Je, kuna haja ya Tanzania kuwa na kiwanda cha majembe ya mkono?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
36,003
40,671
Je , kuna umuhimu wa kuanzishwa kiwanda cha majembe ya mkono Tanzania au ni vyema tu tukaendelea kutumia fedha adimu za kigeni kuagiza majembe toka China?
hand hoe.jpg
 
Mbona tayari tuna chuma chetu cha Liganga na Mchuchuma!

Badala ya kuagiza kutoka China, tungeanzisha tu viwanda vyetu vya ndani kwa ajili ya kuzalisha majembe ya kutumia bustanini, kusafishia mazingira ya nyumbani, nk na siyo kwa ajili ya "kilimo cha jembe la mkono" ambacho kiukweli huchosha na kuwazeesha watanzania walio wengi.
 
Yaani karne ya 21 tunafikiria kutengeneza kiwanda cha majembe ya mkono?
Kwa nini tusifikirie kutengeneza matrekta? Au basi hata plau ya kuvutwa na ng'ombe?
Sasa kama bado mahitaji ya jembe la mkono ni makubwa tufanyeje? Na hatuna kiwanda hata kimoja cha majembe hadi leo hii
 
Sasa kama bado mahitaji ya jembe la mkono ni makubwa tufanyeje? Na hatuna kiwanda hata kimoja cha majembe hadi leo hii
Ukitaka kujua tusivo makini kwa vipambele kama taifa, swala hilo ni mfano hai. Jembe la mkono ni muhimu katika familia yo yote. Kama kweli hakuna kiwanda cha jembe na panga, inasikitisha.
 
ZZK: Kutoka uzalishaji zana za kilimo hadi magofu ya vyuma chakavu


zzk2.jpg Pichani ni mitambo ya zamani ya kutengenezea zana za kilimo iliyorithiwa na mwekezaji kutoka ZZK.

• Wawekezaji watumia hadaa kuonyesha kuna uzalishaji unaendelea
• Yumo kigogo wa CCM, wadai wanajiandaa kutengeneza mabati

UWEKEZAJI katika kilichokuwa Kiwanda cha Zana za Kilimo (ZZK) jijini Mbeya bado ni kitendawili, hakuna kinachofanyika zaidi ya hadaa.


Kiwanda hicho cha zana za kilimo kiliuzwa kwa Kampuni ya CMG inayomilikiwa na mmoja wa makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Christopher Mwita Gachuma, ambapo tangu kiuzwe, takribani miaka 20 iliyopita, hakijawahi kuzalisha hata fyekeo.

Mkurugenzi wa Kampuni ya CMG, Niranjan Band, anadai kwamba wangeanza uzalishaji wa vifaa mbalimbali Januari 15, mwaka huu. Hata hivyo, pamoja na kauli hiyo ya Band, hali halisi haionyeshi kuwapo kwa maandalizi yoyote.

Baadhi ya wakazi wa Jiji la Mbeya waliozungumzia kuhusu kiwanda hicho na mpango wa kampuni hiyo, tayari wamekwishaonyesha shaka yao, wakisema hatua ya kampuni hiyo ni kiini macho kwani imekuja baada ya msimamo mpya wa Serikali ya Awamu ya Tano kuhusu viwanda vilivyobinafsishwa na ambavyo havijaendelezwa kama ilivyokubaliwa katika mauziano na serikali.

“Hakuna, anataka kukwepa tu, anajua watamnyang’anya kiwanda sasa anajidai kachangamka,” anasema mmoja wa wataalamu wa masuala ya kilimo ambaye aliomba kutotajwa jina gazetini.

Wakati wa kampeni, Rais John Magufuli aliweka wazi msimamo wa serikali atakayoiongoza kwamba itavirudisha viwanda na mashamba yaliyobinafsishwa na kutelekezwa.

Tayari timu ya wataalamu kutoka Tume ya Mipango ilitembelea Mkoa wa Mbeya hivi karibuni kukagua maeneo mbalimbali ya uwekezaji, ikiwamo baadhi ya viwanda vilivyobinafsishwa.

Timu hiyo ilikuwa katika utaratibu wake wa kawaida wa kazi kufuatilia mipango ya maendeleo na pia sehemu ya ilani ya uchaguzi ya CCM. Mpango wa miaka mitano 2016/2021 ni kuendeleza sekta ya viwanda, lengo likiwa ni kuifufua sekta hiyo ili iweze kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa.

