Je, Kuna haja ya kuwa na bodi maalum kwa ajili ya kusimamia watoa huduma za kiroho?

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
34,671
40,912
Wakuu,

Kutokana na hali halisi katika jamii zetu ya ongezeko la nyumba kadhaa za ibada, nimeona sio vibaya kuleta kwenu hili jambo kwa mjadala.

Natambua kuwa Serikali haina dini, ingawa kwa namna flani inajihusisha na maswala ya dini kwani imeweka sheria ya taasisi za kijamii (The Societies Ordinance,1954).

Msajili wa Taasisi za kijamii ( Registrar of societies) ndio mwenye jukumu la kuregulate taasisi zote za kijamii ikiwemo zile za kidini. Huyu atasimamia kuanzishwa na kuendeshwa kwa taasisi husika kulingana na sheria za nchi.

Ukiachana na huyo Registrar of Societies, naona kuna haja ya kuwa na bodi maalum ambayo hii itajihusisha tu na wale watoa huduma za kiroho, kwa maana kwamba utakuwa ikiwasajili na kuwasimamia utendaji kazi wao na pia inapobidi kutetea maslahi yao.

Umuhimu wa kuanzishwa kwa bodi hiyo, kutasaidia kuifanya huduma ya kiroho kutolewa na watu ambao ni qualified, najua kuwa nature ya huduma ya kiroho ni "wito" na kwamba elimu sio muhimu sana lakini ipo haja sasa ya kuiboresha huduma hiyo ikawa inatolewa na watu waliohitimu elimu flani ya dini toka taasisi zinazotambulika na sio kila mtu anayejisikia kuifanya kazi hiyo.

Inafikia mahali mtu anadai anawito, anakusanya watu na kuendelea kujinufaisha. Naomba Mungu anisamehe kama nitakuwa nimevuka mipaka, lakini nadhani Serikali inayo wajibu wa kutunza roho za raia wake pia ukiachana na huduma za kimwili inazotoa.

Serikali inayo wajibu wa kuhakikisha kuwa aina ya mafundisho Raia wake wanayopata ni mafundisho sahihi.

Serikali ya aina hii itakuwa imefanya jambo jema kwa raia na kupata thawabu kwa Mungu.

Wanasheria wanayo TLS, Wahasibu NBAA, Wahandisi CRB, kwanini hawa watoa huduma za kiroho wasiwe na bodi yao??

Naamini kabisa sio kila mtu anauwezo wa kutoa huduma ya kiroho, mtu unaona kabisa kuwa mafundisho mengine sio sahihi.

Wapo watakao sema kuwa huko kutakuwa kuingilia imani za watu, lakini ipo haja ya kuregulate aina ya mafundisho ambayo watu wanayapata, na hii bodi itatusaidia mno.

Karibuni kwa mjadala.
 
well said..kuna haja ya serikali kulifanya hili..kuna kikundi fulani miaka kadhaa ya nyuma kilienda airport kikidai ndege ya bure ili kiende sijui nchi ya ahadi ..asa hii si ilikuwa dharau kwa serikali??
 
Umuhimu upo sana,tena wangeachana na hata na hayo mambo ya sijui bodi za korosho sijui nini,huko kwny mambo ya kiroho kuna mambo mengi sana yanaendelea.

Kuna jamaa mmoja wa hapa E/Africa yeye hata hakuunda bodi aliamka tu na wenzake wakaanza kubomoa makanisa kama 8000 hivi wasiyoyaelewa elewa na wakaweka sheria huna degree ya theology,huna kanisa lenye Sound Proof,huna vifaa vya kuokoa watu incase kuna janga limetokea humo kanisani hakuna kibali cha kufungua kanisa,full stop.

Tatizo siasa zitakua nyingi sana,bodi ikiundwa ikaanza kufanya kazi yake litaibuka kundi moja linapinga jingine linaunga mkono na yatachukua tena mtizamo wa kisiasa/kichama itakua tena Ccm vs Chadema.
 
Kwa tukio hili la Kilimanjaro , kuna haja ya kuharakisha hiyo Board.
 
Wakuu,

Kutokana na hali halisi katika jamii zetu ya ongezeko la nyumba kadhaa za ibada, nimeona sio vibaya kuleta kwenu hili jambo kwa mjadala.

