Je, kuna madhara yatokanayo na kufanya tendo la ndoa kwa mama mjamzito au baada ya kujifungua ?

mjumbewenu

Member
May 5, 2016
10
3
Mama anapokuwa mjamzito je, ni miezi ipi huruhusiwi kufanya naye tendo la ndoa ukiacha mwezi wa nane na wa tisa; baada ya kupata ujauzito.
Pia baada ya kujifungua kufanya tendo la ndoa haina athari kiafya kwa mtoto anayenyonya. Naomba mchango wenu kwa wale wenye uzoefu na haya mambo.
 
Mjumbe Wetu, nenda clinic na mkeo na haya masuali uyaulize huko. Kutegemeana na afya ya mama, tendo la ndoa linaruhusiwa kila wakati mpaka uchungu wa kuzaa utakapoanza. Infwakti unahimizwa has a siku za mwisho katika mkakati wa kuandaa kujifungua.

Hongera na kila la kheir
 
Baada ya kupata mimba unaruhusiwa kufanya tendo la ndoa hadi pale utakapoona inatosha,kipindi cha kujifungua (labour) huwezi kufanya mapenzi, baada ya kujifungua unatakiwa kukaa siku 42 yaani wiki sita, kipindi hiki kinaitwa (puerperium), na kuna maji maji ambayo yanaweza kujitokeza kwa mama yanaitwa lochi. Baada ya wiki sita unaweza kukutana na mkeo kama atakuwa tayari na hana tatizo lolote, muhimu kutumia uzazi wa mpango ili kuepuka mimba isiyotarajiwa
 
usimuhakikishie kwamba ni baada ya wiki 6, ni vyema umwambie baada ya wiki 6 kukiwa hamna tatizo, kuna wengine wanakua hawajapona vizuri kama alichanika akashonwa,
kuna wengine wale wa operations wanakua na complications pia.
 
Back
Top Bottom