Kwa mujibu wa mtaalamu kutoka Tume ya Mipango, Yohana Mpande, itakuwa ni ndoto kujikwamua kwenye umasikini bila viwanda.

Mpande anabainisha kuwa uwekezaji kwenye viwanda utaliwezesha taifa kuuza nje na kuondokana na hali ya sasa ambapo taifa linauza zaidi malighafi nje na kuwa wachuuzi wa bidhaa za viwandani kutoka nchi za nje.



Kiini macho cha uzalishaji:

zzk.jpg Baadhi ya zana za kilimo zilizowekwa kwenye jengo la maonyesho la kiwanda hilo, zikiwemo power tiller(pichani), ambazo hata hivyo hazitengezwi na kiwanda hicho.

Katika jengo la mbele la kiwanda hicho yamewekwa matrekta madogo (power tiller) yasiyozidi kumi, mashine mbili za nafaka na mbili za kufyatua tofali, zana ambazo huonyeshwa wageni wanaotembelea kiwanda hicho.

Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, matrekta hayo madogo yameagizwa kutoka China, na zile mashine za nafaka pamoja na kufyatulia matofali ndizo zilizotengezwa kiwandani hapo.

Band anadai kuwa uwezo wao kwa sasa ni kutengeneza mashine sita au saba za kufyatulia matofali, huku zile za nafaka akisema hutengenezwa baada ya kupata maagizo maalumu kutoka kwa wateja.

Uzalishaji mashine hizo kiwandani hapo, kama ilivyoelezwa na Mkurugenzi huyo, ulianza Desemba, mwaka jana na kwamba kufikia Januari 15, mwaka huu ndipo kiwanda kilipaswa kuanza uzalishaji mkubwa kwa vifaa mbalimbali, yakiwamo mabati ya kuezekea nyumba.

Vifaa vingine vinavyodaiwa na uongozi wa kiwanda hicho kuwa katika mipango yao ya uzalishaji ni pamoja na fyekeo, matoroli (wheelbarrows) na magodoro.

Hata hivyo ziara ya ndani ya kiwanda hicho haitoi picha ya kuwapo uzalishaji wowote. Waandishi wa habari za Utalii na Uwekezaji walitembelea kiwanda hicho mapema mwezi huu, lakini pamoja na kuzungushwa kiwandani hapo, hawakuweza kushuhudia uzalishaji wowote.

Hali halisi ya kiwanda:


Miongoni mwa maeneo yenye kusikitisha unapotembelea kiwanda hicho ni pamoja na jengo la lililotumika kutengeza zana mbalimbali za kilimo wakati wa uhai wa kiwanda hicho. Leo hii, jengo hilo limegeuka kuwa mithili ya ghala la kuhifadhia vyuma chakavu.

Taarifa za ndani ya kiwanda hicho zinafichua kuwa, pamoja na mitambo hiyo mfu, baadhi ya majengo ya kiwanda hicho yamekuwa yakitumika kama maghala ya kuhifadhi bia aina ya Serengeti.

Mitambo haionyeshi kuwa na uzima wowote, imechakaa huku vyuma vya ukubwa mbalimbali vikionekana kutawanyika kwenye sakafu ya jengo hilo la mitambo lililotumika kutengeneza zana za kilimo.

Mitambo pekee yenye kuonekana kuwa katika hali nzuri ni ile ya kutengezea mabati ya kuezekea nyumba, ambapo malighafi yake wanatarajia kuagiza kutoka China.

Mipango ya kiwanda hicho, kama ilivyoelezwa na mkurugenzi wake haionyeshi kuwepo dhamira ya kweli ya kuzalisha zana za kilimo ambayo ndio shughuli ya msingi ya kuanzishwa kwa kiwanda hicho.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, aliliambia Raia Mwema kuwa, wanafuatilia kwa karibu uwekezaji katika viwanda mbalimbali mkoani kwake, kikiwamo kilichokuwa Kiwanda cha Zana za Kilimo Mbeya.
Katika harakati zake za kuhakikisha viwanda hivyo vinafufuliwa, wawekezaji katika viwanda vya ZZK, nguo, nyama na sabuni walialikwa katika jumuiko la wawekezaji la Mkoa wa Mbeya lililofanyika mwaka 2014, mkoani hapa.
Miongoni mwa ahadi za mwekezaji katika Kiwanda cha Zana za Kilimo, ilikuwa kuendeleza mpango wa asili wa kiwanda hicho, ambao ni kutengeneza zana za kilimo kwa kuingiza teknolojia ya kisasa.