Natambua kuwa Serikali haina dini, ingawa kwa namna flani inajihusisha na maswala ya dini kwani imeweka sheria ya taasisi za kijamii (The Societies Ordinance,1954).

Msajili wa Taasisi za kijamii ( Registrar of societies) ndio mwenye jukumu la kuregulate taasisi zote za kijamii ikiwemo zile za kidini. Huyu atasimamia kuanzishwa na kuendeshwa kwa taasisi husika kulingana na sheria za nchi.

Ukiachana na huyo Registrar of Societies, naona kuna haja ya kuwa na bodi maalum ambayo hii itajihusisha tu na wale watoa huduma za kiroho, kwa maana kwamba utakuwa ikiwasajili na kuwasimamia utendaji kazi wao na pia inapobidi kutetea maslahi yao.

Umuhimu wa kuanzishwa kwa bodi hiyo, kutasaidia kuifanya huduma ya kiroho kutolewa na watu ambao ni qualified, najua kuwa nature ya huduma ya kiroho ni "wito" na kwamba elimu sio muhimu sana lakini ipo haja sasa ya kuiboresha huduma hiyo ikawa inatolewa na watu waliohitimu elimu flani ya dini toka taasisi zinazotambulika na sio kila mtu anayejisikia kuifanya kazi hiyo.

Inafikia mahali mtu anadai anawito, anakusanya watu na kuendelea kujinufaisha. Naomba Mungu anisamehe kama nitakuwa nimevuka mipaka, lakini nadhani Serikali inayo wajibu wa kutunza roho za raia wake pia ukiachana na huduma za kimwili inazotoa.

Serikali inayo wajibu wa kuhakikisha kuwa aina ya mafundisho Raia wake wanayopata ni mafundisho sahihi.

Serikali ya aina hii itakuwa imefanya jambo jema kwa raia na kupata thawabu kwa Mungu.

Wanasheria wanayo TLS, Wahasibu NBAA, Wahandisi CRB, kwanini hawa watoa huduma za kiroho wasiwe na bodi yao??

Naamini kabisa sio kila mtu anauwezo wa kutoa huduma ya kiroho, mtu unaona kabisa kuwa mafundisho mengine sio sahihi.

Wapo watakao sema kuwa huko kutakuwa kuingilia imani za watu, lakini ipo haja ya kuregulate aina ya mafundisho ambayo watu wanayapata, na hii bodi itatusaidia mno.

Karibuni kwa mjadala.
Ndio naunga hoja mkono bodi ziwepo tz madhebu yanazi kua menge na mitume na manaabii wanazidi ongezeka kwa asilimia mia naunga mkono tunaweza kua taifa la mfano bodi ikiwepo na wengine waje kuiga kwetu haiwezekani vitabu vitakatifu vitumike vya aina moja ila ndani ya watoa huduma kuwe na sarakasi za kila aina
 
Umuhimu upo sana,tena wangeachana na hata na hayo mambo ya sijui bodi za korosho sijui nini,huko kwny mambo ya kiroho kuna mambo mengi sana yanaendelea.

Kuna jamaa mmoja wa hapa E/Africa yeye hata hakuunda bodi aliamka tu na wenzake wakaanza kubomoa makanisa kama 8000 hivi wasiyoyaelewa elewa na wakaweka sheria huna degree ya theology,huna kanisa lenye Sound Proof,huna vifaa vya kuokoa watu incase kuna janga limetokea humo kanisani hakuna kibali cha kufungua kanisa,full stop.

Tatizo siasa zitakua nyingi sana,bodi ikiundwa ikaanza kufanya kazi yake litaibuka kundi moja linapinga jingine linaunga mkono na yatachukua tena mtizamo wa kisiasa/kichama itakua tena Ccm vs Chadema.

Well said

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ndio naunga hoja mkono bodi ziwepo tz madhebu yanazi kua menge na mitume na manaabii wanazidi ongezeka kwa asilimia mia naunga mkono tunaweza kua taifa la mfano bodi ikiwepo na wengine waje kuiga kwetu haiwezekani vitabu vitakatifu vitumike vya aina moja ila ndani ya watoa huduma kuwe na sarakasi za kila aina
Mpaka maafa yatokee kama hivi ndio tunaanza kuangalia, inatakiwa tuwe proaktive.
 
Back
Top Bottom