Je, kuna sheria kamati ya nidhamu kumvua mtu ubunge?

Chibudee

JF-Expert Member
Dec 28, 2016
1,775
2,400
Salaam wakuu, kwanza poleni sanaa kwa uzuni tulizonazo kwa kuondokewa na mzee wetu Ndesamburo

Niende kwenye lengo kutokana na vuta nikuvute kati ya Bulaya, Mdee na Mnyika
kamati ya maadili imewapa adhabu kutohudhuria vikao kadhaa vya bunge.

Lakini pia haijaishia hapo kuna baadhi ya wabunge wametokwa mapovu wakidai watuhumiwa hawa kufutwa kabisa ubunge.

Naomba kwenda kwenye swali... Je, kuna sheria inayoruhusu kamati ya maadili kumvua ubunge mbunge?

Na kama ipo inaangalia vigezo gani?
Na hatua zipi za makosa na makosa ya aina gani?

Wataalam mtusaidie hapa

Nawasilisha
 
Ni UPOFU na UJUHA wa wasiojua sheria ama kudhani wao ni SHERIA kukimbilia KUFIKIRIAkuwavua wenzao Ubunge..
 
Kiukweli wanatamani sana kufanya hivyo kwa kuwa hao wanamama wawili ni mwiba sana kwa 'Team Ndiooooo'. Lakini hizo ni porojo tu za Dodoma, Ubunge wamepewa na wananchi.

Ukiangalia sana, mashabiki wengi wa azimio hilo ni wabunge wa vitu maalum. Wanadhani na Mdee naye kapewa ubunge kama shukrani za kampeni.
 
kiujumla bado maswali ni mengi kuliko majibu. inakuwaje mbunge azuiwe na wabunge wenzake kuwawakilisha wananchi wake waliomchagua?
 
Salaam wakuu kwanza poleni Sanaa kwa uzuni Tulizo nazo kwa kuondokewa na Mzee wetu ndesamburo

Niende kwenye lengo kutokana na vuta nikuvute kati Ya bulaya Mdee na mnyika
Kamati Ya maadili imewapa adhabu kuto hudhuria vikao kadhaa vya bunge

Lakini pia haijaishia hapo Kunabaadhi Ya wabunge wametokwa mapovu wakidai Watuhumiwa hawa kufutwa kabisa ubunge

Naomba kwenda kwenye swali je??
Kunasheria inayo ruhusu kamati Ya maadili kumvua ubunge mbunge ???

Nakama ipo inaangalia vigezo gani?
Nahatua zipi za makosa namakosa ya aina gani ?? Wataalamu Mtusaidie hapa

Nawasilisha :

Kwani Bungeni wamepelekwa na Kamati ya Maadili ya CCM au sisi wana nchi ndiyo tumewapeleka.!Wapelekeeni meseji kwamba na mwaka 2020 titawapeleka hao hao.
 
kiujumla bado maswali ni mengi kuliko majibu. inakuwaje mbunge azuiwe na wabunge wenzake kuwawakilisha wananchi wake waliomchagua?
Nashangaa sanaa mkuu alafu hao wanao waita wenzao watomvu wa nidhamu washafanya mambo yaaajabu haijapata kutokea

Kama spika alisha mtifua mwenzie rungu adi kuzimia kisa siasa tu

Kweli shetani hawezi kuzaa mtoto malaika
 
Back
Top Bottom