Je kuna sheria ya kusikiliza simu zinazoingia Tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je kuna sheria ya kusikiliza simu zinazoingia Tanzania?

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Richard, Aug 2, 2010.

 1. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #1
  Aug 2, 2010
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 7,750
  Likes Received: 3,524
  Trophy Points: 280
  Kuna habari ambazo nilizipata kutoka kwa mmoja wa "reliable sources" wangu kwamba simu zote zinazoingia Tanzania hasa zile za kutoka Ulaya Magharibi huwa zinasikilizwa na kuchujwa na kisha kufanyiwa kazi.

  Kitendo cha kusikiliza simu za wananchi kwa siri bila ridhaa yao kinaitwa kwa kiingereza "Eavesdropping" au "wiretapping".

  Ni pale embapo waya wa kusikilizia mazungumzo ya wananchi unaambatanishwa na waya wa simu wa kawaida au ule wa simu za karatasi telefax au telegram, email, instant messaging na njia zingine za mawasiliano zinazochukuliwa kuwa ni binafsi.

  Sasa je kuna sheria ambazo zimepitishwa na bunge kuruhusu vyombo vya usalama viweze kufanya kazi yao hasa ya kufuatilia watu ambao ni tishio kwa usalama wa nchi na sio vinginevyo?

  Hio ni moja tu ya mbinu ya vyombo vya usalama katika kufuatilia mienendo ya wananchi tufuatao na kutii sheria za nchi sasa ni nani ana haki ya kusikiliza au kufuatilia mawasiliano ya mwenzie bila ridhaa yake?
   
 2. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #2
  Aug 2, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,780
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160

  Mkuu Richard:

  Kuna post moja ya mwaka jana MMKJJ: Yaweza kukupa mwanga zaidi

  https://www.jamiiforums.com/jamii-intelligence/30198-wanaharakati-ziachieni-simu-za-vodacom.html

   
 3. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #3
  Aug 2, 2010
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 7,750
  Likes Received: 3,524
  Trophy Points: 280
  Nashukuru sana kwa hili. Je ni hawa Vodacom tu ndio wanakuwa "implicated" hapa au wale watoa huduma wote wa simu za mikononi?
   
 4. N

  Nyanzura Member

  #4
  Aug 2, 2010
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mkuu Richard,
  Siyo VODACOM tu, nadhanai ni watoa huduma wote. Nimeshuhudia hili mimi mwenyewe TIGO na ZAIN pia.
   
 5. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #5
  Aug 2, 2010
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 4,959
  Likes Received: 440
  Trophy Points: 180
  Bongo kuna sheria kwani? Tena sasa hivi wameregister namba za watu lazima mambo ya blackmail yataongezeka sana, cha kufanya ni kwenda kwa encryption kama kitu kiko sensitive.
   
 6. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #6
  Aug 2, 2010
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 7,750
  Likes Received: 3,524
  Trophy Points: 280
  Mimi nafikiri kuna upungufu mkubwa sana kwenye makampuni ya simu za mikononi, kwamba hawawi makini katika kuhakikisha simu za wananchi zinakuwa ni siri kati ya wanaozungumza.

  Lakini kama kuna sheria inayowaonya wamiliki wa mitambo ya simu za mikononi kwamba ni lazima wawe wanairekebisha kiusalama kuzuia "eavesdropping" na kuhakikisha mitambo yao inakuwa up-todate.

  Simu za mikononi zinalindwa na system ambayo inatumia namba nyingi kwenye mafumbo (encryption) pale mtu anapokuwa ameandika ujumbe (text message) au kutuma sauti yake kwa upande wa pili kwenye simu ingine anapoacha ujumbe wa sauti (voicemail message) na hivyo kuzuia udondoaji "eavesdropping".

  Ni pale muda mwingi unapotumika kufumbua au (decryption) ndio kunazuia eavesdroping lakini ikiwa system za operators wa iwe voda na wengine zinakuwa up-todate. Lakini hali ni tofauti kabisa Tanzania ambapo watu wanafanya vitu bila kufuata sheria.
   
 7. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #7
  Aug 2, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  Nadhani nadhani
  Sheria zozote zinazofanya hii kitu zimajeificha kwneye mgongo wa sheria za Kijasuzi na usalama wa nchi. Na mambo ya usalama wa taifa nchi nyingi yamefunikwa funikwa hata mabunge hayapewi nafasi ya kujadili na kuyachambua. N mwisho wa siku serikali iko above the law.

  Kwa kampuni binafsi au mtu binafis kufanya wiretapping ni kosa lakini kampuni za simu zinaweza kushinikiwa kurekodi mazungumzo ya watu fulani. na serikali. Au kufanya hivyo kwa manufaa wanayojua wenyewe

  May be kampuni hizi za simu zinalipwa hela nzuri tu na mashirika ya a kijasusi eg CIA kwa kuwasilisha tape za simu zilipigwa/ kupokolewa kutoka nje.

  Lakini hivi leo kwa maendeleo ya Teknolojia kuna vifaa unaweza kuvinunua kwaabei nafuu vinawawezesha watu binafsi mfano kupata call register za watu mtu mwenye number fulani aliowasilina nao na sms.

