Je, kuna mzungu au mwarabu ana jina la kiafrika?

Jumong S

JF-Expert Member
Jul 3, 2013
7,312
10,492
Hebu tuhoji hapa, wengi wetu tuna majina ya Peter, Anna, John, Hamad, Ashura, Hassan nk. Haya ni majina ya kigeni na tumeyatupilia mbali majina yetu mazuri ya Urio, Nyangeta, Ndikumana, Chacha, Bhoke, Masawe, Kabwe nk.

Je, hawa wageni waliotuletea hizo tamaduni zao na kuziona zetu za kishamba wana majina Kama ya asili yetu?

Wazazi vijana tunakwama wapi kuwapa majina asilia watoto tunaowazaa?

Tunahitaji nini walau hili la majina tujikomboe?
 
Majina mengi hasa ya Kikristu yanatokana na Dini ambayo ililetwa na hao wazungu kwahiyo wengi tukibatizwa kanisani tunapewa yale majina ya dini husika iliyokuja na mzungu. haya mangine ya akini mwakitenkimwakilipuka hayaapo kwenye biblia.
 
Malaika Mkuu Gabrieli (mjumbe wa Mungu); Malaika Mkuu Mikaeli (nani aliye kama Mungu?); Malaika Mkuu Raphael (Mungu ni kinga yangu)! Mengine ni majina ya malaika na sio ya kizungu tu Mkuu. Kwani hata Emmanuel si limetajwa - Mungu pamoja nasi?
 
Jina lina athari fulani kwa mhusika

Ikiwa jina linabeba maana nzuri na ya kupendeza,basi hakuna neno kutumika

Ila watu wengi sana,wanatumia majina,bila kujua maana na makusudio
Hili si jema

Hakuna ubaya kutumia majina ya asili,ikiwa ni mazuri kimaana,kadhalika majina ya kigeni
...hebu tuhoji hapa, wengi wetu tuna majina ya Peter, Anna, John, Hamad, Ashura, Hassan nk. Haya ni majina ya kigeni na tumeyatupilia mbali majina yetu mazuri ya Urio, Nyangeta, Ndikumana, Chacha, Bhoke, Masawe, Kabwe nk. Je, hawa wageni waliotuletea hizo tamaduni zao na kuziona zetu za kishamba wana majina Kama ya asili yetu?

Wazazi vijana tunakwama wapi kuwapa majina asilia watoto tunaowazaa?

Tunahitaji nini walau hili la majina tujikomboe?
 
Malaika Mkuu Gabrieli (mjumbe wa Mungu); Malaika Mkuu Mikaeli (nani aliye kama Mungu?); Malaika Mkuu Raphael (Mungu ni kinga yangu)! Mengine ni majina ya malaika na sio ya kizungu tu Mkuu. Kwani hata Emmanuel si limetajwa - Mungu pamoja nasi?
Na waliosema Yana maana ulizotaja ni hao hao wazungu!
 
Majina mengi hasa ya Kikristu yanatokana na Dini ambayo ililetwa na hao wazungu kwahiyo wengi tukibatizwa kanisani tunapewa yale majina ya dini husika iliyokuja na mzungu. haya mangine ya akini mwakitenkimwakilipuka hayaapo kwenye biblia.
Na ukikutana na Padre sijui mchungaji mwenye msimamo na unataka mwanao abatizwe jina la Mwakalukwa anakufungia mpk kuingia kanisani
 
Hebu tuhoji hapa, wengi wetu tuna majina ya Peter, Anna, John, Hamad, Ashura, Hassan nk. Haya ni majina ya kigeni na tumeyatupilia mbali majina yetu mazuri ya Urio, Nyangeta, Ndikumana, Chacha, Bhoke, Masawe, Kabwe nk.

Je, hawa wageni waliotuletea hizo tamaduni zao na kuziona zetu za kishamba wana majina Kama ya asili yetu?

Wazazi vijana tunakwama wapi kuwapa majina asilia watoto tunaowazaa?

Tunahitaji nini walau hili la majina tujikomboe?

Thubutu. Sisi ndo tunajiona wastaarabu kubeba majina yao huku tukiaminishwa eti majina ya mababu zetu hayana baraka ila majina ya wazungu walokufa miaka na mikaka ndo yenye baraka kwetu.

Mimi nimeamua watoto wangu wote wanapew majina ya kiafrika na siwapeleki kanisani hata iweje maana huko ndiko wanapooshwa akili.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom