Je Kuna madhara ya Kulazimisha kuwa Kiongozi katika Jamii? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je Kuna madhara ya Kulazimisha kuwa Kiongozi katika Jamii?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Felister, Feb 26, 2011.

 1. F

  Felister JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2011
  Joined: Aug 5, 2008
  Messages: 377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kabla ya kusema haya acha niweke bayana haya yafuatayo ni muhimu kuzingatiwa:

  • Mimi ni mkristo wa kilokole
  • Ni msomi wa kati
  • Napenda upinzani zaidi kuliko chama tawala.
  Hizo tabia hapo juu zaweza sababisha nilalie upande mmoja ambao ndizo zinazotawala fikra zangu katika maisha kwa hiyo kila atakaye soma au kujadili azingatie hayo katika kufikia majumuisho.

  Kumekuwa na maneno mengi na dhana inayotawala based on JF kama main reference; kuwa kiongozi wanchi yetu hakutumia mfumo na njia zilizozoelewa na kukubalika na wengi ikiwamo chama chake na hata baadaye kwa mara ya pili kutumia mfumo ambao japo kisheria siyo batili lakini kimtazamo na mazoea pamoja na matakwa ya wengi, usiyo faa (CDM na most of JF members)? Je madhara yake ni matokeo ya matatizo tunayoendelea kuyaona ya watu kunong'ona mabaya na hata kutamani huu utawala usifikie malengo iliyojiwekea (JF)?

  Ukisoma biblia hali kama hii ilishawahi kutokea wakati wa enzi ya Yakobo (Israel) kwa wana wake kumi na mbili ambao wanaunda taifa la Israel. Alipokaribia kufa aliwaita wanawe awabariki na katika kufanya hivyo kutokana na kosa la mtoto wake wakwanza aliyekuwa na haki ya kupata double portion alikosa Baraka ya baba na kupata laana kwani alitembea na mke wa baba yake. Hivyo baba akambariki Yuda ndiyo uzao wake utoe mfalme wa Israel badala ya Reuben. Lakini Kutokana na zambi ya uzinzi Mungu aliamua kuwa kiongozi wahilo taifa mpaka atakapo deal na hiyo dhambi bahati mbaya wana wa Israel wakalilia kuwa na mfalme wao kama mataifa mengine wakalazimisha Nabii Samweli awape Kiongozi na hivyo akatokea Sauli kutoka katika kabila la Benjamini tofauti na Baraka za baba yao Yakobo(Israel) mpaka hapo Daudi akatawazwa kuwa mfalme wa Israel na hata leo ufalme wake unadumu milele (Imani ya wakristo) kwani Yesu ni zao la ukoo wa Daudi ambaye ni Simba wa kabila la Yuda na hapo ndipo napoanza ku build case yangu (Genesis: 49).

  Tuliona mawazo au Baraka za baba wa Taifa hapo mwaka 1995 katika kupata kiongozi alitoa sifa za kiongozi na alikataa kutaja jina. Je kiongozi aliyeingia madarakani alikataa kufuata mfumo unaofaa/kubalika kwa sababu gani? Je aliona chama chake kilikuwa kina enda kinyume na Baraka za baba au kinyume chake ndo ukweli? Na je huu uongozi mambo yake hayaendi kwa sababu watu wamevunja wosia wa baba au ni vipi? Je kuna mahusiano yeyote kati ya hali tuliyonayo na hayo yaliyotokea enzi za baba Yakobo? Kwa vyovyote vile kila mwenye pumzi iliyohai anajua ukweli wa hili jambo na kila mhusika aweza kana mbele ya watu lakini dhamira yake inanguvu ya kuhukumu sawasawa na ukweli. Ni wakati basi wakutafakari na kuchukua hatua kukubali ukweli na kuwa mashujaa ama kuukana na kuaibika milele. The same story is found in Nigerians film called "The Anointed Quine" Chamsingi ni kuwa Mungu anachukia dhambi lakini anapenda mwenye dhambi na njia ya kupata neema na rehema kwa yeyote ni kwa kutubu na kusimama katika kweli. Kila anayetubu anaepuka aibu na adhabu ya milele.
   
 2. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Mkuu unajua tofauti ya kiongozi na mtawala? from there tunaweza kujadili kitu...
   
 3. F

  Felister JF-Expert Member

  #3
  Feb 26, 2011
  Joined: Aug 5, 2008
  Messages: 377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Context ni means as both have the denominator of position.

  To make you get the clear link; Kabila hapa lina represent traits/attributes ambazo mfumo unamtaka ndo awe kiongozi tuki refer hotuba ya baba wa Taifa ambaye ndiye aliyeweka base ya system ambayo ndo ina operate up to now if I am correct.
   
Loading...