Je, Kuna Mwandishi katekwa Dar?

Kiranja

JF-Expert Member
May 19, 2007
751
336
Kuna habari kwamba Mwandishi wa Habari, wa Alasiri mwanamke alitekwa na kutelekezwa Mbagala leo mchana muda huu ametoka polisi Oysterbay..... Habari zaidi baadaye
 
Kuna habari kwamba Mwandishi wa Habari, wa Alasiri mwanamke alitekwa na kutelekezwa Mbagala leo mchana muda huu ametoka polisi Oysterbay..... Habari zaidi baadaye

2163571305_814a7313b3.jpg
 
GT hiyo picha ya nani? Anayedaiwa kutekwa anaitwa Mwanaidi Sued. Hadi sasa haijulikani ni majambazi, wabakaji, wezi, watishaji au mafisadi wanaotaka kuzidisha woga kwa waandishi wa habari. LIWALO NA LIWE WOTE SI WEMA HATA KIDOGO... Hii nchi haiwezi kuwekwa katika mazingira haya ya TINDIKALI, KUTEKANA na kadhalika
 
Quote: GAME THEORY


GT vipi tena na hiyo picha!?

Hiyo picha inafanana na ya Mzee wetu, Adam Lusekelo!!! Unamchuria? Au ndiye aliyekusudiwa? Lakini yeye si mwanamke!!!!
 
Thank God, siioni hiyo picha maana mara nyingi hazihusiani na mada. Halisi kwani huyo dada anajulikana kwa namna yoyote kuhusika na mambo ya uandishi wa uchunguzi au inawezekana ikawa ni uhalifu tu?
 
eddy murphy huyo kwenye dreamgirls, GT bwana, sasa hapo unataka kutuambia nini..............?

mbagala mpaka osterbay police??? au na-miss kitu hapa!!!?
 
eddy murphy huyo kwenye dreamgirls, GT bwana, sasa hapo unataka kutuambia nini..............?

mbagala mpaka osterbay police??? au na-miss kitu hapa!!!?

Temeke hadi Kinondoni kudeka au nini ina maana hawaamini Polisi wa Temeke???? Ila pole sana kwa kutekwa hao hawakuwa na tindikali.
 
Journalist briefly kidnapped by thugs

2008-01-26 09:34:11
By Guardian Reporter


A journalist with the Guardian Limited Mwanaidi Swedi was yesterday kidnapped by unknown people and kept hostage for hours before the kidnappers released her.

Mwanaidi, who writes for a Kiswahili evening paper�Alasiri�was kidnapped just a few metres from the Guardian Ltd offices at Mikocheni as she was going to town for an assignment.

Speaking to this reporter Mwanaidi said a dark blue saloon car with tinted windows stopped nearby with three men and offered to give her a ride to town.

According to Mwanaidi, one of the three men seemed to look familiar to her making her believe that they knew her.

``The car then headed to town but when we reached at Bamaga one of the men suggested that they take Shekilango Road to avoid traffic jam,`` she said.

She said on the way, the two men who were sitting with her on the back seat strangled her.

``They asked me if I know a man called Thomas who lives at Wazo Hill. I told them I do not know the man,`` she said.

Mwanaidi said the kidnappers told her they had come from Arusha for a special assignment to teach a lesson to journalists who write about other people.
``They kept on strangling me and one of them told me to hand over all my belongings,`` she said.

She said she attempted to resist but the kidnapers threatened to kill her.

``They took my cellular phone, my wedding rings and the money I had in my handbag,`` she said.

Mwanaidi further said that she was thrown out of the car when they reached at Kinondoni cemetery before the car sped away.

Kinondoni Regional Police Commander Jamal Rwambow said they have not arrested anybody yet and that investigations were going on to net the suspects.

``We are still investigating on the incident. It is not good to ignore the incident but it is also wise to investigate,`` he said.

SOURCE: Guardian http://www.ippmedia.com/ipp/guardian/2008/01/26/107071.html
 
Mwandishi wa The Guardian atekwa, aporwa

2008-01-26 09:46:36
Na Mwandishi Wetu


Watu watatu wasiojulikana ``wamemteka`` kwa zaidi ya saa moja mwandishi wa habari wa kampuni ya The Guardian, na kisha kumpiga na kumpora fedha, simu na pete yake ya ndoa.

