Je, kuna kiongozi yoyote wa Upinzani amezungumzia habari za kesi ya Ugaidi ya Mbowe kwenye kongamano la maalim Seif?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,616
141,447
Nauliza tu kwa sababu Zitto Kabwe amekuwa akihudhuria hii kesi pale mahakama ya mafisadi na kila wakati amekuwa akidai Mbowe aachiliwe kwa sababu hii kesi ni ya kubumba.

Maalim Seif ni mhanga wa kuwekwa gerezani mara kadhaa kutokana na harakati zake za kisiasa hivyo niliamini katika kongamano hilo ni sehemu sahihi ya kuzungumzia kwa kifupi kadhia anayopitia rafiki wa maalim Seif aliyeko gerezani Freeman Mbowe.

Mungu wa mbinguni awabariki sana!
 
Gaidi asubiri adhabu yake aliyataka mwenyewe, wenzake aliwadhulumu nafasi za wabunge walizokubaliana wakati wanaunda ukawa.Acha apambane na hali yake.Ubinafsi nouma
 
Mama anajua fika Ila alitaka awaridhishe wafuasi wa mwendazake na Kisha aibu na adha awabebeshe
 
Mbowe alipokaribishwa na JPM jukwaani kuongea kwny sherehe za Uhuru mwaka 2019 kule Mwanza aliongea lolote kuhusu kupotea kwa Ben saanane, Masheikh wa Uamsho au risasi alizopigwa Tundulissu?
 
Mbowe alipokaribishwa na JPM jukwaani kuongea kwny sherehe za Uhuru mwaka 2019 kule Mwanza aliongea lolote kuhusu kupotea kwa Ben saanane, Masheikh wa Uamsho au risasi alizopigwa Tundulissu?
Kikao cha JPM ni tofauti na kikao cha Jussa!
 
Hakuna anayetaka kumuuzi huyo bibi. Kwanz akisikia neno katiba mpya , ndio anazidi kuchukia.
 
Back
Top Bottom