wamekuwa wakieleza kuwa, Ncha za Kaskazini na Kusini zina uwazi (hollow) ambayo huwa hauonyeshwi kwa makusudi na picha za satellite. Wanadai licha ya jitihada nyingi za NASA ku-edit eneo hilo, bado baadhi ya picha zinaonyesha shimo (hole) kwenye Ncha ya Kaskazini.
IMG_5329.PNG


Aidha, inaelezwa kuwa, ukifika eneo hilo joto huongezeka licha ya eneo la Ncha ya Kaskazini kufunikwa na barafu kutokana na joto linalotoka ndani ambako kuna jua dogo.
Eneo hilo linalindwa na Marekani na ndege haziruhusiwi kupita eneo hilo, ukilazimisha unadunguliwa.
IMG_4892.jpg


Wajuvi wa mambo nadhani mtatusaidia juu ya hii kitu.
Ukifuatilia You Tube juu ya Hollow Earth utajifunza mengi.
 
Hiyo dhana inapingana na Giologia ,Giologia inaeleza kuwa muundo wa ndani ya dunia umegawanyika katika matabaka makuu matatu.Tabaka la juu ni crust la katikati ni Mantle na mwisho core.Na hiyo core sehem ya katikati kabsa ni yabisi (Solid) kutokana na element zinazoiunda na pia high pressure.Hakuna mahali giologia inapoeleza kama kutoka tabaka la chini kuna tundu lililotokea kwenye hizo ncha.
Lakini Elimu juu ya haya mambo ni pana.Niko radhi kusikia mawazo mbadala pia.
 
Last edited:
Hiyo dhana inapingana na Giologia ,Giologia inaleeza kuwa muundo wa ndani ya dunia umegawanyika katika matabaka makuu matatu.Tabaka la juu ni crust la katikati ni Mantle na mwisho core.Na hiyo core sehem ya katikati kabsa ni yabisi (Solid) kutokana na element zinazoiunda na pia high pressure.Hakuna mahali giologia inapoeleza kama kutoka tabaka la chini kuna tundu lililotokea kwenye hizo ncha.
Lakini Elimu juu ya haya mambo ni pana.Niko radhi kusikia mawazo mbadala pia.
Nimeisoma Jiografia A-Level vizuri na naifahamu vyema na layers zake zote. But still uelewe kuwa, mwanadamu hajawahi kwenda chini ya km hata 10. Hivyo hata hiyo layer ya Crust hajafika hata robo ya upana wake, japokuwa Crust ndo kembamba zaidi. So utakuta kuwa, theory ya uwepo wa moving molten materials kwenye Mantle nayo ni debatable tu still. Na uelewe pia kuwa ukiacha Crust, layers za Mantle na Core, ziligundulika material compositions kupitia movement ya mawimbi ya matetemeko ya ardhi. Pasipo matetemeko tusingejua for sure materials ya ndani ya Dunia zaidi ya kutegemea vulcanicity na volcano.

IMG_5326.JPG


Hivyo kwa muktadha huo, Dunia inaweza kuwa hollow kwa ndani but still mawimbi ya matetemeko yakapita kwenye maeneo mengine ya milima iliyomo ndani ya Dunia.
Issue hii wazee tukubali kuwa inafikirisha. Na nimeongea haya nikiwa pia mtaalamu wa jiografia.
Ndiyo maana nikaileta tuchanganye akili za kuambiwa na za kwetu.
 
Huo ni ujinga na uongo
Panua akili yako kutaka kujifunza zaidi, elimu haina mwisho.
Hakuna mtu aliyewahi kufikiria kuwa, kuna siku Gravity itakuja kuwa proved wrong. Kuna Mtaalamu wa Chuo Kikuu cha Leiden, Uholanzi amefanikiwa mwaka 2016 kushawishi umma wa Wanasayansi dhidi ya theory ya Gravity na Dark Matter na sasa, kuna hofu kuwa, huenda suala hilo lita-transform Physics completely.

A theory that challenges Newton’s and Einstein’s gravity and nixes dark matter passed its first test
 
Huyu Ndege kila Winter inapoanza Kizio cha Kaskazini, yeye huelekea Eneo la Arctic (Bahari iliyoko North Pole). Kwa kawaida ndege karibia wote wakati wa Winter hukimbilia barani Afrika (Tropical) lakini huyu huenda huko North Pole na kurudi na watoto Winter inapoisha huko Ulaya, Why?

IMG_5342.jpg


 
Kutokana na theory hii, inadaiwa kuwa, hata sayari zingine pia zina holes kwenye Ncha (poles) zao. Angalia Sarateni (Saturn), Sumbura (Jupiter) na Mihiri (Mars)
IMG_5374.JPG
IMG_5373.JPG
 

Attachments

  • IMG_5375.JPG
    IMG_5375.JPG
    13.6 KB · Views: 68
Hiyo dhana inapingana na Giologia ,Giologia inaleeza kuwa muundo wa ndani ya dunia umegawanyika katika matabaka makuu matatu.Tabaka la juu ni crust la katikati ni Mantle na mwisho core.Na hiyo core sehem ya katikati kabsa ni yabisi (Solid) kutokana na element zinazoiunda na pia high pressure.Hakuna mahali giologia inapoeleza kama kutoka tabaka la chini kuna tundu lililotokea kwenye hizo ncha.
Lakini Elimu juu ya haya mambo ni pana.Niko radhi kusikia mawazo mbadala pia.
 
Back
Top Bottom