  Kuna kampuni nyingine zina mitandao ukijisajili kwa kiasi kidogo ukiandika number unayotaka kumonitor utatumiwa Sms ulizotuma na kupokea .
   
 8. Shy

  Shy JF-Expert Member

  #8
  Aug 2, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,238
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Kampuni zote za simu huwa zinaweka rekodi ya kile unachofanya na simu yako kupitia mtandao wao wa simu na huwa wanakwambia kabisa kwamba unachofanya kinaweza kurekodiwa kwa sababu fulani fulani mfano za masuala ya kodi unaponunua vocha kuongea na huduma zingine nyingi kwa kutumia simu yako --

  Lakini msiwe na shaka sheria nyingi zinazomlinda mteja anapotumia huduma za mawasiliano zinakuja na zitaweza kunufaisha wengi haswa wanaharakati

  Kuna siku moja nilitoa namba yangu ya simu kwa mwanachama mmoja wa jf miaka 3 iliyopita kutokana na kuandika mada fulani basi nilipofuatilia kwenye mtandao wangu kujua namba hiyo ni ya nani manake ilikuwa private wakasema natakiwa kuonana na mwanasheria wao anisainishe ndio nipewe taarifa zaidi toka siku hiyo naogopa prvt nambas
   
 9. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #9
  Aug 2, 2010
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 7,750
  Likes Received: 3,524
  Trophy Points: 280
  Mimi nakumbuka baada bomu kuharibu na kuharibu jengo la ubalozi wa marekani pale Dar na baadae kulipotulia kukawa na malalamiko kwamba wananchi waliokuwa wakiishi maeneo ya jirani walikuwa wakilalamika kwamba walligundua kwamba wapo chini ya Surveillance kutoka kwa ubalozi wa marekani ulipokuwapo pale Kenyata Road.

  Ok tuachane na hayo, kwa mfano bunge la USA wao mwaka 2008 walipitisha sheria inayoitwa "anti-terrorism wiretaps" ambayo inawalinda wenye makampuni ya simu endapo yatashtakiwa kwa kurekodi simu za watu bila idhini yao. Sasa utaona sheria hii inahusiana na masuala ya ugaidi.

  Nchi za ulaya kama UK inazingatia sheria iitwayo Regulation of Investigatory Powers Act ya mwaka 2000 ambayo inaipa uwezo serikali kufanya "wiretaping", na hapo pana utaratibu wa kuhakikisha haki za msingi chini ya sheria iitwayo "European Convention on Human Rights" chini ya sehemu ya nane au artical 8 ambayo inasema kama ifuatavyo:

  ARTICLE 8

  1.Everyone has the right to respect for his private and family life, his home and his correspondence.

  2.There shall be no interference by a public authority with the exercise of this right except such as is in accordance with the law and is necessary in a democratic society in the interests of national security, public safety or the economic well-being of the country, for the prevention of disorder or crime, for the protection of health or morals, or for the protection of the rights and freedoms of others.

  Nchini Ufaransa ni lazima jaji atoe uamuzi wa kufanya wiretaping ingawa wakati mwingine serikali hu-bypass na kufanya itakavyo kutegemea na aina ya suspect anaehusika.

  Nchini Uholanzi polisi wanafanya wiretaping iwapo tu kuna serious kesi na nchini Ugiriki ni hivyohivyo.

  Sasa kwa nchi yetu na kujua kama kuna taratibu hizi bila kuiga bali kuelewa taratibu za wenzetu bado sifahamu iwapo sheria zinapitishwa na bunge kulinda uhuru wa wananchi bila kuwaingilia.
   
 10. Shy

  Shy JF-Expert Member

  #10
  Aug 2, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,238
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Angalia attachment ya kipindi cha jana SHERIA MTANDAO tulizungumzia suala hilo na hatua zilizofikia mpaka sasa hivi haswa juu ya afrika mashariki yote kuwa na sheria zao za jumuiya lakini majadiliano hajaisha mengine yatazungumzwa jumapili ijayo ungekuwa tanzania ingependeza kwa sababu ungeweza kuwa mchangiaji mzuri wa kipindi
   
 11. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #11
  Aug 2, 2010
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 7,750
  Likes Received: 3,524
  Trophy Points: 280
  Sawa mkuu, kwa hio nielewe kwamba hakuna sheria yoyote mpaka sasa!
   
 12. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #12
  Aug 2, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  Sheria Ipo kwa siri kali tu. ila ukiuliza utajiwe kifungu usshange hutaona neno wire taping wala eavedroping. "wanaruusiwa kutumia raslimaliz zozote kulinda usalama wa nchi" Unajua hata sheria isiyokuwepo kuna kifungu kitaicover tu teh teh teh. Hapo Learned brother/sister ndo wanapotuibiaga

  Shy
  Kuhusu makampuni ya ni kosa kurekodi mawasiliono ispikokuwa kama mteja kawapigia wao yaani kampuni husika hapo sawa. Ni kosa kwa Kampuni XXX kurekokdi mazungumzo ya Shy na Mtazamaji bila ridhaaa yao. Otherwise labda wawe wameamrishwa /kuagizwa na siri kali kufanya hivyo.
   
Loading...