Tukio hilo lilitokea katika kituo cha ITV kilichopo Mwenge jijini Dar es Salaam jana, ikiwa ni siku chache baada ya Mhariri wa MwanaHalisi Bw. Saed Kubenea na Mshauri wa gazeti hilo, Bw. Ndimara Tegambwage kuvamiwa, kupigwa na kumwagiwa tindikali na watu wasiojulikana.

Akisimulia tukio hilo, mwandishi huyo (jina linahifadhiwa kwa sababu za kiusalama) alisema alipofika katika kituo hicho, kwa lengo la kwenda katikati ya jiji, lilitokea gari moja ambalo lilisimama jirani yake na waliokuwemo wakamwomba aingie katika gari hilo kwa lengo la kwenda mjini pia.

Alisema hakuwatilia shaka watu hao kwa vile gari hilo lilikuwa likitokea barabara ya ITV ziliko ofisi za The Guardian pia, kwa hiyo akahisi ni watu wanaomfahamu.

Alisema baada ya kuingia katika gari hilo lililokuwa na vioo vya giza, watu hao walivifunga vioo vyote na kuingia barabara ya Shekilango kwa madai ya kukwepa foleni na wakamhoji iwapo alikuwa mtangazaji au mwandishi wa habari.

``Nilipofika maeneo ya baa ya Hongera, gari hilo lilikata kushoto kuelekea jengo la ofisi za Tume ya Sayansi na Teknolojia na kabla ya kufika maeneo hayo, abiria mmoja aliyekuwa ameketi kiti cha mbele alihamia kiti cha nyuma na ghafla mwingine niliyekuwa nimekaa naye kiti cha nyuma alinikaba na kunifunika macho kwa kitambaa,`` alisema.

Alisema baada ya kitendo hicho, aliambiwa, ``mnajifanya kujua kuandika habari za maslahi ya watu na sisi tupo kazini, tulia tufanye kazi yetu.``

Alisema wakati huo walikuwa wamekwisha mnyanga`nya fedha, simu na pete ya ndoa, huku mwingine akiendelea kumhoji.

``Mkurugenzi wenu juzi tulimmwagia tindikali, na mwenyekiti wenu anawatetea kwamba muendelee kufanya kazi zetu, lakini muangalie mnachoandika muangalie pia na maisha yetu,`` alisema.

Hata hivyo, walisema mtu waliyekuwa wakimtafuta hakuwa yeye na walipewa picha ya mtu mwingine.

``Sasa tunataka utusaidie, tulia, unamfahamu Thomas wa Wazo Hill, mnamtumia sana huyo,`` walisema huku wakimpiga vibao na kumweleza kwamba wanaweza kumfanya kitu chochote kile, ikiwa ni kumbaka, kumuua na kumtupilia mbali.

Huku akiwa amefunikwa kitambaa usoni, waliendelea kumhoji iwapo kazi alianza lini na yeye akawaeleza kuwa alianza hivi karibuni.

``Kumbe ni mtoto mdogo, umeanza kazi juzi tu,`` alisema mmojawapo na kuongeza, "hilo siyo dili, tunayemtafuta bado, tungempata huyo leo, ingekuwa dili kweli,`` alisema mmoja wapo na kisha walikubaliana kumwacha huku wakimtisha asizungumzie tukio hilo kwa watu wala kuliripoti katika vyombo vya habari.

Hata hivyo, walimshusha karibu na makaburi ya Kinondoni, lakini alikwenda kuripoti taarifa hiyo kituo cha polisi cha Oysterbay ambako alipata OB/RB/1669/08.

SOURCE: Nipashe

Aluta continua!
Inabidi pia wawe makini na lifti.
 
kiranja

Kuna habari kwamba Mwandishi wa Habari, wa Alasiri mwanamke alitekwa na kutelekezwa Mbagala leo mchana muda huu ametoka polisi Oysterbay..... Habari zaidi baadaye

halafu soma hapa tena

...Mwanaidi further said that she was thrown out of the car when they reached at Kinondoni cemetery before the car sped away....

Mbona maelezo yanagongana hapo kuhusu eneo la tukio????

Ila dalili ya mavua ni mawingu hivyo ni budi vyombo vya usalama kuanza kuchukua hatua na tahadhari dhidi ya matukio haya maana mafisadi wameshapagawa na wanamkwaa kila aliye mbele yao. Lazima tuwe waangalifu sana sisi wanahabari....
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom