Je, kuna mzungu au mwarabu ana jina la kiafrika?

Mkuu majina hayo tunayoyaita sisi kwa kychukua kutoka kwao, kama utaitwa kwa Kiswahili utalibadilisha siku hiyo hiyi, mfano: Seif kwa Kiarabu ni upanga, Hassan maana yake ni mwema/mzuri. Yako mengi. Wazungu wenyewe husema what is in a name? Sisi Waswahili tunasema "jina si mboje".
 
Majina ya asili yetu ya mababu wafu(mizimu), bali majina ya kizungu ambao pia ni wafu (watakatifu).... ukielewa tofauti kati ya mizimu na watakatifu utakuwa katika uelekeo wa kujikomboa.
 
Ukiangalia kwenye world cup kuna wazungu kibao wa America ya kusini, na baadhi ya nchi za ulaya wanamajina ya kiafrika
 
Hebu tuhoji hapa, wengi wetu tuna majina ya Peter, Anna, John, Hamad, Ashura, Hassan nk. Haya ni majina ya kigeni na tumeyatupilia mbali majina yetu mazuri ya Urio, Nyangeta, Ndikumana, Chacha, Bhoke, Masawe, Kabwe nk.

Je, hawa wageni waliotuletea hizo tamaduni zao na kuziona zetu za kishamba wana majina Kama ya asili yetu?

Wazazi vijana tunakwama wapi kuwapa majina asilia watoto tunaowazaa?

Tunahitaji nini walau hili la majina tujikomboe?
Govinda
 
Nilikuwa sehemu ya kutoa huduma, nilikuwa ninaita majina ya watu. Jina la mwisho lilikuwa
Aisher Abdul. Nimetoka ninaita Aisher Abdul nikitegemea she mwanamke na hijab, alitokea mama wa kizungu na jeans.
Huyu atakua alislim akiwa huko Madina
 
Majina ya asili yetu ya mababu wafu(mizimu), bali majina ya kizungu ambao pia ni wafu (watakatifu).... ukielewa tofauti kati ya mizimu na watakatifu utakuwa katika uelekeo wa kujikomboa.
Kwa hiyo waafrika hakuna watakatifu? Hii dharau sasa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom