Je kuna Taifa lolote Duniani limeendea kwa kuendekeza kupindisha ukweli?

mmaroroi

JF-Expert Member
May 8, 2008
2,960
544
Ndugu zangu wanaJF na watanzania kwa ujumla naomba tuijadili mada hii kuwa, Je kuna Taifa lolote Duniani limeendelea kwa kuendekeza kupindisha ukweli?

Maana yangu hapa ni kwamba kama inatokea katika Taifa/Jamii au chama cha siasa kunakosekana uaminifu na haki haitolewi miongoni mwa jamii wanaweza kweli kusaidiana na kujiletea maendeleo?
Katika imani ya dini yoyote ile ukweli na haki kwa wote ni kitu muhimu sana, kama kuna dini ya shetani huko sijui. Ikifikia mahali viongozi wa serikali katika nchi hawaaminiki kutokana na matendo yao na wao ndio wahamasishaji wa maendeleo na ndio waliokabidhiwa rasilimali za nchi kuwaletea wananchi maendeleo si hapo pana tatizo kweli tena kubwa.

Viongozi wa dini hapa wanatakiwa waongeze bidii katika maombi ili kuwa na taifa na watu wakweli na wanaotoa haki kwa wote bila kubagua, ikitokea na viongozi wa dini wakawepo wasio wakweli ni tatizo lingine ambalo kama waumini hawatang'amua ni balaa. Kuna mambo mengi yanayoonyesha uongo kupambwa na kutaka kuwaminisha watu kuwa ni ukweli tena wakati mwingine kwa mambo ya hatari kabisa.

Tuendelee kuchangia kwani mimi kwa upande wangu naona kusimamia ukweli na haki kwa wote kutatupeleka mbali kimaendeleo kama taifa. Nitoe mfano kwanini watu wanawashabikia watu walio na mali ambazo inajulikana kabisa kuwa wamewadhulumu wengine kama watoto kukosa dawa hospitalini kwa sababu ya ufisadi. Ajabu nyingine watu wanawasema vibaya kwa kuwabeza watumishi wanaotenda wema bila ufisadi ila watastaafu maskini.
Nina mengi ngoja niishie hapa karibuni wote tuijadili hoja hii.
 
Ujerumani Magharibi na Mashariki vilitengana kwa muda mrefu kutokana na uchonganishi wa uongo na walipogundua ukweli walivunja ukuta na kuungana upya ambapo sasa ni Ujerumani moja yenye maendeleo.
 
Marekani Imeendelea kwa Kupindisha Ukweli, Ilienda Iraq kuchota Mafuta ikapindisha eti inaenda kusaka Silaha za Maangamizi, Kwenye Marshal Plan after Second Worl War iliwahadaa Watu wa Europe hasa Engalnd chini ya Winston Churchil eti wazipe uhuru nchi za Afrika ili zijitawale kumbe Lengo watutawale In direct, Hakuna Taifa lililoendelea Bila ya Propaganda na Kiufupi Propaganda ni kupindisha ukweli
 
Marekani Imeendelea kwa Kupindisha Ukweli, Ilienda Iraq kuchota Mafuta ikapindisha eti inaenda kusaka Silaha za Maangamizi, Kwenye Marshal Plan after Second Worl War iliwahadaa Watu wa Europe hasa Engalnd chini ya Winston Churchil eti wazipe uhuru nchi za Afrika ili zijitawale kumbe Lengo watutawale In direct, Hakuna Taifa lililoendelea Bila ya Propaganda na Kiufupi Propaganda ni kupindisha ukweli
Hizo ni mbinu za kiuchumi sasa nchi za Afrika zinapindisha ukweli kwa watu wake si ni kujididimiza badala ya mbinu za maendeleo kwa nchi na watu wake?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom