Je, kuna somo ambalo hutakuja kulisahau kwa jinsi lilivyokutoa jasho?

Fohadi

JF-Expert Member
Jul 24, 2020
770
2,408
Kila mtu ana somo ambalo halikuwahi kuwa rahisi kwake. Labda kwa wachache ambao ni exceptional wanaweza wasiwe walikutana na hii situation.

Nimekumbuka enzi zangu nipo chuo. Katika harakati zangu za kuijenga future yangu nikabahatika kutua kwenye chuo kimoja wapo kikubwa hapa nchini kwa course ya miaka 3.

Harakati zikaanza, siku zikaenda nikafanikiwa kuingia mwaka wa pili hapa sasa ndipo nilikutana na ugumu na kuiona elimu ngumu...

Sitakuja kulisahau somo moja linaitwa ECONOMETRICS. Kwa wale waliosoma Economics au course zenye uhusiano na economics watakuwa wanalielewa hili somo. Kwa course yangu na department yangu nilipokuwa. Hili ni moja wapo ya masomo ambayo huwa 'yanawakamata' watu wengi sana.

Ingawa nilibahatika kulifaulu vizuri chamoto nilikiona na nilinyoosha mikono juu.

 
Hahaaaaha kwawale walisoma engineering ( mechanical, automobile, irrigation etc) watakua wanaelewa unondo wa stregh of material na thermodynamics ni hatar....
hatari sana mkuu..kuna muda ukiona mwenizo yuko mwaka wa mbele kuliko wewe au amegraduate..unaanza kujiuliza amewezaje au amefikaje kule..na usiombe ukutane na page za motivational speakers ukiwa katika situation hiyo, unaweza tamani kudrop chuo kwasababu unahisi kama unachelewa maisha
 
Dahh Hadi kesho kutwa sitokuja kusahau, nimeingia zangu chuo semester ya Kwanza nikakutana na bwana biochemistry, huyu jamaa Hadi leo nampa respect yake maana alichokuwa ananifanyia kwenye examination sio poa

Cat One nakuta nimepata 8%, dahh nikachanganyikiwa Ila nikasema fresh nitamake Tu next cat, ohhh cat 2 ikaja nimekula 7%, Kwa ufupi nilikuwa sielewi hii Ngoma pamoja na kuwekeza nguvu kubwa kwenye kuisoma Ila wapi, nikaona litanipotezea mood ya shule hili ata Kwa masomo mengine

Baada ya kufanya cat kama 3 na zote nikiwa sijawahi kupata 10, ikabid niache kabisa kusoma biochemistry na nikaiweka kwenye kundi ambalo lazima nitakuja kusapua, nikawa naenda Tu kufanya cat narudi zangu hostel na Hadi semester inaisha nina average ya 7, nikasema hii Ngoma nitaiwekea special force kipindi cha September conference Ila Kwa sasa niiangalie Tu kama manzi ya lecturer

Wakati nasoma level zote nilikuwa na kauli mbiu yangu ya kujifariji maana sikuwahi kuwa serious na shule, hivo watu wangu wa karibu walikuwa wananionea huruma sana na kunisihi nisome lasivyo nitafeli, Ila Mie nilikuwa nawajibu "kufaulu ni TABIA ya mtu, kama huna TABIA ya kufaulu utatumia nguvu kubwa Sana kufaulu Ila kama Una TABIA ya kufaulu basi utafaulu Tu we usiulize HOW"
 
Back
Top Bottom