Kwa mujibu wa ahadi yake hiyo kwa Serikali ya Mkoa wa Mbeya, Gachuma alielezea kufanya mawasiliano na wawekezaji ili kubaini ni kwa jinsi gani wanaweza kuendeleza mpago wa asili wa kiwanda hicho wa kutengeza zana za kilimo lakini kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

Gachuma alitoa ahadi hiyo wakati wa jumuiko la wawekezaji la mkoa huo, lililofanyika mwaka 2014 jijini Mbeya, likiwajumuisha wawekezaji kutoka ndani na nje ya mkoa huo.

Pamoja na ahadi hiyo, kulikuwa na ahadi pia ya kufufua mitambo iliyokuwepo, ambapo hata hivyo Mkuu wa Mkoa huo anaiona mitambo hiyo kuwa sehemu ya tatizo kutokana kuwa katika teknolojia ya zamani.

“Nimekuwa nikifuatilia mara kwa mara, wanasema wanajaribu kufufua mitambo, lakini kinachosumbua pale mitambo ni ya zamani, katika mwelekeo wa kilimo kinachotumia zana za kisasa, hatuwezi kurudi kwenye majembe, tunahitaji teknolojia mpya, twende kwenye kutengeneza matrekta madogo, mapanga yaliyo bora zaidi,” anasema Kandoro.

Miongoni mwa mambo yanayotatiza wafuatiliaji wa sekta ya viwanda mkoani Mbeya ni iwapo serikali itatekeleza msimamo wake wa kunyang’anya viwanda na mashamba yaliyouzwa na ambayo hajaendelezwa kama ilivyokubaliwa katika mauziano.

Inaelezwa na watalaamu kuwa kisheria kuna kipengele cha ukomo wa muda (time limit), hapo ndipo anaweza akabanwa, iwapo hakipo basi anaweza kukwepa hatua hiyo ya serikali kwa kutumia kisingizio cha uwekezaji kwenye teknolojia ya kisasa, kwa madai ya kuchukua muda mrefu. Hata hivyo, wanabainisha kuwa mradi wowote ule ni lazima kuwe na ukomo wa muda.



zzk1.jpg Pichani ni baadhi ya vyuma chakavu ndani ya majengo ya ZZK Mbeya ambavyo ni sehemuya mitambo iliyokuwepo wakati wa uhai wake.

“Kama hawabanwi na sheria wanaweza kupiga chenga, lakini mradi wowote lazima kuwe na ukomo,” anasema mtaalamu wa kilimo, Kanyiki Sokolo alipozungumza na Raia Mwema.

Kiwanda cha Zana za Kilimo Mbeya ni miongoni mwa viwanda vikubwa vinne vilivyouzwa mkoani humo na tangu viuzwe havijaweza kuendelea na uzalishaji.
 
Ukitaka kujua tusivo makini kwa vipambele kama taifa, swala hilo ni mfano hai. Jembe la mkono ni muhimu katika familia yo yote. Kama kweli hakuna kiwanda cha jembe na panga, inasikitisha.
Mo Dewji anaagiza mapanga toka China na kubandika label ya 'Mo panga', it seems kuna incentives kubwa zaidi kuagiza toka nje kuliko kuzalisha ndani, labda tusubiri huo umeme wa bei nafuu toka Rufiji, pengine gharama za uzalishaji nchini zitashuka kiasi cha kuweza kushindana kwenye soko
 
Kwani China ama Uingereza wanaounda hayo majembe hadi sasa, hawajaendelea?

Na si kwamba Tanzania haijawahi kuwa na kiwanda cha majembe mfano: Ufi Dsm ama Zzk Mbeya nk nk, ambavyo vyote hivyo ukifuatilia namna ambavyo viliishia, lazima ukasirike.
 
Back
Top Bottom