Je! Kuna Kuna haja Vyama vya upinzani kuanzisha vituo vyao vya TV? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je! Kuna Kuna haja Vyama vya upinzani kuanzisha vituo vyao vya TV?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by analysti, Sep 2, 2010.

 1. analysti

  analysti JF-Expert Member

  #1
  Sep 2, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 704
  Likes Received: 354
  Trophy Points: 80
  Ndugu wana JF, Tumeshuhudia na tunaendelea kushuhudia jinsi kituo cha TV cha TBC kinavyokandamiza upinzani, hasa chama kilichojidhihirisha kuwa ni tishio kwa chama tawala mwaka huu,kwa kuwalimit ni mambo gani wazungumzie kwenye kampeni, na hata kuonyesha habari za kampeni zilizochakachuliwa. Mimi nafikiri ni wakati muafaka, kwa vyama hivi kuanzisha vituo vya TV ili kuhakikisha ujumbe wa ukombozi ambao chama tawala usingependa wananchi uwafikie, unawafikia wananchi kama inavyokusudiwa.
   
 2. M

  Msharika JF-Expert Member

  #2
  Sep 2, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kweli kabisa, tunahitaji vituo mbadala kwa vyama vya upinzani
   
 3. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #3
  Sep 2, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,065
  Likes Received: 3,992
  Trophy Points: 280
  ccm lazma wale deal na tcra wanyang`anywe leseni na wafunge hiyo TV au watahakikisha hamna kampuni binafsi inapeleka matangazo ishindwe kujiendesha
   
 4. D

  Dopas JF-Expert Member

  #4
  Sep 3, 2010
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kimsingi hakuna sababu ya kuanzisha kingine kwa sababu tayari kuna vyombo kama hivyo vya umma ambavyo vimelipiwa kodi na wananchi wote wakiwepo wapinzani. Chombo cha mojawapo cha umma ni TBC1, TBC taifa, TBC fm.

  Iweje leo kinatumika kwa manufaa ya mafisadi, ilhali kodi ya kuiendesha ni ya mwananchi fukara? Nadhani wapinzani cha msingi ni kudai haki yetu ya kutumia chombo hicho kwa manufaa ya wote.

  Ikibidi kuwafukuza wanafiki wote kina Marin Hasan kwenye majukumu. Najua wapo wengi wa aina hiyo TBC. Ila naamini hatawakosekana wenye uwezo wa kutumia taaluma yao ya habari vema. Nadhani hii ndiyo muhimu.

  Kuanzisha kingine, tutaanzisha mangapi? Wakiingia huko tena mafisadi tufanyeje?
  Muhimu ni kupigania haki mpaka kieleweke.
   
 5. TingTing

  TingTing Member

  #5
  Sep 5, 2010
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 93
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Dhamira yao itawashitaki wahusika wote iwe ni walio uongozini au katika utangazaji. Siku hiyo ikifika ndio utawaona wanavyojipendekeza sasa kwa dhati. Inabidi watu tuingie field tuanze kufanya grassroots campaign ado ado tu kwa ajili ya 2015. Watakandamiza TV na radio lakini mwisho wa siku kama grassroot campaign ilikuwa superb then hata wafanyeje matokeo yatawaumbua. Inabidi kuanzisha transparet balot boxes ili kura ikipigwa na kuhesabiwa hapo hapo na majibu hapo hapo. Iwe ya uraisi au ubunge au udiwani. Hii itasaidia kupunguza uwizi wa kura kwa kiasi fulani. Watanganyika wameanza kuamka na ndio neema inaonekana sasa kuanzia Busanda na Biharamulo walioamua kuwafuata wa wapiganaji wa ukweli wa demokrasia walio Tarime. Uchaguzi huu sijui watapeleka askari zaidi ya elfu 1000 Tarime, na busanda na biharamulo sijui watapeleka wangapi maana watu ni wamechoka si kidogo. Elimu, Afya, Miundombinu taaabu kweli kweli. Huduma zero watu wanaleana na kulindana kila kukicha. SHIDA NO MORE. Ongea sasa kwa kura yako au ukae kimya na usilalamike hapo baadaye. Chagua unachoona kinafaa au bora kwako wewe au nisikusikie unalalama hapo baadaye. Maamuzi unayo wewe raia. Sote tukumbuke ya kuwa TUKIAMUA TUNAWEZA. TUKITAKA KITAFANYIKA.
   
 6. Negotiator

  Negotiator JF-Expert Member

  #6
  Sep 5, 2010
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  ipo haja ya kuandaa mjadala wa kitaifa juu ya haki kwa raia kutoka kwene vyombo vya umma. Ni hapa pia tunaona haja ya katiba mpya kupunguza madaraka ya rais katika uteuzi wa wakurugenz wa mashirika ya umma.
   
Loading...