Je, kuna haja ya Spika Ndugai kumjibu Mbowe juu ya tafsiri halisi ya Katiba na Kanuni kuhusu kiapo cha mbunge?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,754
139,558
Spika Ndugai alisema kanuni za bunge zinaruhusu mbunge kuapishwa nje ya ukumbi wa bunge jambo muhimu ni lazima mbunge aape mbele ya Spika wa bunge.

Mwenyekiti wa Chadema ambaye ni mbunge mstaafu na pia alikuwa mjumbe kwenye kamati ya kanuni amesema kanuni ile inakwenda kinyume cha katiba.

Kwamba katiba inatamka mbunge ataapishwa " before national assembly maana yake ikiwa mbele ya bunge zima.

Kufuatia sintofshamu hii je kuna haja ya Spika Ndugai kuitisha press na kutoa elimu itakayofunga huu mjadala?

Maendeleo hayana vyama!
 
Spika Ndugai alisema kanuni za bunge zinaruhusu mbunge kuapishwa nje ya ukumbi wa bunge jambo muhimu ni lazima mbunge aape mbele ya Spika wa bunge....
Mwanasheria Mkuu naye ni sehemu ya Bunge (a.k.a Bange baada ya uchafuzi mkuu). Huyu ndiye mtu sahihi wa kutoa ufafanuzi, ingawaje naye itategemea atashauriwa aseme nini kupitia mamlaka iliyopo juu yake.

Sent from my Nokia 2.1 using JamiiForums mobile app
 
Napata shida Sana na baadhi ya wasomi wa Tanzania wakishajiingiza kwenye siasa,hata kama wana PHD wanakuwa hana tofauti na mwanafeunzi wa chekechea.Tatizo nini hasa?
 
Kama kanuni zinaruhusu wanaweza hata kuapishana kwenye lodge na bar, sasa watu wapoteze muda kufungua ofisi za bunge halafu unaapisha covid-19 , kesho yake haina chama na ubunge si matumizi mabaya ya rasilimali
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom