Je kuna haja ya kupeleka watuhumiwa wa rushwa mahakamani?

Kakende

JF-Expert Member
Aug 18, 2012
2,741
1,225
Kwa muda wa miaka kadhaa sasa Tanzania tafiti zinaonesha kuwa kinara namba moja wa rushwa ni idara ya polisi ikifuatiwa na Mahakama. Kimsingi kazi ya polisi ni kuhakikisha inawakamata na kuwafikisha mahakamani wale wote wanaovunja sheria za nchi.

Na kazi ya mahakama ni kutoa haki kwa watuhumiwa. Sasa swala la kujiuliza, kama idara hizi mbili ndizo zinazosimamia sheria za nchi lakini bado ndio zinaongoza kwa kupokea rushwa, hivi kweli wana uhalali wa kutoa hukumu kwa wala rushwa au bora turudie zile hukumu zetu za kimila za kuchapana viboko?
 
Top Bottom