Je, kuna haja ya majeshi ya SADC kuingia Msumbiji kupambana na Jihadist/Kundi la kigaidi lililoishinda serikari ya Msumbiji?

jiwekuu770

JF-Expert Member
Feb 12, 2015
2,247
1,634
Miaka kadhhaa tu majeshi ya SADC yaliingia DRC Na kufanikiwa kuliteleteza Kundi la waasi la M23 kwa muda mfupi ..ambalo lilishaishinda serikari ya DRC.

Tangu mwaka 2017 serikali ya msumbiji imeshuhudia mashambuliz toka kwa wanamgambo wa kigaidi kaskazin mwa msumbiji

Pia Kundi Hilo limefanya mashambulizi hayo baadhi ya vijij vya nchi jiran.

Kwa kutambua kua Kundi Hilo litadestabilise nchi za SADC na kuleta machafuko kwa nchi jumuiya Kama ilivo kwa West Africa ambapo Boko haramu wamedhoofisha Aman ya nchi hizo had central Africa Chad!!

images%20(2).jpg

Karibu kwa maoni
 
Weng tunashindwa kutofautisha kati M23 na islamic states hao ni balaa hata kule Syria walifanikiwa kuiotoa baada ya dunia mzima kuwashambulia NATO, iran Russia na Israel hao SADC wala hawawezi
 
..hapo Msumbiji wanatakiwa wapeleke jeshi la ANGOLA.

..Katika nchi za kusini mwa afrika Angola ndio wenye jeshi lenye uzoefu wa kulinda vitega uchumi kama visima vya mafuta na gesi.

..Uzoefu wa Angola unatoka na ukweli kwamba wamekuwa wakilinda visima vya mafuta ktk kisiwa cha Cabinda, na mradi wa lng ktk eneo la Soyo.
 
Hawa jamaa wakiachwa waendelee kujiimarisha itakuwa ni maficho ya majambazi wanaosakwa kwa udi na uvumba kwenye nchi zao hata mimi sasa hivi nikiua mtu nitakwenda kujificha huko
 
Kama wewe ni mtanzania,na huna interest binafsi kwenye vita,basi nitaendelea kuamini kuwa uwezo wa kufikiri ni tatizo kubwa sana hasa nchi zetu hizi za waafrika
Miaka kadhhaa tu majeshi ya SADC yaliingia DRC Na kufanikiwa kuliteleteza Kundi la waasi la M23 kwa muda mfupi ..ambalo lilishaishinda serikari ya DRC.

Tangu mwaka 2017 serikali ya msumbiji imeshuhudia mashambuliz toka kwa wanamgambo wa kigaidi kaskazin mwa msumbiji

Pia Kundi Hilo limefanya mashambulizi hayo baadhi ya vijij vya nchi jiran.

Kwa kutambua kua Kundi Hilo litadestabilise nchi za SADC na kuleta machafuko kwa nchi jumuiya Kama ilivo kwa West Africa ambapo Boko haramu wamedhoofisha Aman ya nchi hizo had central Africa Chad!!

Karibu kwa maoni
 
Waulize Kenya nini kimawapata dhidi ya Al- Shaba.Islamic fundamentalist na waasi kama M 23 ni vitu viwili tofauti.Kama Nigeria imeshindwa kupambana na Boko haramu sisi uchumi duni tutaweza kuwashambulia IS? ikianzishwa hio vita tegemea majanga makubwa kutokea TZ, kumbuka hata TZ kuna waislamu wenye itikadi Kali ila hawajapata tu kaupenyo.Tuendelee kulinda mipaka kila nchi ipambne na hali yake.
 
Back
Top Bottom