Je, Kuna haja ya Tundu Lissu na wapinzani kwa ujumla wao kumjibu IGP Sirro?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
79,270
2,000
Nimemsikia Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Simon Sirro alipokuwa anaongea na waandishi wa habari , ameongea mengi na wala hakuna haja ya kuyarudia tena hapa, lakini nitagusia machache hasa kwenye Wapinzani kutishiwa maisha , kwa maana ya kutishiwa kuuawa.

IGP anakanusha na kupinga wanasiasa kutishiwa maisha na anabeza kitendo hicho as if wapinzani hao wametunga , na amefikia hitimisho kwamba hakuna aliyetishwa na kwamba jambo hilo limezushwa ili kuwezesha wapinzani hao kuishi nje ya nchi kama walivyopanga ili kuichafua Serikali.

Je, umefika wakati wa wapinzani nao kujibu kikamilifu kauli ya IGP ili kubalance Story au wakae kimya na kuacha kauli ya Sirro iwe ndio ya Mwisho?
 

Tripo9

JF-Expert Member
Sep 9, 2009
3,740
2,000
Weka mzigo woote tuusikilize sisi wenyewe, sababu mi sijaona hiyo vidio.
 

Godfrey-K

JF-Expert Member
Jan 5, 2016
1,857
2,000
Lissu alilamika kutishiwa maisha miaka mitatu iliyopita na hakupewa ulinzi hatimaye alipigwa risasi, je IGP anataka yatokee tens yaliyompata Tundu Antipas Lissu? Huyu ni wa kumsamehe tu, kwani anayemlipa mpiga zumari ndiye anayechagua wimbo.
 

Kuyata

Member
Nov 3, 2020
95
150
Kichekesho kingine kwenye hiyi press yake ansema yule askari aliyesema mbowe hashind, eti bado wanafanya uchinguzi, sijui ni uchunguzi wa wa kumpandisha cheo? yaani hadi nilijisikia kutapika. Jeshi let limeishiwa heshima, wamebaki kutumia ubabe tu. ila Mungu anawaona
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom