Je kuna Parents stock ya kuroiler Tanzania kwa ajili ya kutoa F1?

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
7,789
8,914
Kwanza Tambua kwamba F1 au First generation hutoka kwenye Parents stock pekee.

Parents stock ndo huzaa F1.na parents stock huagizwa nje na parents stock hutoka kwenye Grand Parents.

Grands parents ndo hutoa parents stock na Parents stock hutoa F1.

kwa Tanzania acording to Keg Farm kuna kampuni 1 waliuzia Parents srock wa Kuroiler.
 
Sasa kwa kuku chotara bila kununua F1 unakuwa hujafuga na tegemea hasara za kutosha kama huna F1
 
Ni kampuni gani hiyo mkuu,wengi mtaani utasikia anauza kuku kuroiler na mayai yake.
 
Kuna sehemu moja nilienda kuulizia kuku,namuuliza kuku wako ni aina gani? Ananiambia chotara,chotara wa aina gani? Anasema chotara tu! Dah hata hamu ya kununua kwake ikawa imekwisha.
 
Kwanza Tambua kwamba F1 au First generation hutoka kwenye Parents stock pekee.

Parents stock ndo huzaa F1.na parents stock huagizwa nje na parents stock hutoka kwenye Grand Parents.

Grands parents ndo hutoa parents stock na Parents stock hutoa F1.

kwa Tanzania acording to Keg Farm kuna kampuni 1 waliuzia Parents srock wa Kuroiler.
Ni Nzua Poultry farm ipo Dar es salaam. 0712705839
 
kuna jamaa (duka la mifugo) maeneo ya Tegeta wameweka tangazo wanauza F1 kuroiler.....nafikiri ni hao Nzua kama mchangiaji hapo juu alivyosema.
 
Wanazo Document za kuagiza Parents stock? make wale sio kwa kutamka bali lazima uonyeshe vibali
Nina wafahamu na hatua zote za kuingiza hao kuku kutoka India wamefuata taratibu za nchi, na Wahindi wenyewe walikuja kusaidia kwenye matunzo ya awali ya vifaranga hao.
 
Muhimu document mkuu, bila hio kitu ni ujanja ujanja tu. Hata Kegg farm wametoa sample ya Certificate wanayotoa kwa mtu, taasisi au kampuni yoyote itakayo nunua Parent Stock ya Kuroiler. Ukienda hapo Nzua hakuna hio Certificate zaidi ya bango tu ambalo unaweza ukatengeneza hata ukiwa upo nyumbani kwako.
 
Attachments

  • certificate.jpg
    certificate.jpg
    6.6 KB · Views: 111
Muhimu document mkuu, bila hio kitu ni ujanja ujanja tu. Hata Kegg farm wametoa sample ya Certificate wanayotoa kwa mtu, taasisi au kampuni yoyote itakayo nunua Parent Stock ya Kuroiler. Ukienda hapo Nzua hakuna hio Certificate zaidi ya bango tu ambalo unaweza ukatengeneza hata ukiwa upo nyumbani kwako.
Toa unayoijua maana kila kitocholewacho kinaonekana sicho na unakijua
 
kuna kampuni inaitwa GMK Glitters ofisi ziko karibu na Mlimani city jaribu kucheki nao.
 
Back
Top Bottom