Je, kuna mwanaume asiyechepuka?

Ndivyo unavyoamini mkuu?

Wengi hamuelewi majukumu ya mwanaume hasa anapoamua kuwa Baba wa familia,nimekuwa na rafiki zangu ambao wanaendekeza huu umwamba ila kila wakati jasho lao hulitumia kwa maumivu makali sana mf:yupo mmoja siku hiyo anaogopa kupokea simu ananiambia niipokee mimi nidanganye amesahau simu kisa anayepiga ni ma.laya wake aliyemuahidi kumlipia kodi miezi 6 Tabata (yeye mwenyewe anaishi chumba na sebule Tegeta na familia) acha mizinga ya saloon etc na maendeleo hana.

Ukitoa kuogopa dhambi ya uzinzi kutulia na mwanamke mmoja kuna manufaa sana (wachache wamefanikiwa kuyajua),kwanza unakuwa huru mimi simu zangu muda wowote mahali popote mke wangu anashika passwords zote anazijua wakati mwengine nikiwa mbali hutoa yeye maelezo,kufanya sex iliyo safi na kwa uhuru,salama na ya furaha,wakati fulani bado mgeni kwenye ndoa mke wangu alipojifungua first born wetu nikaiga kutoka nje nilikutana na ex ujinga ujinga nikajaa,hofu hofu nimevaa mipira nikiwaza gharama nilizotumia mpaka kukamilisha hiyo mission nikaona ni ujinga,ukishakuwa na watoto wawili+ (though ninao wawili bado nitaongeza Mungu akipenda najiona niko aged 50) najua ndoto zao nimezibeba mimi kutumia pesa 100K pasi na manufaa siioni faida yake zaidi nitawaza niifanyie nini kwa kesho yao au bora waitumie wao kuvaa kula ada etc.

Kuwa muaminifu kwenye ndoa hukupa amani ya maisha,muda wote nyumba inatamalaki furaha mke anacheka watoto wanafurahi hakuna hisia mbaya dhidi yako watoto wanaijua ratiba ya Baba yao kurudi nyumbani ni furaha sana unaingia home watoto wanakufurahia na wanakupa taarifa siku yao ilivyoisha najua hata siku sipo wataukumbuka uwepo wangu (ukiwa mzinzi haya yote utayafanya muda gani wakati ukirudi wamelala?)
 
Ni rahisi ukiwa huna hela. Ila kama una hela ni ngumu mno maana hawa watoto wa kileo ukiwapa kizawadi tu tayari
 
Waziri kasema hakuna cha fumanizi Tena hivyo Kama huna cheti na unaishi na mtoto wa mtu miaka nenda Rudi nitamtafuna na huna la kunifanya maana Sasa tumehalalishiwa
 
hongera sana Mkuu
Asante mkuu baadhi ya mambo unafanya kwa ajili ya watoto

Ku cheat gharama kwanza aisee hata kama pesa zipo i can't do that stupidity

Sema inategemea na level yenu ya mapenzi aisee

Mkipendana kama kaka na dada kama mimi au Mkipendana kama Marafiki believe me kuna muda hamu ya kufanya mapenzi inaisha ila knachobaki ni urafki wenu na kupendana kwenu mpk pale hamu imerudi
 
Wapo wanaume wasiochepuka ila wengi ni wenye umri kuanzia miaka 40 na kupanda hao ndo wanatosha kwenye hii mada yako, ambapo ni kwamba chini ya umri huo anakuwa amefanya uwindaji wa aina zote halali na haramu akiamua kutulia na mwanamke mmoja wengi wao hutulia kabisa, ila ndo sio wote wengine huendeleza kujitutumua mpaka uzeeni na wengi wao huzeeka kwa aibu sana.

Hakuna tuzo kwenye kubadili wanawake, watajisifia ndo uanaume lakini waliofanya hizi mambo ukiongea nao katika umri wao wa uzee wanajutia sana muda waliopoteza.
Vyema mkuu tupo hatuchepuki
 
Back
Top Bottom