Je, kuna taasisi au NGO's zinazohusika na re-entry programs kwa wafungwa wanaorejea uraiani?

Hakimu Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2018
Messages
1,272
Points
2,000

Hakimu Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined Oct 30, 2018
1,272 2,000
Toka Rais Magufuli ameingia madarakani kafanya jitihada zake binafsi kubwa za kupunguza msongamano wa wafungwa kwenye magereza yetu hasa kwa kuwapa msamaha wafungwa maelfu kwa maelfu kila inapotokea sherehe ya kitaifa kama uhuru au muungano.

Juzi rais kavunja rekodi kwa kuachia idadi kubwa sana ya wafungwa(30%) kurudi uraiani na hasa wengi ni wale waliokua wamefungwa miaka mingi, zaidi ya miaka 15. Nimeona kwenye vyombo vya habari vingi wafungwa wakitoa ushuhuda na wengi ni wa miaka mingi sana wamekua gerezani.

Cha kunisikitisha zaidi baada ya furaha kuu ya juzi ya msamaha wa wafungwa, sasa tunasikia tena wafungwa wengi waliosamehewa wakikamatwa kuhusika na matukio ya uhalifu na wengine wakikataa kutoka magereza. Je hawa wafungwa tunaowaachia kuja huku nje kuna mafunzo au program maalum za kuwasaidia kukabiliana na maosha ya uraiani ambayo hawajayaishi kwa miaka mingi na hawayajui?

Mfano mtu alifungwa mwaka 1978, mwingine 92, hata simu za mkononi tu hazikuwepo kabisa Tanzania, leo unamrejesha uraiani, unategemea atakabiliana vipi na maisha haya bila mafunzo maalumu ya kumuwezesha ili asirudie tena kwenye uhalifu?

Je, kuna NGOs au taasisi zinazohusika na re-entry programs kwa wafungwa wa zamani kuwasaidia wasirudi kule walikotoka? Au ndio vile kua atajijua mwenyewe huko?
 

Forum statistics

Threads 1,392,185
Members 528,564
Posts 34,101,118
Top