Je, kuna mzungu au mwarabu ana jina la kiafrika?

Hebu tuhoji hapa, wengi wetu tuna majina ya Peter, Anna, John, Hamad, Ashura, Hassan nk. Haya ni majina ya kigeni na tumeyatupilia mbali majina yetu mazuri ya Urio, Nyangeta, Ndikumana, Chacha, Bhoke, Masawe, Kabwe nk.
Je, hawa wageni waliotuletea hizo tamaduni zao na kuziona zetu za kishamba wana majina Kama ya asili yetu?
Wazazi vijana tunakwama wapi kuwapa majina asilia watoto tunaowazaa?
Tunahitaji nini walau hili la majina tujikomboe?
SATO alikuwa balozi
MASAKI alikuwa balozi
KAZIMOTO alikuwa balozi
KAZINYINGI
hawa wachache ila nina majina mengi sana mengine tutalaumiana bure.
 
Na aliyekuletea habari ya malaika mkuu Gabriel ni nani??
Malaika Mkuu Gabrieli (mjumbe wa Mungu); Malaika Mkuu Mikaeli (nani aliye kama Mungu?); Malaika Mkuu Raphael (Mungu ni kinga yangu)! Mengine ni majina ya malaika na sio ya kizungu tu Mkuu. Kwani hata Emmanuel si limetajwa - Mungu pamoja nasi?
 
Jina la Sia lipo kwa wazungu pia. Kuna majina ni kama coincidence yapo kwa waafrika na wazungu pia. Mfano jina la Tatu wafinland Tatu ni jina la mwanaume kama sijakosea. Hii kwa mujibu wa mfin mwenyewe.
Mkuu... naunga mkono hoja. Mfano mwingine ni Gurisha Liko Bongo, Ásia... Rwanda...
 
Sijui kama na jamii zengine zinajari asili za majina kama sisi,ila nachojua jina ni neno lolote la kumtaja mtu au kitu na hakuna cha ziada kwenye jina(neno) zaidi ya maana ya hilo neno ambalo limetumika kama ndio jina. Na ndiyo maana utakuta baadhi ya majina ya watu yana maana ya matusi kwenye lugha za watu wengine hufanya kuwa tabu kutamka hayo majina.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom