Je, kuna mzungu au mwarabu ana jina la kiafrika?

Mzungu hataki ujue historia yako na ndio maana kubadili majina ilikuwa ni moja ya njia maalum ya wewe kusahau ulipotoka. Wao wanabaki na historia yao vizuri tu lakini sisi tunabaki empty
 
Malaika Mkuu Gabrieli (mjumbe wa Mungu); Malaika Mkuu Mikaeli (nani aliye kama Mungu?); Malaika Mkuu Raphael (Mungu ni kinga yangu)! Mengine ni majina ya malaika na sio ya kizungu tu Mkuu. Kwani hata Emmanuel si limetajwa - Mungu pamoja nasi?
Hayo majina yatafute asili kwanza yalikuwa ya kiebrania na hawayaandiki hivyo ulivyoandika
 
Majina ya asili yetu ya mababu wafu(mizimu), bali majina ya kizungu ambao pia ni wafu (watakatifu).... ukielewa tofauti kati ya mizimu na watakatifu utakuwa katika uelekeo wa kujikomboa.
We ni mpumbavu wa mwisho. Nani alikuambia hao wazungu ni WATAKATIFU??
 
Unajua maana ya Sia wewe?hapo kwanza ni jina la kabila la wachaga hakuna uzungu hapo
Jina la Sia lipo kwa wazungu pia. Kuna majina ni kama coincidence yapo kwa waafrika na wazungu pia. Mfano jina la Tatu wafinland Tatu ni jina la mwanaume kama sijakosea. Hii kwa mujibu wa mfin mwenyewe.
 
Kuna kitu muelewe watu. Kuna majina yanaingiliana. Mifano hasa majina ya wajapani na baadhi ya majina ya wazungu. Mfano jina la Maruri ni mavumbi kwa watu wa kabila la Warangi na waitaliano wana Maruri pia.
 
Clemens Mulokozi - Founder of Jambo Bukoba NGO.

Nyamiasa Azikiwe - Assistant Chief Editor at Warner Bros Cables.

Munjago Afifi Rutta - Secretary of Police Academy in Saõ Paulo.
 
Hebu tuhoji hapa, wengi wetu tuna majina ya Peter, Anna, John, Hamad, Ashura, Hassan nk. Haya ni majina ya kigeni na tumeyatupilia mbali majina yetu mazuri ya Urio, Nyangeta, Ndikumana, Chacha, Bhoke, Masawe, Kabwe nk.

Je, hawa wageni waliotuletea hizo tamaduni zao na kuziona zetu za kishamba wana majina Kama ya asili yetu?

Wazazi vijana tunakwama wapi kuwapa majina asilia watoto tunaowazaa?

Tunahitaji nini walau hili la majina tujikomboe?
Kuna padri mmoja wa Kanisa Katoliki, amesomea mambo ya mila na utamaduni na utamadunisho (inculturation) na amefanya utafiti wake nchini Malawi tangu miaka ya 60 na anaongea Chichewa (fasaha) vizuri zaidi (nadhani) kuliko watu wengi wa Malawi na kwa sababu ya kuwa karibu na watu wa huko na kujua mila na utamaduni wao na lugha yao amepewa jina la Chichewa, Chisale. Anaitwa Padri Claude Boucher (French Canadian). Yuko Mua Mission (Dedza) na hapo ameanzisha kituo cha mila na utamaduni kinaitwa KuNgoni. Amekua authority kwa lugha ya Chichewa pamoja na mila na tamaduni za Wachewa, Wangoni na Wayao. Abambo Chisale ni Padri wa Shirika la Wamisionari wa Afrika (zamani waliitwa White Fathers).

Padri Chisale alianzisha kituo hiki cha utamaduni pengine kwa kuwa 'inspired' na Padri David Clement (ambaye pia alikuwa French Canadian) aliyeanzisha Kituo cha Mila na Utamaduni kule Mwanza kinachoitwa Bujora Cultural Centre. Padri Clement naye alikuwa shirika la Wamisionari wa Afrika (White Fathers). Naye aliitwa pia Padri Fumbuka.
 
Majina mengi hasa ya Kikristu yanatokana na Dini ambayo ililetwa na hao wazungu kwahiyo wengi tukibatizwa kanisani tunapewa yale majina ya dini husika iliyokuja na mzungu. haya mangine ya akini mwakitenkimwakilipuka hayaapo kwenye biblia.
you made my day
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom