Je, kuna haja ya Serikali kufanya marekebisho kwenye Sekta ya elimu?

escrow

JF-Expert Member
Sep 27, 2016
371
321
Kuanzia miaka ya 2000 kurudi nyuma Tanzania ni moja ya nchi zilizokabiliwa na upungufu mkubwa wa walimu katika ngazi zote za elimu kuanzia msingi mpaka Chuo kikuu.

Wakati wa awamu ya nne Serikali chini Benjamin W. Mkapa ilikuja na mpango kabambe kumaliza Tatizo la walimu nchini kwa kufanya yafuatayo:

1. Serikali ilianzisha vyuo vikuu vishiriki maalum kwa ajili ya kutoa mafunzo wa walimu na kuongeza idadi ya udahili kwenye fani ya Ualimu.

2. Ili kuvutia wanafunzi wasome fani ya Ualimu serikali ilitoa upendeleo maalum kwa wanafunzi wanaosomea Ualimu kwa kutoa asilimia kubwa ya mkopo.

3. Serikali ilibadilisha mfumo wa kupata ajira kwenye sekta ya Ualimu, ambapo wahimu walianza kuajiriwa moja kwa moja baada ya kuhitimu elimu yao.

4. Serikali iliboresha masilahi na makazi ya walimu ili kuwatia moyo kuipenda kazi yao. nk. nk.

5.Serikali ilianzisha mfumo unaitwa "crash programme" au a.k.a voda fasta lengo ni training ya muda mfupi ili kukidhi mahitaji ya walimu nchini

Kwa sasa walimu hawaajiriwi moja Kwa moja kama zamani ila wanatakiwa kuomba ajira kama sekta zingine tu.

Walimu waliohitimu wapo mitaani mwaka wa nne sasa na hawajui nini wafanye.

Je, serikali haioni umuhimu wa kupunguza udahili sekta ya elimu ili kuokoa bajeti ya nchi?
Je, Serikali haioni ulazima wa kuvifunga vyuo rasmi kwa ajili ya kozi za ualimu?

Na badala yake serikali ifanyie mabadiliko ya programme zinazotolewa katika vyuo hivyo kulingana na uhitaji, mf: badala ya kusomesha walimu kwenye vyuo hivyo wasomeshe madaktari na mainjinia, watalamu wa nishati hasa gesi na mafuta? Kuna haja gani kupeleka nje ya nchi watu wakasome masuala ya gesi na petrol, sio hasara kwa nchi wakati kuna vyuo vinasomesha watu wasiajirika?

Kwa sasa serikali inapeleka walimu wa degree hadi shule za msingi, Je, kuna haja ya kupunguza vyuo vya kati (diploma na certificate)? Au kubadili matumizi ya vyuo hivyo?

Nadhani wadau wa elimu wanaweza kuangalia mfumo wa sera yetu ya elimu nchini, sera ifanyiwe marekebisho ili iwe na tija nchi.

Naomba kuwasilisha wadau!! Karibuni sana.
 
Tatizo sera ya elimu inabadilika kila kukichwa na matamko ya kisiasa ndio yanavuruga kabisa
 
Back
Top Bottom