Je, kuna mzungu au mwarabu ana jina la kiafrika?

Malaika Mkuu Gabrieli (mjumbe wa Mungu); Malaika Mkuu Mikaeli (nani aliye kama Mungu?); Malaika Mkuu Raphael (Mungu ni kinga yangu)! Mengine ni majina ya malaika na sio ya kizungu tu Mkuu. Kwani hata Emmanuel si limetajwa - Mungu pamoja nasi?

Nafanya kazi na mzungu Zakarias au Zackary
Upo sahihi kabisa
 
Mzungu hataki ujue historia yako na ndio maana kubadili majina ilikuwa ni moja ya njia maalum ya wewe kusahau ulipotoka. Wao wanabaki na historia yao vizuri tu lakini sisi tunabaki empty
Wapuuzi hawa jamaa!
 
Kuna kitu muelewe watu. Kuna majina yanaingiliana. Mifano hasa majina ya wajapani na baadhi ya majina ya wazungu. Mfano jina la Maruri ni mavumbi kwa watu wa kabila la Warangi na waitaliano wana Maruri pia.
Na yale yanayofanana na sehemu za Siri ya kijapani, yanafanana na majina ya kiswahili
 
Haya majina yalibadilika wakati wa utumwa ili msikumbuke asili zenu na mababu wakapewa majina ya waliokuwa wanawamiliki
Hivyo hata Mweusi akiwa usa akitaka kujua asili yake ni nchi gani ya Africa hawezi kuipata kwani ni karne zimepita
Hapo usithubutu kumwambia eti wewe ni mwafrika?
Atakuambia I am American au I am British
 
Kuna padri mmoja wa Kanisa Katoliki, amesomea mambo ya mila na utamaduni na utamadunisho (inculturation) na amefanya utafiti wake nchini Malawi tangu miaka ya 60 na anaongea Chichewa (fasaha) vizuri zaidi (nadhani) kuliko watu wengi wa Malawi na kwa sababu ya kuwa karibu na watu wa huko na kujua mila na utamaduni wao na lugha yao amepewa jina la Chichewa, Chisale. Anaitwa Padri Claude Boucher (French Canadian). Yuko Mua Mission (Dedza) na hapo ameanzisha kituo cha mila na utamaduni kinaitwa KuNgoni. Amekua authority kwa lugha ya Chichewa pamoja na mila na tamaduni za Wachewa, Wangoni na Wayao. Abambo Chisale ni Padri wa Shirika la Wamisionari wa Afrika (zamani waliitwa White Fathers).

Padri Chisale alianzisha kituo hiki cha utamaduni pengine kwa kuwa 'inspired' na Padri David Clement (ambaye pia alikuwa French Canadian) aliyeanzisha Kituo cha Mila na Utamaduni kule Mwanza kinachoitwa Bujora Cultural Centre. Padri Clement naye alikuwa shirika la Wamisionari wa Afrika (White Fathers). Naye aliitwa pia Padri Fumbuka.
Hizi kitu zinatakiwa ziwe Pana na ziwafikie na wazungu nao wafananie walivyotubatiza sie!
 
Jakaya Mrisho Kikwete.
Kwa hili jina atabarikiwa mpaka kaburini,sio mnazaa mitoto mnayaita kina Ciprian yanaleta tabu tu duniani.
TUNDU LISSU
Haya nyie mitoto yenu mkaipa majina ya livingstone ona li lusinde lilivojinga.
Leo unalipa toto jina Amber Lutty halafu unataka awe msomi una akili kweli?
Mkuu umelichunguza na jina lako?
 
Hayo sio majina ya kizungu na mzungu nae dini mapokeo tu sio dini yake wapo wazungu wanatumia majina ya kitaifa lao na wapo wanatumia majina ya kiafrica pia hata wao wanaiga mkuu fanya utafiti vizur taratibu mkuu kumbuka hilo mzungu dini sio yake mkuu
Catholic ni dini ya watu gani? What about Anglican, Lutheran nk? Yote haya ya wazungu na ndio waliotuletea huu utaratibu wa kubatiza majina ya kigeni
 
Ata simu unayotumia hapa ni technologia ya wazungu. Nguo ulizovaa ni tamaduni ya wazungu. Nenda ukavar magome ya miti
 
Na makanisa yao uchwara haya ukitaka kumbatiza mtoto, paroko anakwambia umpe mtoto jina la kizungu sio la kitanganyika. Ukigoma hakuna ubatizo!
 
Hebu tuhoji hapa, wengi wetu tuna majina ya Peter, Anna, John, Hamad, Ashura, Hassan nk. Haya ni majina ya kigeni na tumeyatupilia mbali majina yetu mazuri ya Urio, Nyangeta, Ndikumana, Chacha, Bhoke, Masawe, Kabwe nk.

Je, hawa wageni waliotuletea hizo tamaduni zao na kuziona zetu za kishamba wana majina Kama ya asili yetu?

Wazazi vijana tunakwama wapi kuwapa majina asilia watoto tunaowazaa?

Tunahitaji nini walau hili la majina tujikomboe?
Nani alikudanganya kuwa Waarabu ni wageni Afrika?

Mitaala ya kurithi wazungu imewajaza sana ujinga.

Hakika hizi shule za kufundisha uhinga zimewajaza sana ujinga.

Hebu jisomee watafiti ambao hawajakusomesha ujinga wanasemaje...

 
Ata simu unayotumia hapa ni technologia ya wazungu. Nguo ulizovaa ni tamaduni ya wazungu. Nenda ukavar magome ya miti
Si kweli. Soma kuhusu algorithms. Bila algorithms hauna kompyuta wala simu hizi za leo.

Soma ujionee ni na nani mvumbuzi wa algorithms.

Sijuwi huwa mnakurupuka vipi kwa mamvo msiyoyaelewa na kujifanya mna majibi ya kila kitu bila kuweka "citations". Mambo mengine siyo ya kukurupuka.

Soma hiyoooo...

 
Si kweli. Soma kuhusu algorithms. Bila algorithms hauna kompyuta wala simu hizi za leo.

Soma uhionee ni na nani mvumbuzi wa algorithms.

Sijuwi huwa mnakurupuka vipi kwa mamvo msiyoyaelewa na kujifanya mna majibi ya kila kitu bila kuweka "citations". Mambo mengine siyo ya kukurupuka.

Soma hiyoooo...

Nishaona jina la kigeni kwenye hiyo link, kumbe ni wale wale tu!
 
We ni mpumbavu wa mwisho. Nani alikuambia hao wazungu ni WATAKATIFU??

Ni wazi hujaelewa nilichomaanisha, rudia kujifunza tofauti ya MIZIMU na WATAKATIFU mi sijaegemea upande wowote.... matusi ni ishara ya kupaniki.

NYWANOKO.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom