Je, Kuna mtumishi wa umma yeyote aliyekamatwa na vyeti feki katika hakiki na kufukuzwa kazi?

Ndikwega

R I P
Feb 1, 2012
5,979
5,527
Salaam Wadau!

Naomba kujuzwa kwa anayejua hili. Je, kuna Mtumishi wa Umma yeyote aliyekamatwa na vyeti bandia/bandia katka Uhakiki wa Watumishi wa Uliyofanywa halafu akafukuzwa kazi ama Kusimamishwa?

Maana kuna mdau kanipenyezea kuwa eti watu walidakwa na vyeti Bandia lakini aliyefukuzwa, zaidi wamepangwa kwenye nafasi inayoendana na Elimu yake. Kama alikuwa ameajiliwa kwa Ngazi ya Masters lakini Sitahiki ya elimu yake ni Kidato cha nne, karudiswa kwenye nafasi ya elimu ya mtu wa Kidato cha Nne, nadharika.

Kama ni kweli, je, kulikuwa na Umuhimu gani wa Kutumia nguvu kubwa kwa jambo ambalo halina Tija saana kihivi?

Karibuni wadau, tupashane katka hili.
 
Mi nina list ya Jamaa flani ambao wanafanya kazi kwenye kivuko cha Kigongo Ferry Mwanza..cha serikali.... hata cheti cha la 7 hana na hajafukuzwa kazi......anasifika sana kwa kutumia mizizi..... Jina maarufu wanamwita KATAI au MVAA MIWANI. Balaa sana jamani kama Ubashite utaendelea kwa style hii.
 
Kwa ujumla hi serikali n ya kisanii sana inakwepa kusema ukweli kuwa hapo wanasubiria bajeti mpya ili wawalipe watumish stahiki zao ila ili kufika huko lazima watumie njia hyo ingawa wale ambao walifoji vyeti wameingia mitini lkn bado utawala hauna la kisingizia tena ndo maana huanzisha mada kila uchao,wamewakata wanufaika wa bodI ya mikopo lkn bado bajeti haisomeki
 
Mi nina list ya Jamaa flani ambao wanafanya kazi kwenye kivuko cha Kigongo Ferry Mwanza..cha serikali.... hata cheti cha la 7 hana na hajafukuzwa kazi......anasifika sana kwa kutumia mizizi..... Jina maarufu wanamwita KATAI au MVAA MIWANI. Balaa sana jamani kama Ubashite utaendelea kwa style hii.
Wengi wanasema hakuna aliyefukuzwa na nasikia waliyokuwa wamekimbia wenyewe wamefuatwa na kurejeshwa kazini.
 
Kama serikali haikuwa na nia ya dhati katika zoezi hili kwa nini wakalianzisha na kuliendesha nchi nzima tena kwa gharama kubwa na usumbufu mwingi. Kama serikali haijamfukuza yeyote ni baada ya kubaini kuwa hata wahakiki vyeti wenyewe hawakuwa na vyeti au walikuwa navyeti vya kughushi.
 
Rais alisema waachie ngazi wenyewe, na wengi walifanya hivyo! Nashangaa huyo mmoja wa Dar amegoma kabisa!
 
Serikali kama Serikali je, kuna mtu imemfukuza zaidi ya Kujikimbiza wenyewe?
Hakuna_! wala haijawahi kutangazwa kitu kama hicho. Ni kwamba upelelezi haujakamilika! Ila kuna mamia walioingia mitini wenyewe kwa kuogopa mkwala mzito!
Daudi Bashite yeye alikomaa na bado anakomaa japo mchozi unamtoka na kuna dalili naye anaelekea kuingia mitini!
 
Inaonesha watu hawakufukuzwa walikimbia wenyewe, hata huyu wa sasa atakuwa ameamua kukimbia mwenyewe
Ha ha ha naona yuko mahali anaangalia upepo!
Tatizo inaelekea kuna wakubwa pia ni waathirika wa hii kitu! Sasa kigugumizi naona hakiepukiki hasa huko maj*sh*ni!
 
Kama serikali haikuwa na nia ya dhati katika zoezi hili kwa nini wakalianzisha na kuliendesha nchi nzima tena kwa gharama kubwa na usumbufu mwingi. Kama serikali haijamfukuza yeyote ni baada ya kubaini kuwa hata wahakiki vyeti wenyewe hawakuwa na vyeti au walikuwa navyeti vya kughushi.
Ndiyo utajua Serikali hii Usanii mtupu aisee!
 
Namfahamu dada mmoja kazini kwetu,nafanya naye kazi idara moja.ametoroka kusiko julikana.ni mwezi wa tatu sasa,hata kwenye simu hapatikani.
 
Sidhani, kwani hata palipo na ushahidi wa wazi kama Bashite unaoa kinachoendelea. Hiyo ndio picha halisi ya zoezi zima!
 
Back
Top Bottom