Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature currently requires accessing the site using the built-in Safari browser.
Kuna habari kwamba Mwandishi wa Habari, wa Alasiri mwanamke alitekwa na kutelekezwa Mbagala leo mchana muda huu ametoka polisi Oysterbay..... Habari zaidi baadaye
Quote: GAME THEORY
GT vipi tena na hiyo picha!?
mbagala mpaka osterbay police??? au na-miss kitu hapa!!!?
eddy murphy huyo kwenye dreamgirls, GT bwana, sasa hapo unataka kutuambia nini..............?
mbagala mpaka osterbay police??? au na-miss kitu hapa!!!?
Mwandishi wa The Guardian atekwa, aporwa
2008-01-26 09:46:36
Na Mwandishi Wetu
Watu watatu wasiojulikana ``wamemteka`` kwa zaidi ya saa moja mwandishi wa habari wa kampuni ya The Guardian, na kisha kumpiga na kumpora fedha, simu na pete yake ya ndoa.
Tukio hilo lilitokea katika kituo cha ITV kilichopo Mwenge jijini Dar es Salaam jana, ikiwa ni siku chache baada ya Mhariri wa MwanaHalisi Bw. Saed Kubenea na Mshauri wa gazeti hilo, Bw. Ndimara Tegambwage kuvamiwa, kupigwa na kumwagiwa tindikali na watu wasiojulikana.
Akisimulia tukio hilo, mwandishi huyo (jina linahifadhiwa kwa sababu za kiusalama) alisema alipofika katika kituo hicho, kwa lengo la kwenda katikati ya jiji, lilitokea gari moja ambalo lilisimama jirani yake na waliokuwemo wakamwomba aingie katika gari hilo kwa lengo la kwenda mjini pia.
Alisema hakuwatilia shaka watu hao kwa vile gari hilo lilikuwa likitokea barabara ya ITV ziliko ofisi za The Guardian pia, kwa hiyo akahisi ni watu wanaomfahamu.
Alisema baada ya kuingia katika gari hilo lililokuwa na vioo vya giza, watu hao walivifunga vioo vyote na kuingia barabara ya Shekilango kwa madai ya kukwepa foleni na wakamhoji iwapo alikuwa mtangazaji au mwandishi wa habari.
``Nilipofika maeneo ya baa ya Hongera, gari hilo lilikata kushoto kuelekea jengo la ofisi za Tume ya Sayansi na Teknolojia na kabla ya kufika maeneo hayo, abiria mmoja aliyekuwa ameketi kiti cha mbele alihamia kiti cha nyuma na ghafla mwingine niliyekuwa nimekaa naye kiti cha nyuma alinikaba na kunifunika macho kwa kitambaa,`` alisema.
Alisema baada ya kitendo hicho, aliambiwa, ``mnajifanya kujua kuandika habari za maslahi ya watu na sisi tupo kazini, tulia tufanye kazi yetu.``
Alisema wakati huo walikuwa wamekwisha mnyanga`nya fedha, simu na pete ya ndoa, huku mwingine akiendelea kumhoji.
``Mkurugenzi wenu juzi tulimmwagia tindikali, na mwenyekiti wenu anawatetea kwamba muendelee kufanya kazi zetu, lakini muangalie mnachoandika muangalie pia na maisha yetu,`` alisema.
Hata hivyo, walisema mtu waliyekuwa wakimtafuta hakuwa yeye na walipewa picha ya mtu mwingine.
``Sasa tunataka utusaidie, tulia, unamfahamu Thomas wa Wazo Hill, mnamtumia sana huyo,`` walisema huku wakimpiga vibao na kumweleza kwamba wanaweza kumfanya kitu chochote kile, ikiwa ni kumbaka, kumuua na kumtupilia mbali.
Huku akiwa amefunikwa kitambaa usoni, waliendelea kumhoji iwapo kazi alianza lini na yeye akawaeleza kuwa alianza hivi karibuni.
``Kumbe ni mtoto mdogo, umeanza kazi juzi tu,`` alisema mmojawapo na kuongeza, "hilo siyo dili, tunayemtafuta bado, tungempata huyo leo, ingekuwa dili kweli,`` alisema mmoja wapo na kisha walikubaliana kumwacha huku wakimtisha asizungumzie tukio hilo kwa watu wala kuliripoti katika vyombo vya habari.
Hata hivyo, walimshusha karibu na makaburi ya Kinondoni, lakini alikwenda kuripoti taarifa hiyo kituo cha polisi cha Oysterbay ambako alipata OB/RB/1669/08.
SOURCE: Nipashe
kiranja
Kuna habari kwamba Mwandishi wa Habari, wa Alasiri mwanamke alitekwa na kutelekezwa Mbagala leo mchana muda huu ametoka polisi Oysterbay..... Habari zaidi baadaye
...Mwanaidi further said that she was thrown out of the car when they reached at Kinondoni cemetery before the car sped away....