Je, kuna hatari gani watumishi wa Umma kukimbilia Ubunge?

MakinikiA

JF-Expert Member
Jun 7, 2017
5,011
6,542
Je, kuna hatari gani watumishi wa umma kukimbilia ubunge?

Kwanza sheria inakataza watumishi wa umma kujiunga na vyama vya siasa. Lakini walio wengi wameingia kwenye mtego wa kuamini kuwa hata wasipopenya kwenye kupitishwa kugombea basi wanajua kwamba kuna nafasi nono za kuteuliwa watakuja kuzipata, kwahiyo wanauza wasifu wao kwenye mamlaka za uteuzi
"Utitiri wa watia nia wengi kutoka utumishi wa umma si ishara nzuri hata kama watu wengi wanachukulia kama hali ya kawaida na haki za watia nia kulindwa kikatiba.

Ni tishio kwenye amani ya nchi kuliko matisho mengine. Utumishi wa Umma umedharauliwa na hivyo watu hawana uadilifu kufanya kazi za taaluma. Wanatamani walau wateuliwe na kwa hilo wako tayari kufuata masharti yoyote watakayopewa ili waweze kuteuliwa maana wanafanya mbinu za kuvaa sare za CCM hata kama ndani wana mapenzi na vyama vingine tofauti ili waonekane na wateuzi hao hapo baadaye"

"Kutia nia na kuchukua fomu wala si ajenda yao, wengi wao wanataka kuonekana na hilo wameamua kutumia kidogo walichonacho ama ni sawa na kuvaa jezi ya Simba nje huku ndani wakiwa wamevaa jezi ya Yanga kwa kuhofia tu kuwa Yanga haiwezi kuchukua kombe, hivyo wanajifanya nao ni mashabiki wa Simba ili waishi kwa amani mitaani huku wakifaidi keki ya wana Simba kutokana na kelele na ubabe. Watu wa aina hiyo ni hatari kwa amani ya nchi siku ikitokea mtu wa kuwashawishi kupindua sahani, wakipata hamasa kidogo hao wanaweza kuwa mstari wa mbele kuchochea maasi."

Mtumishi wa umma akitaka kujiunga na chama cha siasa anatakiwa kufuata taratibu. Kiutaratibu anatakiwa kujiuzulu nafasi yake ya utumishi kwanza ndipo aingie chama cha siasa au anatakiwa kuomba ruhusa ya kuwa nje ya ajira yake kwa sababu zenye zinazoeleweka"

Suala la maslahi yatokanayo na ubunge linavutia watu wengi, hivyo siasa imekuwa sehemu inayolipa zaidi. Takwimu zinaonesha kuwa mbunge analipwa mshahara wa shilingi milioni 3.8 kwa mwezi, posho ya mwezi shilingi milioni 8, posho ya kikao kimoja ni shilingi 240,000 kwa siku, posho ya kujikimu shilingi 120,000 kwa siku. Baada ya miaka mitano ya ubunge wake anapokea pensheni ya shilingi milioni 240 (ipunguzwe hii)
 
Chadema wanaweza kumpa mtu aliyekatwa ccm nafasi ya kugombea Urais wa nchi Wakati CCM haiwezi kumpa hata ubunge mtu aliyetoka upinzani.

Unapata picha gani hapo?
 
Back
Top Bottom